Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 23:9 - Swahili Revised Union Version

9 BWANA wa majeshi ndiye aliyefanya shauri hili, ili kuharibu kiburi cha utukufu wote, na kuwaaibisha watu wa duniani wote pia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi! Yeye ndiye aliyeyapanga haya yote. Alifanya hivyo akiharibu kiburi chao na kuwaaibisha waheshimiwa wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi! Yeye ndiye aliyeyapanga haya yote. Alifanya hivyo akiharibu kiburi chao na kuwaaibisha waheshimiwa wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi! Yeye ndiye aliyeyapanga haya yote. Alifanya hivyo akiharibu kiburi chao na kuwaaibisha waheshimiwa wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ndiye alipanga jambo hili, ili kukishusha kiburi cha utukufu wote na kuwanyenyekeza wale wote ambao ni mashuhuri duniani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 bwana Mwenye Nguvu Zote ndiye alipanga jambo hili, ili kukishusha kiburi cha utukufu wote na kuwanyenyekesha wale wote ambao ni mashuhuri duniani.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 BWANA wa majeshi ndiye aliyefanya shauri hili, ili kuharibu kiburi cha utukufu wote, na kuwaaibisha watu wa duniani wote pia.

Tazama sura Nakili




Isaya 23:9
29 Marejeleo ya Msalaba  

Humwaga aibu juu ya hao wakuu, Na kulegeza mshipi wa wenye nguvu.


Aliwamwagia wakuu dharau, Na kuwazungusha katika nyika isiyo na njia.


Kisha hao vyura watakwea juu yako wewe, na juu ya watu wako, na juu ya watumishi wako wote.


Angalia, Bwana, BWANA wa majeshi, atayakata matawi kwa nguvu za kutisha; nao walio warefu wa kimo watakatwa; na hao walioinuka wataangushwa chini;


Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayashusha chini majivuno yao walio wakali;


BWANA wa majeshi ameapa, akisema, Hakika yangu kama vile vilivyoazimia, ndivyo itakavyokuwa; na kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyotokea;


Hilo ndilo kusudi lililokusudiwa duniani kote, na huo ndio mkono ulionyoshwa juu ya mataifa yote.


Maana BWANA wa majeshi amekusudia, naye ni nani atakayelibatili? Na mkono wake ulionyoshwa, ni nani atakayeugeuza nyuma?


Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.


Kwa maana kutakuwa siku ya BWANA wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini.


Na majivuno ya mwanadamu yatainamishwa, na kiburi cha watu kitashushwa; naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.


Pita katika nchi yako, kama Nile, Ee binti wa Tarshishi, hapana tena mshipi wa kukuzuia.


Juu ya nchi ya watu wangu itamea michongoma na mibigili; naam, juu ya nyumba za furaha katika mji ulio na shangwe;


Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.


Mzee mwenye kuheshimiwa ndiye kichwa, na nabii afundishaye uongo ndiye mkia.


BWANA asema hivi, Jinsi iyo hiyo nitakiharibu kiburi cha Yuda, na kiburi kikuu cha Yerusalemu.


ukaseme, Ee BWANA, umenena kuhusu mji huu kwamba utakatiliwa mbali, usikaliwe na awaye yote, wala wanadamu wala wanyama, lakini uwe ukiwa hata milele.


Basi mimi, Nebukadneza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.


Tazama, nimekufanya mdogo kati ya mataifa; Umedharauliwa sana.


Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuri; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.


ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee.


na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.


kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.


Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo