Wakasema, “Ondoka hapa!” Kisha wakasema, “Mtu huyu amekuja kukaa kwetu kama mgeni; naye kumbe anataka kuhukumu! Basi tutakutenda vibaya kuliko hawa”. Wakamsonga sana Lutu, wakakaribia wauvunje mlango.
Methali 5:12 - Swahili Revised Union Version Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo utasema, “Jinsi gani nilivyochukia nidhamu, na kudharau maonyo moyoni mwangu! Biblia Habari Njema - BHND Hapo utasema, “Jinsi gani nilivyochukia nidhamu, na kudharau maonyo moyoni mwangu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo utasema, “Jinsi gani nilivyochukia nidhamu, na kudharau maonyo moyoni mwangu! Neno: Bibilia Takatifu Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu! Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo! Neno: Maandiko Matakatifu Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu! Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo! BIBLIA KISWAHILI Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa; |
Wakasema, “Ondoka hapa!” Kisha wakasema, “Mtu huyu amekuja kukaa kwetu kama mgeni; naye kumbe anataka kuhukumu! Basi tutakutenda vibaya kuliko hawa”. Wakamsonga sana Lutu, wakakaribia wauvunje mlango.
Ikawa, aliposema naye, mfalme akamwambia, Je! Tumekutia wewe kuwa mshauri wa mfalme? Nyamaza; kwa nini upigwe? Ndipo yule nabii akaacha, akasema, Najua ya kuwa Mungu amekusudia kukuangamiza, kwa sababu umeyafanya haya, wala hukulisikiliza shauri langu.
lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya.
Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?
Umaskini na fedheha zitampata yeye akataaye kurudiwa; Bali yeye aangaliaye maonyo ataheshimiwa.
Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru, Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima.
Tena nilituma kwenu watumishi wangu wote, manabii, nikiamka mapema na kuwatuma, nikisema, Basi ninyi; msilifanye chukizo hili linalochukiza.