Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hesabu 26:54 - Swahili Revised Union Version

54 Hao waliozidi hesabu yao utawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka hesabu yao, utawapa urithi kama upungufu wao; kila mtu kama watu wake walivyohesabiwa, ndivyo atakavyopewa urithi wake.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

54 Kabila kubwa litapewa sehemu yao kubwa na dogo litapewa sehemu yao ndogo. Kila kabila litapewa urithi wake kulingana na idadi ya watu wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

54 Kabila kubwa litapewa sehemu yao kubwa na dogo litapewa sehemu yao ndogo. Kila kabila litapewa urithi wake kulingana na idadi ya watu wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

54 Kabila kubwa litapewa sehemu yao kubwa na dogo litapewa sehemu yao ndogo. Kila kabila litapewa urithi wake kulingana na idadi ya watu wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

54 Kundi kubwa zaidi lipe urithi mkubwa zaidi, na kundi dogo zaidi lipewe urithi mdogo zaidi; kila kundi litapokea urithi wake kulingana na hesabu ya wale walioorodheshwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

54 Kundi kubwa zaidi lipe urithi mkubwa zaidi, na kundi dogo zaidi lipewe urithi mdogo zaidi; kila kundi litapokea urithi wake kulingana na hesabu ya wale walioorodheshwa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

54 Hao waliozidi hesabu yao utawapa urithi zaidi, na hao waliopungua hesabu yao, utawapa urithi kama upungufu wao; kila mtu kama watu wake walivyohesabiwa, ndivyo atakavyopewa urithi wake.

Tazama sura Nakili

Hesabu 26:54
7 Marejeleo ya Msalaba  

Watu hawa watagawiwa nchi hiyo iwe urithi wao, kulingana na idadi yao ilivyo.

Atarothi, na Diboni, na Yazeri, na Nimra, na Heshboni, na Eleale, na Sebamu, na Nebo na Beoni,

Wakasema, Kama tumepata kibali mbele ya macho yako, sisi watumishi wako na tupewe nchi hii iwe milki yetu; usituvushe mto wa Yordani.

Nanyi mtairithi nchi kwa kufanya kura, kama jamaa zenu zilivyo; hao walio wengi mtawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka utawapa kama kupunguka kwao; mahali popote kura itakapomwangukia mtu yeyote, mahali hapo ni pake; mtarithi kama makabila ya baba zenu yalivyo.

Tena katika miji mtakayotoa ya hiyo milki ya wana wa Israeli, katika hao walio wengi mtatwaa miji mingi; na katika hao walio wachache mtatwaa miji michache; kila mtu kama ulivyo urithi wake atakaourithi, atawapa Walawi katika miji yake.

Kisha wana wa Yusufu wakanena na Yoshua, wakasema, Kwa nini umenipa mimi sehemu moja tu na fungu moja kuwa ni urithi wangu, kwa kuwa mimi ni taifa kubwa la watu, kwa sababu BWANA amenibariki hata hivi sasa?

Huo urithi wa hao wana wa Simeoni ulitoka katika fungu la wana wa Yuda; kwa maana hilo fungu la wana wa Yuda lilikuwa ni kubwa mno kwao; kwa hiyo wana wa Simeoni walikuwa na urithi katikati ya urithi wao.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo