Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 19:23 - Swahili Revised Union Version

23 Kumcha BWANA huelekea uhai; Atakaa ameshiba; hatajiliwa na ubaya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Kumcha Mwenyezi-Mungu kunaleta uhai; amchaye hujaliwa pumziko la kutosheleza, wala hatapatwa na baa lolote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Kumcha Mwenyezi-Mungu kunaleta uhai; amchaye hujaliwa pumziko la kutosheleza, wala hatapatwa na baa lolote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Kumcha Mwenyezi-Mungu kunaleta uhai; amchaye hujaliwa pumziko la kutosheleza, wala hatapatwa na baa lolote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Kumcha Mwenyezi Mungu huongoza kwenye uzima, kisha mtu hupumzika akiwa ameridhika, bila kuguswa na shida.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Kumcha bwana huongoza kwenye uzima, kisha mtu hupumzika akiwa ameridhika, bila kuguswa na shida.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

23 Kumcha BWANA huelekea uhai; Atakaa ameshiba; hatajiliwa na ubaya.

Tazama sura Nakili




Methali 19:23
28 Marejeleo ya Msalaba  

Bali fadhili za BWANA ni kwa wamchao Tangu milele hata milele, Na haki yake ni kwa vizazi vyote;


Kicho cha BWANA ni kitakatifu, Kinadumu milele. Hukumu za BWANA ni kweli, Zina haki kabisa.


Watafanikiwa maishani mwao; Na wazawa wao wataimiliki nchi.


Hakika wokovu wake uko karibu na wamchao, Ndipo utukufu wake ukae katika nchi yetu.


Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako, Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.


Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.


Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonesha wokovu wangu.


Kumcha BWANA kwaongeza siku za mtu; Bali miaka yao wasio haki itapunguzwa.


Haki huelekea uzima; Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe.


Mwenye haki hatapatikana na msiba wowote; Bali wasio haki watajazwa mabaya.


Haja ya mwanadamu ni hisani yake; Ni afadhali maskini kuliko mwongo.


Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha BWANA Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima.


Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu.


Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawachomozea, likiwa na uwezo wa kuponya katika miale yake; nanyi mtatoka nje, na kuchezacheza kama ndama watokapo mazizini.


Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.


Basi kanisa likapata raha kote katika Yudea na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.


Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.


Maana, mazoezi ya viungo vya mwili yana manufaa kidogo, lakini utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.


Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike katika ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo