Methali 13:2 - Swahili Revised Union Version Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake; Bali nafsi ya mtu haini itakula jeuri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu mwema hupata mema kutokana na maneno yake, lakini wadanganyifu huishi kwa ukatili. Biblia Habari Njema - BHND Mtu mwema hupata mema kutokana na maneno yake, lakini wadanganyifu huishi kwa ukatili. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu mwema hupata mema kutokana na maneno yake, lakini wadanganyifu huishi kwa ukatili. Neno: Bibilia Takatifu Kutoka tunda la midomo yake, mtu hufurahia mambo mema, bali wasio waaminifu wanatamani sana jeuri. Neno: Maandiko Matakatifu Kutoka tunda la midomo yake mtu hufurahia mambo mema, bali wasio waaminifu wanatamani sana jeuri. BIBLIA KISWAHILI Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake; Bali nafsi ya mtu haini itakula jeuri. |
Maana mkononi mwa BWANA mna kikombe, Na mvinyo yake inatoka povu; Kumejaa machanganyiko; Naye huyamimina. Na sira zake wasio haki wa dunia Watazifyonza na kuzinywa.
Kinywa chake mwenye haki ni chemchemi ya uzima; Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu,
Haja ya mwenye haki ni kupata mema tu; Bali kutaraji kwake mtu mwovu huishia katika ghadhabu.
Mmelima dhuluma, mmevuna uovu; mmekula matunda ya uongo; kwa maana uliitumainia njia yako, na wingi wa mashujaa wako.
Kwa maana udhalimu uliotendwa juu ya Lebanoni utakufunikiza, na kuangamizwa kwao wanyama kutakutia hofu; kwa sababu ya damu ya watu, na kwa sababu ya udhalimu iliotendwa nchi hii, na mji huu, na watu wote wanaokaa ndani yake.
Kwa sababu umeteka nyara mataifa mengi, mabaki yote ya kabila watakuteka wewe; kwa sababu ya damu ya watu, na kwa sababu ya udhalimu iliotendwa nchi hii, na mji huu, na watu wote wanaokaa ndani yake.
kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; ndiyo wanayostahili.