Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Samueli 22:28 - Swahili Revised Union Version

28 Na watu wanaoonewa wewe utawaokoa; Ila macho yako huwapinga wenye kiburi, uwadhili.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Wewe wawaokoa walio wanyenyekevu, lakini wawaangalia wenye majivuno kuwaporomosha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Wewe wawaokoa walio wanyenyekevu, lakini wawaangalia wenye majivuno kuwaporomosha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Wewe wawaokoa walio wanyenyekevu, lakini wawaangalia wenye majivuno kuwaporomosha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Wewe huwaokoa wanyenyekevu, lakini macho yako ni juu ya wenye kiburi ili uwashushe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Wewe huwaokoa wanyenyekevu, lakini macho yako ni juu ya wenye kiburi ili uwashushe.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

28 Na watu wanaoonewa wewe utawaokoa; Ila macho yako huwapinga wenye kiburi, uwadhili.

Tazama sura Nakili




2 Samueli 22:28
23 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.


BWANA, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala mambo yanayozidi nguvu zangu.


Ingawa BWANA yuko juu, anamjali mnyenyekevu, Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali.


Najua ya kuwa BWANA atamfanyia mnyonge hukumu, Na wahitaji haki yao.


Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, na kumwambia, BWANA, Mungu wa Waebrania, asema hivi, Je! Utakataa hata lini kujinyenyekeza mbele zangu? Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie.


Sasa najua ya kuwa BWANA ni mkuu kuliko miungu yote; naam, katika jambo hilo walilowatenda kwa ujeuri.


Mwenye kiburi na moyo wa majivuno, Taa yake ni dhambi.


Na majivuno ya mwanadamu yatainamishwa, na kiburi cha watu kitashushwa; naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.


Ni nani uliyemshutumu na kumtukana? Umeinua sauti yako juu ya nani, na kuinua macho yako juu? Juu ya Mtakatifu wa Israeli.


Na mtu mnyonge ainamishwa, na mtu mkubwa amedhilika, na macho yao walioinuka hunyenyekezwa,


Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale.


Basi mimi, Nebukadneza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.


Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.


Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo