Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yoeli 3:18 - Swahili Revised Union Version

18 Tena itakuwa siku ile, ya kwamba milima itadondoza divai tamu, na vilima vitatiririka maziwa, na vijito vyote vya Yuda vitatoa maji tele; na chemchemi itatokea katika nyumba ya BWANA, na kulinywesha bonde la Shitimu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 “Wakati huo, milima itatiririka divai mpya, na vilima vitatiririka maziwa. Vijito vyote vya Yuda vitajaa maji; chemchemi itatokea nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu, na kulinywesha bonde la Shitimu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 “Wakati huo, milima itatiririka divai mpya, na vilima vitatiririka maziwa. Vijito vyote vya Yuda vitajaa maji; chemchemi itatokea nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu, na kulinywesha bonde la Shitimu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 “Wakati huo, milima itatiririka divai mpya, na vilima vitatiririka maziwa. Vijito vyote vya Yuda vitajaa maji; chemchemi itatokea nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu, na kulinywesha bonde la Shitimu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 “Katika siku hiyo milima itadondosha divai mpya, na vilima vitatiririka maziwa; mabonde yote ya Yuda yatatiririka maji. Chemchemi itatiririka kutoka nyumba ya Mwenyezi Mungu na kunywesha Bonde la Shitimu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 “Katika siku hiyo milima itadondosha divai mpya, na vilima vitatiririka maziwa; mabonde yote ya Yuda yatatiririka maji. Chemchemi itatiririka kutoka kwenye nyumba ya bwana na kunywesha Bonde la Shitimu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

18 Tena itakuwa siku ile, ya kwamba milima itadondoza divai tamu, na vilima vitatiririka maziwa, na vijito vyote vya Yuda vitatoa maji tele; na chemchemi itatokea katika nyumba ya BWANA, na kulinywesha bonde la Shitimu.

Tazama sura Nakili

Yoeli 3:18
18 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati hatua zangu zilipokuwa zikioshwa kwa siagi, Nalo jabali liliponimiminia mito ya mafuta!

Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye Juu.

nami nimeshuka ili niwaokoe kutoka kwa mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hadi nchi njema, kisha pana; nchi itiririkayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.

Na juu ya kila mlima mrefu, na juu ya kila kilima kilichoinuka, itakuwapo mito na vijito vya maji, katika siku ya machinjo makuu itakapoanguka minara.

Ndipo mtu aliye kilema atarukaruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani.

Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa;

Dondokeni, enyi mbingu, toka juu, Mawingu na yamwage haki; Nchi na ifunuke, ili kutoa wokovu, Nayo itoe haki ikamee pamoja; Mimi, BWANA, nimeiumba.

Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila gharama.

mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa ya faraja zake, mpate kukama, na kufurahiwa kwa wingi wa utukufu wake.

Nao watakuja, na kuimba katika mlima Sayuni, wataukimbilia wema wa BWANA, nafaka, na divai, na mafuta, na wachanga wa kondoo na wa ng'ombe; na roho zao zitakuwa kama bustani iliyotiwa maji; wala hawatahuzunika tena kabisa.

Enyi watu wangu, kumbukeni sasa alivyouliza Balaki, mfalme wa Moabu, na alivyojibu Balaamu, mwana wa Beori; kumbukeni yaliyotukia toka Shitimu hadi Gilgali, mpate kuyajua matendo ya haki ya BWANA.

Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba maji yaliyo hai yatatoka katika Yerusalemu; nusu yake itakwenda upande wa bahari ya mashariki, na nusu yake upande wa bahari ya magharibi; wakati wa joto na wakati wa baridi itakuwa hivi.

Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo