Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 10:17 - Swahili Revised Union Version

17 Akubaliye kurudiwa huwa katika njia ya uzima; Bali yeye aachaye maonyo hukosa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Anayekubali maonyo anaelekea kwenye uhai, lakini anayekataa kuonywa amepotoka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Anayekubali maonyo anaelekea kwenye uhai, lakini anayekataa kuonywa amepotoka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Anayekubali maonyo anaelekea kwenye uhai, lakini anayekataa kuonywa amepotoka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima, lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima, lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

17 Akubaliye kurudiwa huwa katika njia ya uzima; Bali yeye aachaye maonyo hukosa.

Tazama sura Nakili




Methali 10:17
22 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, aliposema naye, mfalme akamwambia, Je! Tumekutia wewe kuwa mshauri wa mfalme? Nyamaza; kwa nini upigwe? Ndipo yule nabii akaacha, akasema, Najua ya kuwa Mungu amekusudia kukuangamiza, kwa sababu umeyafanya haya, wala hukulisikiliza shauri langu.


Hawakukubali mashauri yangu, Wakayadharau maonyo yangu yote.


Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa; Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama.


Adhabu kali ina yeye aiachaye njia; Naye achukiaye kukemewa atakufa.


Akataaye maonyo huidharau nafsi yake mwenyewe; Bali yeye asikilizaye lawama hujipatia ufahamu.


Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafla, wala hapati dawa.


Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu anayeshikamana naye.


Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.


Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi.


Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa;


Nilikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko.


Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru, Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima.


Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako; wala usiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba hukukusudia; kwa nini Mungu akasirishwe na maneno yako, na kuiharibu kazi ya mikono yako?


Lakini yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika.


Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye atuonyaye kutoka mbinguni;


Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo tuliyoyasikia tusije tukayakosa.


Naye alipotazama, akamwona huyo mtu msafiri katika eneo la mji lililokuwa wazi; huyo mzee akamwuliza, Unaenda wapi na umetoka wapi?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo