Hesabu 26 - Swahili Revised Union VersionHesabu ya kizazi kipya 1 Ikawa baada ya hilo pigo, BWANA akanena na Musa na Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, na kuwaambia, 2 Fanya hesabu ya jumuiya yote ya wana wa Israeli, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi, kwa nyumba za baba zao, hao wote katika Israeli wawezao kutoka kuenenda vitani. 3 Kisha Musa na Eleazari kuhani wakanena nao katika nchi tambarare za Moabu karibu na mto wa Yordani, huko Yeriko, wakawaambia, 4 Fanyeni hesabu ya watu, kuanzia umri wa miaka ishirini, na zaidi; kama BWANA alivyomwagiza Musa na wana wa Israeli, hao waliotoka nchi ya Misri. 5 Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli, wana wa Reubeni; wa Hanoki, jamaa ya Wahanoki; na wa Palu, jamaa ya Wapalu; 6 na wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; na wa Karmi, jamaa ya Wakarmi. 7 Hizi ndizo jamaa za Wareubeni; na hao waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na tatu, mia saba na thelathini. 8 Na wana wa Palu; Eliabu. 9 Na wana wa Eliabu; Nemueli, na Dathani, na Abiramu. Hawa ndio Dathani na Abiramu waliochaguliwa na mkutano, ambao walishindana na Musa na Haruni katika mkutano wa Kora, hapo waliposhindana na BWANA; 10 nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza pamoja na Kora, mkutano huo ulipokufa; wakati moto ulipowateketeza watu mia mbili na hamsini, nao wakawa ishara. 11 Hata hivyo, hao wana wa Kora hawakufa. 12 Na wana wa Simeoni kwa jamaa zao; wa Yemueli, jamaa ya Wayemueli; wa Yamini, jamaa ya Wayamini; na Yakini, jamaa ya Wayakini; 13 wa Sohari, jamaa ya Wasohari; wa Shauli, jamaa ya Washauli. 14 Hawa ndizo jamaa wa Wasimeoni, watu elfu ishirini na mbili na mia mbili. 15 Na wana wa Gadi kwa jamaa zao; wa Sifoni, jamaa ya Wasifoni; wa Hagi, jamaa ya Wahagi; wa Shuni, jamaa ya Washuni; 16 wa Ezboni, jamaa ya Waezboni; wa Eri, jamaa ya Waeri; 17 wa Arodi, jamaa ya Waarodi; wa Areli, jamaa ya Waareli. 18 Hawa ndio jamaa wa wana wa Gadi kama waliohesabiwa kwao, elfu arubaini na mia tano. 19 Na wana wa Yuda, Eri na Onani; na hao Eri na Onani wakafa katika nchi ya Kanaani. 20 Na wana wa Yuda kwa jamaa zao; wa Shela, jamaa ya Washela; wa Peresi, jamaa ya Waperesi; wa Zera, jamaa ya Wazera. 21 Na wana wa Peresi walikuwa; wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; wa Hamuli, jamaa ya Wahamuli. 22 Hawa ndio jamaa wa Yuda kama waliohesabiwa kwao, elfu sabini na sita na mia tano. 23 Na wana wa Isakari kwa jamaa zao; wa Tola, jamaa ya Watola; wa Puva, jamaa ya Wapuva; 24 wa Yashubu, jamaa ya Wayashubu; wa Shimroni, jamaa ya Washimroni. 25 Hawa ndio jamaa wa Isakari kama waliohesabiwa kwao, elfu sitini na nne na mia tatu. 26 Na wana wa Zabuloni kwa jamaa zao; wa Seredi, jamaa ya Waseredi; wa Eloni, jamaa ya Waeloni; wa Yaleeli, jamaa ya Wayaleeli. 27 Hawa ndio jamaa wa Wazabuloni kama waliohesabiwa kwao, elfu sitini na mia tano. 28 Na wana wa Yusufu kwa jamaa zao; Manase na Efraimu. 29 Wana wa Manase; wa Makiri, jamaa ya Wamakiri; na Makiri akamzaa Gileadi; wa Gileadi, jamaa ya Wagileadi. 30 Hawa ndio wana wa Gileadi; wa Abiezeri, jamaa ya Waabiezeri; wa Heleki, jamaa ya Waheleki; 31 na wa Asrieli, jamaa ya Waasrieli; na wa Shekemu, jamaa ya Washekemu; 32 na wa Shemida, jamaa ya Washemida; na wa Heferi, jamaa ya Waheferi. 33 Na Selofehadi mwana wa Heferi hakuwa na watoto wa kiume, isipokuwa wa kike; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya, Mala, na Nuhu, na Hogla, na Milka, na Tirza. 34 Hawa ndizo jamaa wa Manase; na waliohesabiwa kwao walikuwa ni elfu hamsini na mbili na mia saba. 35 Na wana wa Efraimu kwa jamaa zao; wa Shuthela, jamaa ya Washuthela; wa Beredi, jamaa ya Waberedi; wa Tahathi, jamaa ya Watahathi. 36 Na wana wa Shuthela ni hawa; wa Erani, jamaa ya Waerani. 37 Hawa ndio jamaa wa wana wa Efraimu kama waliohesabiwa kwao, elfu thelathini na mbili na mia tano. Hao ndio wana wa Yusufu kwa jamaa zao. 38 Na wana wa Benyamini kwa jamaa zao; wa Bela, jamaa ya Wabela; na wa Ashbeli, jamaa ya Waashbeli; wa Ahiramu, jamaa ya Waahiramu; 39 wa Shufamu, jamaa ya Washufamu; wa Hufamu, jamaa ya Wahufamu. 40 Na wana wa Bela walikuwa Ardi na Naamani; wa Ardi, jamaa ya Waardi; wa Naamani, jamaa ya Wanaamani. 41 Hao ndio wana wa Benyamini kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na tano na mia sita. 42 Na wana wa Dani ni hawa kwa jamaa zao; wa Shuhamu, jamaa ya Washuhamu. Hizi ndizo jamaa za Dani kwa jamaa zao. 43 Jamaa zote za Washuhamu, kama waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu sitini na nne na mia nne. 44 Na wana wa Asheri kwa jamaa zao; wa Imna, jamaa ya Waimna; wa Ishvi jamaa ya Waishvi; wa Beria, jamaa ya Waberia. 45 Wa wana wa Beria; wa Heberi, jamaa ya Waheberi; wa Malkieli, jamaa ya Wamalkieli. 46 Na jina la binti wa Asheri aliitwa Sera. 47 Hawa ndio jamaa wa wana wa Asheri kama waliohesabiwa kwao, elfu hamsini na tatu na mia nne. 48 Na wana wa Naftali kwa jamaa zake; wa Yaseeli, jamaa ya Wayaseeli; na wa Guni, jamaa ya Waguni; 49 wa Yeseri, jamaa ya Wayeseri, wa Shilemu jamaa ya Washilemu. 50 Hawa ndio jamaa wa Naftali kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na tano na mia nne. 51 Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli, elfu mia sita na moja, mia saba na thelathini (601,730). 52 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 53 Watu hawa watagawiwa nchi hiyo iwe urithi wao, kulingana na idadi yao ilivyo. 54 Hao waliozidi hesabu yao utawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka hesabu yao, utawapa urithi kama upungufu wao; kila mtu kama watu wake walivyohesabiwa, ndivyo atakavyopewa urithi wake. 55 Lakini nchi itagawanywa kwa kura; kwa majina ya makabila ya baba zao, ndivyo watakavyopata urithi. 56 Kama kura itakavyokuwa, ndivyo urithi wao utakavyogawanywa kati yao, hao wengi na hao wachache. 57 Na hao waliohesabiwa katika Walawi kwa jamaa zao ni hawa; wa Gershoni, jamaa ya Wagershoni; na wa Kohathi, jamaa ya Wakohathi; na wa Merari, jamaa ya Wamerari. 58 Hizi ndizo jamaa za Lawi; jamaa ya Walibni, na jamaa ya Wahebroni, na jamaa ya Wamala, na jamaa ya Wamushi jamaa ya Wakora. Na Kohathi alimzaa Amramu. 59 Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi, binti wa Lawi, ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amramu Haruni, na Musa, na Miriamu dada yao. 60 Tena kwake Haruni walizaliwa hawa, Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. 61 Tena Nadabu na Abihu wakafa, hapo waliposongeza moto wa kigeni mbele za BWANA. 62 Na hao waliohesabiwa kwao walikuwa elfu ishirini na tatu, kila mwanamume tangu huyo aliyepata umri wa mwezi mmoja, na zaidi; kwa kuwa hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli, kwa sababu hawakupewa urithi katika wana wa Israeli. 63 Hao ndio waliohesabiwa na Musa na Eleazari kuhani; ambao waliwahesabu wana wa Israeli katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko. 64 Lakini katika watu hao hapakuwa na mtu hata mmoja wa wale waliohesabiwa na Musa na Haruni kuhani; waliowahesabu wana wa Israeli katika bara ya Sinai. 65 Kwa kuwa BWANA alisema juu yao, Hapana budi watakufa nyikani. Napo hapakusalia mtu mmoja miongoni mwao, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya