Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimwua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng'ombe;
Zaburi 1:1 - Swahili Revised Union Version Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Heri mtu asiyefuata shauri la waovu, asiyeshiriki njia za wenye dhambi, wala kujumuika na wenye dharau; Biblia Habari Njema - BHND Heri mtu asiyefuata shauri la waovu, asiyeshiriki njia za wenye dhambi, wala kujumuika na wenye dharau; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Heri mtu asiyefuata shauri la waovu, asiyeshiriki njia za wenye dhambi, wala kujumuika na wenye dharau; Neno: Bibilia Takatifu Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hasimami katika njia ya wenye dhambi, au kuketi katika baraza la wenye mizaha. Neno: Maandiko Matakatifu Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hasimami katika njia ya wenye dhambi, au kuketi katika baraza la wenye mizaha. BIBLIA KISWAHILI Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. |
Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimwua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng'ombe;
Ikawa, kama ingalikuwa neno dogo tu kuyaendea makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, akaenda akamtumikia Baali, akamsujudia.
Yeye naye akazifuata njia za nyumba ya Ahabu; kwa kuwa mamaye alikuwa mshauri wake katika kufanya maovu.
Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuiunga mkono mipango ya waovu?
BWANA huwahifadhi wageni; Huwategemeza yatima na mjane; Bali njia ya wasio haki huiharibu.
Shikeni yaliyo bora, asije akafanya hasira Nanyi mkapotea njiani, Kwa kuwa hasira yake huwaka upesi; Heri wote wanaomkimbilia.
Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?
Sikuketi katika mkutano wao wanaojifurahisha, wala sikufurahi, niliketi peke yangu kwa sababu ya mkono wako; kwa maana umenijaza ghadhabu.
Kisha nikawaambia watoto wao jangwani, Msiende katika amri za baba zenu, wala msizishike hukumu zao, wala msijitie unajisi kwa vinyago vyao.
Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Baryona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
(wala hakulikubali shauri na tendo lao), naye ni mtu wa Arimathaya, mji mmoja wa Wayahudi, tena anautazamia ufalme wa Mungu;
ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.
Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
na kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, ukapasuka ukwato wake zikawa mbili, naye ni mnyama mwenye kucheua akatafuna tena, katika wanyama wote, ndiye mnyama mtakayemla.
U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.
Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuishi katika uzinzi, tamaa, ulevi, na karamu za kula na kunywa vileo kupindukia, na ibada haramu ya sanamu;
Heri wazifuao nguo zao, ili wawe na haki ya kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.