Isaya 2:11 - Swahili Revised Union Version Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku yaja ambapo kiburi cha watu kitashushwa, majivuno ya kila mtu yatavunjwa; na Mwenyezi-Mungu peke yake atatukuzwa siku hiyo. Biblia Habari Njema - BHND Siku yaja ambapo kiburi cha watu kitashushwa, majivuno ya kila mtu yatavunjwa; na Mwenyezi-Mungu peke yake atatukuzwa siku hiyo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku yaja ambapo kiburi cha watu kitashushwa, majivuno ya kila mtu yatavunjwa; na Mwenyezi-Mungu peke yake atatukuzwa siku hiyo. Neno: Bibilia Takatifu Macho ya mtu mwenye majivuno yatanyenyekezwa na kiburi cha wanadamu kitashushwa, Mwenyezi Mungu peke yake ndiye atakayetukuzwa siku hiyo. Neno: Maandiko Matakatifu Macho ya mtu mwenye majivuno yatanyenyekezwa na kiburi cha wanadamu kitashushwa, bwana peke yake ndiye atakayetukuzwa siku hiyo. BIBLIA KISWAHILI Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo. |
Basi, itakuwa, Bwana atakapokuwa ameitimiza kazi yake yote juu ya mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitamwadhibu matunda ya kiburi cha moyo wake mfalme wa Ashuru, na majivuno ya macho yake.
Na katika siku hiyo utasema, Ee BWANA, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo.
Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa, Litangazeni jina lake kuwa limetukuka.
Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayashusha chini majivuno yao walio wakali;
Na majivuno ya mwanadamu yatainamishwa, na kiburi cha watu kitashushwa; naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.
BWANA wa majeshi ndiye aliyefanya shauri hili, ili kuharibu kiburi cha utukufu wote, na kuwaaibisha watu wa duniani wote pia.
Tena itakuwa katika siku hiyo, BWANA ataliadhibu jeshi la mahali palipo juu katika mahali palipo juu, na wafalme wa dunia katika dunia;
Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye BWANA tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.
Siku ile wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda; Sisi tunao mji ulio na nguvu; Ataamuru wokovu kuwa kuta na maboma.
Katika siku ile BWANA wa majeshi atakuwa ni taji la fahari, na kilemba cha uzuri, kwa mabaki ya watu wake.
Na katika siku hiyo viziwi watasikia maneno ya hicho kitabu, na macho ya vipofu yataona katika upofu na katika giza.
Kwa ajili ya hayo BWANA atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana BWANA ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.
Naye atatoa mvua juu ya mbegu zako, upate kuipanda nchi hii; na mkate wa mazao ya nchi, nayo itasitawi na kuzaa tele; katika siku hiyo ng'ombe wako watakula katika malisho mapana.
Ni nani uliyemshutumu na kumtukana? Umeinua sauti yako juu ya nani, na kuinua macho yako juu? Juu ya Mtakatifu wa Israeli.
Na siku hiyo wanawake saba watamshika mwanaume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.
Kwa hiyo watu wangu watalijua jina langu kwa hiyo watajua siku ile ya kuwa mimi ndimi ninenaye; tazama ni mimi.
Je! Urithi wangu umekuwa kwangu kama ndege mwenye madoadoa? Ndege wakali wamemzunguka pande zote? Nendeni, wakusanyeni pamoja wanyama wote wa mwituni, waleteni ili wale.
bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni BWANA, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema BWANA,
Basi, mwanadamu, tabiri, umwambie Gogu, Bwana MUNGU asema hivi; Katika siku ile watu wangu, Israeli, watakapokaa salama, hutapata habari?
Kwa maana katika wivu wangu, na katika moto wa ghadhabu yangu, nimenena, Hakika katika siku ile kutakuwako tetemeko kubwa katika nchi ya Israeli;
Tena, itakuwa katika siku hiyo, nitampa Gogu pa kuzikia katika Israeli, bonde la wapitao, upande wa mashariki wa bahari; nalo litawazuia wapitao; na huko watamzika Gogu na jamii ya watu wake wote; nao wataliita, Bonde la Hamon-Gogu.
Basi, nyumba ya Israeli watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wao, tangu siku hiyo na baadaye.
Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadneza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;
Nami siku hiyo nitafanya agano na wanyama wa mashamba kwa ajili yao, tena na ndege wa angani, tena na wadudu wa nchi; nami nitavivunja upinde na upanga na silaha vitoke katika nchi, nami nitawalalisha salama salimini.
Tena itakuwa siku hiyo, mimi nitaitika, asema BWANA; nitaziitikia mbingu, nazo zitaiitikia nchi;
Tena itakuwa siku ile, ya kwamba milima itadondoza divai tamu, na vilima vitatiririka maziwa, na vijito vyote vya Yuda vitatoa maji tele; na chemchemi itatokea katika nyumba ya BWANA, na kulinywesha bonde la Shitimu.
Siku hiyo nitaiinua tena maskani ya Daudi iliyoanguka, na kuziba mahali palipobomoka; nami nitayainua magofu yake, na kuyajenga kama siku za kale;
Siku hiyo, je! Sitawaangamiza watu wenye akili katika Edomu, na wenye ufahamu katika kilima cha Esau? Asema BWANA.
Basi BWANA asema hivi, Angalia, nakusudia jambo baya juu ya jamaa hii, ambalo hamtazitoa shingo zenu, wala hamtakwenda kwa kiburi; kwa maana ni wakati mbaya.
Katika siku ile, asema BWANA, nitamkusanya yeye achechemeaye, nami nitamrudisha yeye aliyefukuzwa, na yeye niliyemtesa.
Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema BWANA, nitawakatilia mbali farasi wako watoke kati yako, nami nitayaharibu magari yako ya vita;
Siku ile hutaaibishwa kwa matendo yako yote uliyoniasi; maana hapo nitawaondoa watu wako wanaojigamba na kujivuna, wasiwe kati yako, wala hutatakabari tena katika mlima wangu mtakatifu.
Na BWANA, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo, Kama kundi la watu wake; Kwa maana watakuwa kama vito vya taji, Vikimetameta juu ya nchi yake.
Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuri; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu).
Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.