Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zekaria 9:16 - Swahili Revised Union Version

16 Na BWANA, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo, Kama kundi la watu wake; Kwa maana watakuwa kama vito vya taji, Vikimetameta juu ya nchi yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Wakati huo, Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, atawaokoa, maana wao ni kundi lake; nao watang'aa katika nchi yake kama mawe ya thamani katika taji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Wakati huo, Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, atawaokoa, maana wao ni kundi lake; nao watang'aa katika nchi yake kama mawe ya thamani katika taji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Wakati huo, Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, atawaokoa, maana wao ni kundi lake; nao watang'aa katika nchi yake kama mawe ya thamani katika taji.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Mwenyezi Mungu, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo kama kundi la watu wake. Watang’ara katika nchi yake kama vito vya thamani kwenye taji.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 bwana Mwenyezi Mungu wao atawaokoa siku hiyo kama kundi la watu wake. Watang’aa katika nchi yake kama vito vya thamani kwenye taji.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 Na BWANA, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo, Kama kundi la watu wake; Kwa maana watakuwa kama vito vya taji, Vikimetameta juu ya nchi yake.

Tazama sura Nakili




Zekaria 9:16
25 Marejeleo ya Msalaba  

Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.


Na vile vito vitakuwa sawasawa na majina ya wana wa Israeli, kumi na viwili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora kwa mihuri kila kimoja sawasawa na jina lake, vitakuwa vya hayo makabila kumi na mawili.


Nawe utatwaa vito viwili vya shohamu rangi ya chanikiwiti, nawe utachora juu yake majina ya wana wa Israeli;


Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na fidia yake i mbele zake.


Nami nitaifanya minara yako ya akiki nyekundu, na malango yako ya almasi, na mipaka yako yote ya mawe yapendezayo.


Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha katika nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa BWANA, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli.


Na mataifa wataijia nuru yako, Na wafalme kuujia mwanga wa mapambazuko yako.


Nawe utakuwa taji la uzuri katika mkono wa BWANA, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.


Nami nitakusanya mabaki ya kundi langu, katika nchi zile zote nilizowafukuza, nami nitawaleta tena mazizini mwao; nao watazaa na kuongezeka.


Lisikieni neno la BWANA, enyi mataifa, litangazeni visiwani mbali; mkaseme, Aliyemtawanya Israeli atamkusanya, na kumlinda, kama mchungaji alindavyo kundi lake.


Kwa maana BWANA amemweka huru Yakobo, amemkomboa mkononi mwake aliyekuwa hodari kuliko yeye.


Maana, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi mwenyewe, naam, mimi, nitawatafuta kondoo wangu, na kuwatunza.


Kama vile mchungaji atafutavyo kondoo wake, siku ile anapokuwa kati ya kondoo wake waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta kondoo wangu; nami nitawaokoa katika mahali pote walipotawanyika, katika siku ya mawingu na giza.


Na ninyi, kondoo wangu, kondoo wa malisho yangu, ni wanadamu, na mimi ni Mungu wenu, asema Bwana MUNGU.


Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa nguvu za BWANA, kwa enzi ya jina la BWANA, Mungu wake; nao watakaa; maana sasa atakuwa mkuu hadi miisho ya dunia.


Walishe watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako, wakaao peke yao, msituni katikati ya Karmeli; na walishe katika Bashani na Gileadi, kama siku za kale.


Wakati huo nitawaingizeni, na wakati huo nitawakusanya; kwa maana nitawafanya ninyi msifiwe na mjulikane, miongoni mwa watu wote wa dunia, nitakapowarudisha wafungwa wenu mbele ya macho yenu, asema BWANA.


Katika siku ile, asema BWANA wa majeshi, nitakutwaa wewe, Ee Zerubabeli, mtumishi wangu, mwana wa Shealtieli, asema BWANA, nami nitakufanya kuwa kama pete yenye mhuri; kwa kuwa nimekuchagua, asema BWANA wa majeshi.


Nami nitaitia nguvu nyumba ya Yuda, nami nitaiokoa nyumba ya Yusufu, nami nitawarudisha, kwa maana nawaonea rehema; nao watakuwa kana kwamba sikuwatupa; kwa maana mimi ni BWANA, Mungu wao, nami nitawasikia.


BWANA wa majeshi asema hivi, Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; naam, wataushika wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yuko pamoja nanyi.


Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.


Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo