Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Methali 18:6 - Swahili Revised Union Version

Midomo ya mpumbavu huingia katika fitina, Na kinywa chake huita mapigo.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Maneno ya mpumbavu huleta ugomvi; kila anachosema husababisha adhabu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Maneno ya mpumbavu huleta ugomvi; kila anachosema husababisha adhabu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Maneno ya mpumbavu huleta ugomvi; kila anachosema husababisha adhabu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Midomo ya mpumbavu humletea ugomvi na kinywa chake hualika kipigo.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Midomo ya mpumbavu humletea ugomvi na kinywa chake hualika kipigo.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Midomo ya mpumbavu huingia katika fitina, Na kinywa chake huita mapigo.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Methali 18:6
14 Marejeleo ya Msalaba  

Ghadhabu ya mpumbavu hujulikana mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu.


Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.


Mwenye hekima huhadhari, na kujitenga na uovu; Bali mpumbavu hupuuza yote, na hajali.


Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi.


Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji; Basi acheni ugomvi kabla haujafurika.


Mtu wa hasira nyingi atachukua adhabu yake, Maana ujapomwokoa huna budi kufanya tena.


Hukumu zimewekwa tayari kwa wenye mzaha; Na mapigo kwa mgongo wa wapumbavu.


Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake; Bali kila mpumbavu ataka kugombana.


Mtupe nje mwenye dharau, na ugomvi utatoka; Naam, fitina na fedheha zitakoma.


Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.


Jiwe ni zito, na mchanga hulemea; Lakini ghadhabu ya mpumbavu ni nzito kuliko hivi vyote viwili.


Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu; Akikasirika au akicheka, pia hapana raha.