Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yoshua 15:7 - Swahili Revised Union Version

7 kisha mpaka ukaendelea hadi Debiri kutoka bonde la Akori, na ukaendelea upande wa kaskazini, kwa kuelekea Gilgali, iliyo mkabala wa kukwelea kwenda Adumimu, ulio upande wa kusini wa mto; kisha huo mpaka ukaendelea hadi kufika kwenye maji ya Enshemeshi, na kuishia Enrogeli;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Kutoka hapo, uliendelea hadi Debiri kwenye bonde la Akori na kaskazini kuelekea Gilgali, ulio karibu na mwinuko wa Adumimu ambao uko kusini mwa kijito, kisha ukaelekea kwenye chemchemi za En-shemeshi na kuishia En-rogeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Kutoka hapo, uliendelea hadi Debiri kwenye bonde la Akori na kaskazini kuelekea Gilgali, ulio karibu na mwinuko wa Adumimu ambao uko kusini mwa kijito, kisha ukaelekea kwenye chemchemi za En-shemeshi na kuishia En-rogeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Kutoka hapo, uliendelea hadi Debiri kwenye bonde la Akori na kaskazini kuelekea Gilgali, ulio karibu na mwinuko wa Adumimu ambao uko kusini mwa kijito, kisha ukaelekea kwenye chemchemi za En-shemeshi na kuishia En-rogeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Kisha mpaka ulipanda hadi Debiri kutoka Bonde la Akori, na kugeuka kaskazini hadi Gilgali inayotazamana na miteremko ya Adumimu, kusini mwa bonde. Ukaendelea sambamba hadi maji ya En-Shemeshi na kutokeza huko En-Rogeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Kisha mpaka ulipanda hadi Debiri kutoka Bonde la Akori na kugeuka kaskazini hadi Gilgali inayotazamana na materemko ya Adumimu, kusini mwa bonde. Ukaendelea sambamba hadi maji ya En-Shemeshi na kutokeza huko En-Rogeli.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 kisha mpaka ukaendelea hadi Debiri kutoka bonde la Akori, na ukaendelea upande wa kaskazini, kwa kuelekea Gilgali, iliyo mkabala wa kukwelea kwenda Adumimu, ulio upande wa kusini wa mto; kisha huo mpaka ukaendelea hadi kufika kwenye maji ya Enshemeshi, na kuishia Enrogeli;

Tazama sura Nakili

Yoshua 15:7
13 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Yonathani na Ahimaasi walikuwa wakikaa karibu na Enrogeli; na mjakazi mmoja alikuwa akienda na kuwapa habari; ndipo wakamwambie mfalme Daudi; maana ilikuwa lazima wasionekane wakiingia mjini.

Adonia akatoa sadaka ya kondoo, ng'ombe na ndama wanono, karibu na jiwe la Zohelethi, lililo karibu na chemchemi Enrogeli; akawaita ndugu zake wote, wana wa mfalme, na watu wote wa Yuda, watumishi wa mfalme;

Na Sharoni itakuwa zizi la makundi ya kondoo, na bonde la Akori mahali pa kulala makundi ya ng'ombe, kwa ajili ya watu wangu walionitafuta.

Maana mama yao amezini; yeye aliyewachukua mimba ametenda mambo ya aibu; maana alisema, Nitafuatana na wapenzi wangu, wanipao chakula changu na maji yangu, sufu yangu na kitani yangu, mafuta yangu na vileo vyangu.

Kisha Yoshua akarudi, na Israeli wote pamoja naye, hata kambi yao huko Gilgali.

Kisha akakwea kutoka huko ili kuwaendea wenyeji wa Debiri; jina la Debiri hapo kwanza lilikuwa Kiriath-seferi.

na huo mpaka ukaendelea hadi Beth-hogla, kisha ukaendelea upande wa kaskazini wa Beth-araba; kisha mpaka ukaendelea hadi jiwe la Bohani mwana wa Reubeni;

kisha ulipinda upande wa kaskazini, nao ukatokea hapo Enshemeshi, ukatokea hadi kufikia Gelilothi, ambao ni mkabala wa makweleo ya Adumimu; kisha uliteremka hadi jiwe la Bohani mwana wa Reubeni;

Na hao watu wakakwea kutoka Yordani siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, wakapiga kambi Gilgali, katika mpaka wa mashariki wa Yeriko.

Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na Lile joho, na ile kabari ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng'ombe wake, punda wake na kondoo wake, hema yake na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hadi bonde la Akori.

Kisha wakakusanya juu yake rundo kubwa la mawe hata leo; naye BWANA akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde la Akori, hata leo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo