Methali 6:6 - Swahili Revised Union Version Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ewe mvivu! Hebu ukamchungulie sisimizi, fikiria namna yake ya kuishi ukapate hekima. Biblia Habari Njema - BHND Ewe mvivu! Hebu ukamchungulie sisimizi, fikiria namna yake ya kuishi ukapate hekima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ewe mvivu! Hebu ukamchungulie sisimizi, fikiria namna yake ya kuishi ukapate hekima. Neno: Bibilia Takatifu Ewe mvivu, mwendee mchwa; zitafakari njia zake ukapate hekima! Neno: Maandiko Matakatifu Ewe mvivu, mwendee mchwa; zitafakari njia zake ukapate hekima! BIBLIA KISWAHILI Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. |
Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.
Njia ya mtu mvivu ni kama boma la miiba; Bali mapito yao wenye unyofu hufanyika njia kuu.
Ng'ombe amjua bwana wake, Na punda ajua kibanda cha bwana wake; Bali Israeli hajui, watu wangu hawafikiri.
Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za BWANA.
Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kuliko hao?