Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Samueli 17:23 - Swahili Revised Union Version

23 Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa ushauri wake haukufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajinyonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Ahithofeli alipoona kwamba shauri lake halikufuatwa, alitandika punda wake, akaenda nyumbani, kwenye mji wake. Alipofika huko, alipanga vizuri mambo ya nyumbani kwake, akajinyonga. Akafariki na kuzikwa kwenye kaburi la baba yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Ahithofeli alipoona kwamba shauri lake halikufuatwa, alitandika punda wake, akaenda nyumbani, kwenye mji wake. Alipofika huko, alipanga vizuri mambo ya nyumbani kwake, akajinyonga. Akafariki na kuzikwa kwenye kaburi la baba yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Ahithofeli alipoona kwamba shauri lake halikufuatwa, alitandika punda wake, akaenda nyumbani, kwenye mji wake. Alipofika huko, alipanga vizuri mambo ya nyumbani kwake, akajinyonga. Akafariki na kuzikwa kwenye kaburi la baba yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Ahithofeli alipoona kwamba ushauri wake haukufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka kwenda nyumbani mwake kwenye mji wake. Akaiweka nyumba yake katika utaratibu, kisha akajinyonga mwenyewe. Hivyo akafa na akazikwa katika kaburi la baba yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Ahithofeli alipoona kwamba shauri lake halikufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka kwenda nyumbani kwake kwenye mji wake. Akaiweka nyumba yake katika utaratibu, kisha akajinyonga mwenyewe. Hivyo akafa na akazikwa katika kaburi la baba yake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

23 Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa ushauri wake haukufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajinyonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye.

Tazama sura Nakili

2 Samueli 17:23
15 Marejeleo ya Msalaba  

Absalomu alipokuwa akitoa dhabihu alituma Ahithofeli Mgiloni, Mshauri wake Daudi, aitwe kutoka mji wake, yaani, Gilo. Njama zao zikawa na nguvu; maana watu waliokuwa pamoja na Absalomu walizidi kuongezeka.

Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uugeuze ushauri wa Ahithofeli uwe ubatili.

Na ushauri wake Ahithofeli, aliokuwa akiutoa siku zile, ulikuwa kama mtu aulizapo kwa neno la Mungu; ndivyo yalivyokuwa mashauri yote ya Ahithofeli, kwa Daudi, na kwa Absalomu.

Ndipo Daudi, na watu wote waliokuwa pamoja naye, wakaondoka, wakavuka Yordani; na kulipopambazuka hakubaki hata mmoja wao asiyevuka Yordani.

Ikawa Zimri alipoona ya kuwa mji umetwaliwa, akaingia ngomeni mwa nyumba ya mfalme, akaiteketeza nyumba ya mfalme juu yake kwa moto, akafa;

Siku hizo Hezekia akaugua, akawa katika hatari ya kufa. Isaya, nabii, mwana wa Amozi, akamjia akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.

Je! Siyo msiba kwa wasio haki, Na hasara kwao watendao uovu?

Ndiyo malipo ya washitaki wangu toka kwa BWANA, Na ya hao wanaoisingizia nafsi yangu mabaya.

Wewe, Mungu, uwapatilize, Na waanguke kwa mashauri yao. Uwatoe nje kwa ajili ya wingi wa makosa yao, Kwa maana wamekuasi Wewe.

Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.

Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.

Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake; Na moyo wake hununa juu ya BWANA.

Siku hizo Hezekia aliugua, akawa karibu kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.

Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo