Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 49:6 - Swahili Revised Union Version

6 Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimwua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng'ombe;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 lakini mimi sitashiriki njama zao; ee roho yangu, usishiriki mikutano yao, maana, katika hasira yao, walimuua mtu, kwa utundu wao walikata mshipa wa ng'ombe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 lakini mimi sitashiriki njama zao; ee roho yangu, usishiriki mikutano yao, maana, katika hasira yao, walimuua mtu, kwa utundu wao walikata mshipa wa ng'ombe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 lakini mimi sitashiriki njama zao; ee roho yangu, usishiriki mikutano yao, maana, katika hasira yao, walimuua mtu, kwa utundu wao walikata mshipa wa ng'ombe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Mimi na nisiingie katika baraza lao, nami nisiunganike katika kusanyiko lao, kwa kuwa wamewaua watu katika hasira yao, na kukata mishipa ya miguu ya mafahali kama walivyopenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Mimi na nisiingie katika baraza lao, nami nisiunganike katika kusanyiko lao, kwa kuwa wamewaua watu katika hasira yao, walikata mishipa ya miguu ya mafahali kama walivyopenda.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimwua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng'ombe;

Tazama sura Nakili




Mwanzo 49:6
29 Marejeleo ya Msalaba  

Yakobo akawaambia Simeoni na Lawi, Mmenitaabisha, kunifanya ninuke vibaya kati ya watu wa nchi hii, Wakanaani na Waperizi; na mimi, kwa kuwa watu wangu ni haba, watanikusanyikia, na kunipiga, nami nitaangamizwa, mimi na nyumba yangu.


Daudi akampokonya wapanda farasi elfu moja na mia saba na askari waliokwenda kwa miguu elfu ishirini; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila farasi wa magari mia moja akawabakiza.


Daudi akampokonya magari elfu moja, na wapanda farasi elfu saba, na askari waendao kwa miguu elfu ishirini; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila wa magari mia moja akawaweka.


Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.


Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu.


Ee Mungu, laiti ungewaua waovu! Na laiti watu wa damu wangetoka kwangu;


Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nayo nafsi yangu inashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.


Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji, Wala uhai wangu pamoja na wauaji.


Usinikokote pamoja na wasio haki, Wala pamoja na watenda maovu. Wawaambiao jirani zao maneno ya amani, Lakini mioyoni mwao mna madhara.


Ili nafsi yangu ikusifu, Wala isinyamaze. Ee BWANA, Mungu wangu, Nitakushukuru milele.


Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.


Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumainie Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.


Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Maana nitamsifu tena, Aliye msaada wangu, Na Mungu wangu.


Wewe, Mungu, uwapatilize, Na waanguke kwa mashauri yao. Uwatoe nje kwa ajili ya wingi wa makosa yao, Kwa maana wamekuasi Wewe.


Amka, ee moyo wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri.


Unifiche mbali na njama za watenda mabaya, Mbali na mipango ya watu wafanyao maovu;


Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi, Na tuvizie ili kumwaga damu; Tumwotee asiye na hatia, bila sababu;


Mawazo ya mwenye haki ni adili; Bali mashauri ya mtu mwovu ni hadaa.


Sikuketi katika mkutano wao wanaojifurahisha, wala sikufurahi, niliketi peke yangu kwa sababu ya mkono wako; kwa maana umenijaza ghadhabu.


Mtima wangu, mtima wangu! Naumwa katika moyo wangu wa ndani; moyo wangu umefadhaika ndani yangu; siwezi kunyamaza; kwa sababu umesikia, Ee nafsi yangu, sauti ya tarumbeta, mshindo wa vita.


Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.


Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?


Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina.


Yoshua akawafanyia vile vile kama BWANA alivyomwamuru; akawakata farasi wao, na kuteketeza magari yao kwa moto.


Mto ule wa Kishoni uliwachukua, Ule mto wa zamani, mto wa Kishoni. Ee roho yangu, endelea mbele kwa nguvu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo