Akasema, Na atukuzwe BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hakuacha rehema zake na kweli yake kwa bwana wangu. BWANA akaniongoza mimi nami njiani hata nyumba ya nduguze bwana wangu.
Methali 14:22 - Swahili Revised Union Version Je! Hawakosi wawazao mabaya? Bali fadhili na kweli zina wao wawazao mema. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayepanga maovu kweli anakosea! Wanaopanga kutenda mema hufadhiliwa. Biblia Habari Njema - BHND Anayepanga maovu kweli anakosea! Wanaopanga kutenda mema hufadhiliwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayepanga maovu kweli anakosea! Wanaopanga kutenda mema hufadhiliwa. Neno: Bibilia Takatifu Je, wale wanaopanga ubaya hawapotoki? Bali wale wanaopanga kilicho chema hupata upendo na uaminifu. Neno: Maandiko Matakatifu Je, wale wanaopanga ubaya hawapotoki? Bali wale wanaopanga kilicho chema hupata upendo na uaminifu. BIBLIA KISWAHILI Je! Hawakosi wawazao mabaya? Bali fadhili na kweli zina wao wawazao mema. |
Akasema, Na atukuzwe BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hakuacha rehema zake na kweli yake kwa bwana wangu. BWANA akaniongoza mimi nami njiani hata nyumba ya nduguze bwana wangu.
Lakini BWANA akamwambia Daudi baba yangu, Kwa kuwa ilikuwa moyoni mwako kujenga nyumba kwa jina langu, ulifanya vema kuwaza hivi moyoni mwako;
Rehema na kweli zisiachane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka asubuhi huyafanya, sababu wana uwezo mikononi mwao.
Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
Wale wanaume wakamwambia, Tutautoa uhai wetu badala ya uhai wenu, ikiwa hamwitangazi habari ya shughuli yetu hii; kisha itakuwa, wakati BWANA atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa hisani na uaminifu.