Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 14:26 - Swahili Revised Union Version

26 Kumcha BWANA ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Amchaye Mwenyezi-Mungu ana tumaini imara, na watoto wake watapata kimbilio salama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Amchaye Mwenyezi-Mungu ana tumaini imara, na watoto wake watapata kimbilio salama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Amchaye Mwenyezi-Mungu ana tumaini imara, na watoto wake watapata kimbilio salama.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Yeye amchaye Mwenyezi Mungu ana ngome salama, na kwa watoto wake itakuwa kimbilio.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Yeye amchaye bwana ana ngome salama, na kwa watoto wake itakuwa kimbilio.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

26 Kumcha BWANA ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio.

Tazama sura Nakili




Methali 14:26
19 Marejeleo ya Msalaba  

Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Abrahamu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu.


Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake.


Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti.


Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.


Kumcha BWANA huelekea uhai; Atakaa ameshiba; hatajiliwa na ubaya.


Mwenye haki aendaye katika unyofu wake, Watoto wake wabarikiwa baada yake.


Ni vizuri kwamba ulishike neno hilo; naam, hata kwa neno hilo tena usiuondoe mkono wako; kwa kuwa mtu yule amchaye Mungu atatoka katika hayo yote.


Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa; kumcha BWANA ni hazina yake ya akiba.


BWANA akasema, Hakika nitakutia nguvu upate mema; hakika nitamlazimisha adui akusihi wakati wa uovu, na wakati wa taabu.


Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawachomozea, likiwa na uwezo wa kuponya katika miale yake; nanyi mtatoka nje, na kuchezacheza kama ndama watokapo mazizini.


Basi kanisa likapata raha kote katika Yudea na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo