Naye BWANA akawa pamoja naye, kila alikokwenda alifanikiwa; tena alimwasi mfalme wa Ashuru, wala hakumtumikia.
Isaya 33:6 - Swahili Revised Union Version Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa; kumcha BWANA ni hazina yake ya akiba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Enyi watu wa Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu atawajalieni usalama, atawaokoa na kuwapa hekima na maarifa. Hazina yenu kuu ni kumcha Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Enyi watu wa Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu atawajalieni usalama, atawaokoa na kuwapa hekima na maarifa. Hazina yenu kuu ni kumcha Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Enyi watu wa Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu atawajalieni usalama, atawaokoa na kuwapa hekima na maarifa. Hazina yenu kuu ni kumcha Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Atakuwa msingi ulio imara kwa wakati wenu, hazina ya wokovu tele, hekima na maarifa; kumcha Mwenyezi Mungu ni ufunguo wa hazina hii. Neno: Maandiko Matakatifu Atakuwa msingi ulio imara kwa wakati wenu, ghala za wokovu tele, hekima na maarifa; kumcha bwana ni ufunguo wa hazina hii. BIBLIA KISWAHILI Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa; kumcha BWANA ni hazina yake ya akiba. |
Naye BWANA akawa pamoja naye, kila alikokwenda alifanikiwa; tena alimwasi mfalme wa Ashuru, wala hakumtumikia.
Katika fahari yako usitawi uendelee Kwa ajili ya kweli, upole na haki Na mkono wako wa kulia Utakutendea mambo ya ajabu.
Kwa sababu ya maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi; Bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwa
Kwa maana ulinzi wa hekima ni kama ulinzi wa fedha na ubora wa maarifa ni kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.
Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua BWANA, kama vile maji yanavyoifunika bahari.
Siku ile wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda; Sisi tunao mji ulio na nguvu; Ataamuru wokovu kuwa kuta na maboma.
Na watu wangu watakaa katika makao ya amani; na katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu.
Angalia Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa makao ya raha; hema isiyotikisika; vigingi vyake havitang'olewa, wala kamba zake hazitakatika.
Bali Israeli wataokolewa na BWANA kwa wokovu wa milele; ninyi hamtatahayarika, wala kufadhaika, milele na milele.
Yeye aliyehamishwa na kufungwa atafunguliwa kwa haraka; wala hatakufa na kushuka shimoni, wala chakula chake hakitapunguka.
Inueni macho yenu mbinguni, mkaitazame nchi chini; maana mbingu zitatoweka kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, nao wakaao ndani yake watakufa kadhalika; bali wokovu wangu utakuwa wa milele, na ukombozi wangu hautakoma kamwe.
Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hadi aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.
kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.
Maana, mazoezi ya viungo vya mwili yana manufaa kidogo, lakini utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.