Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa ushauri wake haukufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajinyonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye.
Methali 11:5 - Swahili Revised Union Version Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uadilifu wa watu wanyofu huinyosha njia yao, lakini waovu huanguka kwa uovu wao wenyewe. Biblia Habari Njema - BHND Uadilifu wa watu wanyofu huinyosha njia yao, lakini waovu huanguka kwa uovu wao wenyewe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uadilifu wa watu wanyofu huinyosha njia yao, lakini waovu huanguka kwa uovu wao wenyewe. Neno: Bibilia Takatifu Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyo nyofu, bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyonyooka, bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe. BIBLIA KISWAHILI Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake. |
Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa ushauri wake haukufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajinyonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye.
Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake.
Njia ya mtu mvivu ni kama boma la miiba; Bali mapito yao wenye unyofu hufanyika njia kuu.
Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; kwa sababu hiyo, Israeli na Efraimu watajikwaa katika uovu wao. Yuda naye atajikwaa pamoja nao.
Ndipo watu wa Israeli wakageuka, na watu wa Benyamini walishtushwa; kwa kuwa waliona ya kwamba wamefikiwa na maafa.