Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yoshua 15:8 - Swahili Revised Union Version

8 kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufika ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Kisha, mpaka huo ulipitia kwenye Bonde la Hinomu, upande wa kusini mwa kilima cha Wayebusi, yaani Yerusalemu, kuelekea kilele cha mlima ulio magharibi ya bonde la Hinomu na kufika mwishoni mwa bonde la Refaimu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Kisha, mpaka huo ulipitia kwenye Bonde la Hinomu, upande wa kusini mwa kilima cha Wayebusi, yaani Yerusalemu, kuelekea kilele cha mlima ulio magharibi ya bonde la Hinomu na kufika mwishoni mwa bonde la Refaimu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Kisha, mpaka huo ulipitia kwenye Bonde la Hinomu, upande wa kusini mwa kilima cha Wayebusi, yaani Yerusalemu, kuelekea kilele cha mlima ulio magharibi ya bonde la Hinomu na kufika mwishoni mwa bonde la Refaimu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Kisha ukapanda kwa kufuata Bonde la Ben-Hinomu sambamba na mteremko wa kusini wa mji mkubwa wa Wayebusi (yaani Yerusalemu). Kutoka hapo ukapanda juu ya kilima magharibi mwa Bonde la Hinomu mwisho wa ncha ya kaskazini mwa Bonde la Warefai.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Kisha ukapanda kwa kufuata Bonde la Ben-Hinomu sambamba na mteremko wa kusini wa mji mkubwa wa Wayebusi (yaani Yerusalemu). Kutoka hapo ukapanda juu ya kilima magharibi ya Bonde la Hinomu mwisho wa ncha ya kaskazini mwa Bonde la Warefai.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufika ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini;

Tazama sura Nakili

Yoshua 15:8
17 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kujitawanya bondeni mwa Warefai.

Lakini wakapanda hao Wafilisti tena mara ya pili, wakajitawanya bondeni mwa Warefai.

Naye akainajisi Tofethi, iliyomo katika bonde la wana wa Hinomu, ili mtu asipitishe mwana wake au binti yake motoni kwa Moleki.

Kisha Daudi na Israeli wote wakaenda Yerusalemu, (ndio Yebusi;) nao Wayebusi, wenyeji wa nchi, walikuwamo.

Tena akafukiza uvumba katika bonde la mwana wa Hinomu, akawateketeza wanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza BWANA mbele ya wana wa Israeli.

Zanoa, Adulamu na vijiji vyake, Lakishi na mashamba yake, Azeka na vijiji vyake. Hivyo wakakaa toka Beer-sheba mpaka bonde la Hinomu.

Tena itakuwa kama hapo mvunaji ashikapo mabua ya ngano, na mkono wake ukatapo masuke; tena itakuwa kama hapo mtu aokotapo masuke katika bonde la Warefai.

Kisha Yeremia akatoka huko Tofethi, huko ambako BWANA alimtuma atoe unabii; naye akasimama katika ua wa nyumba ya BWANA, akawaambia watu wote,

ukatoke uende mpaka bonde la mwana wa Hinomu lililo karibu na mahali pa kuingia kwa lango la vigae, ukahubiri huko maneno nitakayokuambia,

basi, angalieni, siku zinakuja, asema BWANA, ambazo katika siku hizo mahali hapa hapataitwa tena Tofethi, wala Bonde la mwana wa Hinomu, bali, Bonde la Machinjo.

Tena katika habari ya Wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwatoa; lakini hao Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Yuda huko Yerusalemu hata hivi leo.

kisha mpaka uliteremka hadi mwisho wa mlima ulio pale mkabala wa bonde la mwana wa Hinomu, lililo pale katika bonde la Warefai, upande wa kaskazini; nao ukateremkia mpaka bonde la Hinomu, hadi ubavuni mwa Myebusi upande wa kusini, kisha ukateremka hadi Enrogeli,

na Zela, na Elefu, na huyo Myebusi (ndio Yerusalemu), na Gibeathi, na Kiriathi; miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. Huo ndio urithi wa wana wa Benyamini kwa kufuata jamaa zao.

Lakini wana wa Benyamini hawakuwafukuza Wayebusi waliokaa mji wa Yerusalemu; bali Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Benyamini ndani ya Yerusalemu hata hivi leo.

Kisha wana wa Yuda wakapigana na Yerusalemu, wakautwaa, wakaupiga kwa makali ya upanga, na kuupiga moto huo mji.

Lakini huyo mtu hakukubali kukaa usiku huo, ila akainuka, akaenda zake, akafika mkabala wa Yebusi (huo ndio Yerusalemu); nao walikuwako pamoja naye punda kadhaa waliotandikwa; suria wake naye alikuwa pamoja naye.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo