Yoshua 15 - Swahili Revised Union VersionNchi ya Yuda 1 Sehemu waliyopewa wana wa Yuda kwa kufuata jamaa zao ilikuwa imefika mpaka wa Edomu, hadi jangwa la Sini upande wa kusini, huko mwisho upande wa kusini. 2 Mpaka wao wa kusini ulikuwa kutoka mwisho wa Bahari ya Chumvi, kutoka ile hori ielekeayo kusini; 3 nao ukaendelea upande wa kusini wa kukwea kwenda Akrabimu, kisha ukaendelea hadi Sini, kisha ukaenda upande wa kusini wa Kadesh-barnea, kisha ukaendelea karibu na Hesroni, kisha ukafika Adari, na kuzunguka kwendea Karka; 4 kisha ukaendelea hadi Azmoni, na kutokea hapo penye kijito cha Misri; na mwisho wa mpaka huo ulikuwa baharini; huu ndio mpaka wenu wa upande wa kusini. 5 Na mpaka wa upande wa mashariki ulikuwa Bahari ya Chumvi, hadi mwisho wa mto wa Yordani. Na mpaka wa upande wa kaskazini ulikuwa kutoka pale penye hori ya baharini mwisho wa mto wa Yordani; 6 na huo mpaka ukaendelea hadi Beth-hogla, kisha ukaendelea upande wa kaskazini wa Beth-araba; kisha mpaka ukaendelea hadi jiwe la Bohani mwana wa Reubeni; 7 kisha mpaka ukaendelea hadi Debiri kutoka bonde la Akori, na ukaendelea upande wa kaskazini, kwa kuelekea Gilgali, iliyo mkabala wa kukwelea kwenda Adumimu, ulio upande wa kusini wa mto; kisha huo mpaka ukaendelea hadi kufika kwenye maji ya Enshemeshi, na kuishia Enrogeli; 8 kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufika ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini; 9 kisha mpaka ulipigwa kutoka juu ya mlima huo hadi kufika chemchemi ya maji ya Neftoa kisha ukatokea hata miji ya kilima cha Efroni; kisha mpaka ulipigwa hadi kufika Baala (ndio Kiriath-yearimu); 10 kisha mpaka ukazunguka kutoka Baala kwendelea upande wa magharibi hadi kilima Seiri, kisha ukaendelea hadi upande wa mlima wa Yearimu upande wa kaskazini (huo ndio Kesaloni), kisha ukateremkia Beth-shemeshi, na kwendelea karibu na Timna; 11 kisha mpaka ukaendelea hadi upande wa kaskazini wa Ekroni; tena mpaka ulipigwa hadi Shikroni, na kwendelea mpaka kilima cha Baala, kisha ukatokea hapo Yabneeli; na ukaishia katika bahari. 12 Na mpaka wa upande wa magharibi ulifika hadi Bahari Kubwa, na mpaka wake. Huo ndio mpaka wa wana wa Yuda kwa kuzunguka kotekote sawasawa na jamaa zao. Kalebu aichukua milki yake 13 Kisha alimpa huyo Kalebu mwana wa Yefune sehemu kati ya wana wa Yuda, kama BWANA alivyomwamuru Yoshua, Kiriath-arba, ndiyo Hebroni (ni huyo Arba aliyekuwa babaye Anaki). 14 Huyo Kalebu aliwafukuza watoke hapo hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, na Ahimani, na Talmai, wazawa wa Anaki. 15 Kisha akakwea kutoka huko ili kuwaendea wenyeji wa Debiri; jina la Debiri hapo kwanza lilikuwa Kiriath-seferi. 16 Kalebu akasema, Yeyote atakayeupiga Kiriath-seferi na kuutwaa, mimi nitampa Aksa binti yangu awe mkewe. 17 Naye Othnieli mwana wa Kenazi, nduguye Kalebu, aliutwaa; basi akampa Aksa binti yake awe mkewe. 18 Kisha ikawa, hapo huyo mwanamke alipokwenda kwa mumewe, akamtaka aombe shamba kwa baba yake; akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Unataka nikupe nini? 19 Huyo mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa umeniweka katika nchi ya kusini, unipe na chemchemi za maji pia. Ndipo akampa chemchemi za maji ya upande wa juu, na chemchemi za maji yaupande wa chini. Miji ya Yuda 20 Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Yuda sawasawa na jamaa zao. 21 Miji ya mwisho ya kabila la wana wa Yuda upande wa kuelekea mpaka wa Edomu katika nchi ya Negebu ilikuwa ni Kabseeli, Ederi, Yaguri; 22 Kina, Dimona, Adada; 23 Kedeshi, Hazori, Ithnani; 24 Zifu, Telemu, Bealothi; 25 Hazor-hadata, Kerioth-hezroni (ndio Hazori); 26 Amamu, Shema, Molada; 27 Hasar-gada, Heshmoni, Beth-peleti; 28 Hasar-shuali, Beer-sheba, Biziothia; 29 Baala, Iyimu, Esemu; 30 Eltoladi, Kesili, Horma; 31 Siklagi, Madmana, Sansana; 32 Lebaothi, Shilhimu, Aini na Rimoni; miji hiyo yote ni miji ishirini na tisa, pamoja na vijiji vyake. 33 Katika nchi ya Shefela, Eshtaoli, Sora, Ashna, 34 Zanoa, Enganimu, Tapua, Enamu; 35 Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka; 36 Shaarimu, Adithaimu, Gedera na Gederothaimu miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. 37 Senani, Hadasha, Migdal-gadi; 38 Dilani, Mispe, Yoktheeli; 39 Lakishi, Bozkathi, Egloni; 40 Kaboni, Lamasi, Kithilishi; 41 Gederothi, Beth-dagoni, Naama na Makeda; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake. 42 Libna, Etheri, Ashani; 43 Yifta, Ashna, Nesibu; 44 Keila, Akizibu na Maresha; miji tisa, pamoja na vijiji vyake. 45 Ekroni, pamoja na miji yake na vijiji vyake; 46 kutoka huko Ekroni mpaka baharini, yote iliyokuwa upande wa Ashdodi, pamoja na vijiji vyake. 47 Ashdodi, na miji yake na vijiji vyake; Gaza, na miji yake na vijiji vyake; mpaka kijito cha Misri, na bahari kuu na pwani yake. 48 Na katika nchi ya vilima, Shamiri, Yatiri, Soko; 49 Dana, Kiriath-sana (ambao ni Debiri); 50 Anabu, Eshtemoa, Animu; 51 Gosheni, Holoni na Gilo; miji kumi na mmoja, pamoja na vijiji vyake. 52 Arabu, Duma, Eshani; 53 Yanumu, Beth-tapua, Afeka; 54 Humta, Kiriath-arba (ndio Hebroni) na Siori; miji tisa, pamoja na vijiji vyake. 55 Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta; 56 Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa; 57 Kaini, Gibea na Timna; miji kumi, pamoja na vijiji vyake. 58 Halhuli, Beth-suri, Gedori; 59 Maarathi, Bethanothi na Eltekoni; miji sita, pamoja na vijiji vyake. 60 Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu) na Raba; miji miwili, pamoja vijiji vyake. 61 Huko nyikani, Beth-araba, na Midini, na Sekaka; 62 na Nibshani, na huo Mji wa Chumvi, na Engedi; miji sita, pamoja na vijiji vyake. 63 Tena katika habari ya Wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwatoa; lakini hao Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Yuda huko Yerusalemu hata hivi leo. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya