Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yobu 10:3 - Swahili Revised Union Version

3 Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuiunga mkono mipango ya waovu?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Je, ni sawa kwako kunionea, kuidharau kazi ya mikono yako na kuipendelea mipango ya waovu?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Je, ni sawa kwako kunionea, kuidharau kazi ya mikono yako na kuipendelea mipango ya waovu?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Je, ni sawa kwako kunionea, kuidharau kazi ya mikono yako na kuipendelea mipango ya waovu?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Je, inakupendeza wewe kunidhulumu, kuikataa kazi ya mikono yako, huku ukiunga mkono mipango ya waovu?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Je, inakupendeza wewe kunionea, kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako, huku wewe ukitabasamu juu ya mipango ya waovu?

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuiunga mkono mipango ya waovu?

Tazama sura Nakili




Yobu 10:3
27 Marejeleo ya Msalaba  

Mikono yako imeniumba na kunifinyanga; Nawe utageuka na kuniangamiza?


Wewe ungeita, nami ningekujibu; Ungekuwa na tamaa ya kazi ya mikono yako.


Hata ukageuza roho yako kinyume cha Mungu, Na kuyatoa maneno kama hayo kinywani mwako.


Mungu amenitia kwa hao wapotovu, Na kunitupa mikononi mwao waovu.


Jueni basi kuwa Mungu amenipotosha, Na kunizingira kwa wavu wake.


Tazama, kufanikiwa kwao hakumo mkononi mwao; Mipango ya waovu na iwe mbali nami.


Naye ndiye aliyezijaza nyumba zao vitu vyema; Lakini mashauri ya waovu na yawe mbali nami.


Kama aishivyo Mungu, aliyeniondolea haki yangu; Huyo Mwenyezi aliyeitesa nafsi yangu;


Wewe umegeuka kuwa mkali kwangu; Nawe waniudhi kwa uweza wa mkono wako.


Je! Huyo aliyenifanya mimi ndani ya tumbo, siye aliyemfanya na yeye? Si yeye mmoja aliyetufinyanga tumboni?


Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.


Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi? Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye.


Je! Hata hukumu yangu utaibatilisha? Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki?


Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu, Wala hatawathibitisha watendao uovu.


Hayo yote ni mamoja; kwa hiyo nasema, Yeye huangamiza wakamilifu na waovu pia.


Dunia imetiwa mkononi mwa waovu; Yeye hufunika nyuso za waamuzi wake; Kama si yeye, ni nani basi?


Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.


BWANA atanitimizia malengo yake kwangu; Ee BWANA, fadhili zako ni za milele; Usiiache kazi ya mikono yako.


Kwa kuwa BWANA huwasikia wahitaji, Wala hawadharau wafungwa wake.


Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako.


Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo