Methali 19:1 - Swahili Revised Union Version Afadhali maskini aendaye katika uadilifu wake, Kuliko mpotovu wa midomo aliye mpumbavu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Afadhali maskini aishiye kwa unyofu, kuliko mtu mpotovu wa maneno na mpumbavu. Biblia Habari Njema - BHND Afadhali maskini aishiye kwa unyofu, kuliko mtu mpotovu wa maneno na mpumbavu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Afadhali maskini aishiye kwa unyofu, kuliko mtu mpotovu wa maneno na mpumbavu. Neno: Bibilia Takatifu Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama, kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka. Neno: Maandiko Matakatifu Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama, kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka. BIBLIA KISWAHILI Afadhali maskini aendaye katika uadilifu wake, Kuliko mpotovu wa midomo aliye mpumbavu. |
Yeye aendaye kwa unyofu wake humcha BWANA; Bali aliye mkaidi katika njia zake humdharau.
Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong'ona uovu.
Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kuipoteza nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Basi sasa ujue na kufikiri utakayotenda; kwa sababu yamekusudiwa mabaya juu ya bwana wetu, na juu ya nyumba yake yote; kwa kuwa yeye ni mtu asiyefaa kabisa, hata mtu hawezi kusema naye.
Nakusihi, bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani Nabali; kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma.