Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 14:16 - Swahili Revised Union Version

16 Mwenye hekima huhadhari, na kujitenga na uovu; Bali mpumbavu hupuuza yote, na hajali.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Mwenye hekima ni mwangalifu na huepa uovu, lakini mpumbavu hajizuii wala hana uangalifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Mwenye hekima ni mwangalifu na huepa uovu, lakini mpumbavu hajizuii wala hana uangalifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Mwenye hekima ni mwangalifu na huepa uovu, lakini mpumbavu hajizuii wala hana uangalifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Mtu mwenye hekima humcha Mwenyezi Mungu na kuepuka mabaya, bali mpumbavu hukasirika kwa hamaki na uzembe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Mtu mwenye hekima humcha bwana na kuepuka mabaya, bali mpumbavu hukasirika kwa hamaki na uzembe.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 Mwenye hekima hujihadhari, na kujitenga na uovu; Bali mpumbavu hupuuza yote, na hajali.

Tazama sura Nakili




Methali 14:16
27 Marejeleo ya Msalaba  

Esau akasema, Ninayo tele, ndugu yangu, hifadhi uliyo nayo yawe yako.


Siku ya tatu, Yusufu akawaambia, Fanyeni hivi, mkaishi, maana mimi namcha Mungu.


Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao.


Akasema, Kwamba wametoka kwa amani, wakamateni wa hai; au kwamba wametoka kwa vita, wakamateni wa hai.


Lakini watawala wa kwanza walionitangulia, wakawalemea watu, wakawatwalia chakula na mvinyo, zaidi ya shekeli arubaini za fedha; tena hata watumishi wao nao wakawatawala watu; lakini mimi sikufanya hivyo, kwa kuwa nilimcha Mungu.


Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.


Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.


Mwili wangu unatetemeka kwa kukucha Wewe, Nami ninaziogopa hukumu zako.


Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie.


Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.


Mjinga huamini kila neno; Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo.


Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga; Na mtu mwenye hila mbaya huzirwa.


Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu; Yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake.


Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu.


Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.


Mwanadamu mwenye kicho yu heri sikuzote; Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara.


Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu; Akikasirika au akicheka, pia hapana raha.


Usiwe na hekima machoni pako; Mche BWANA, ukajiepushe na uovu.


Huyo akafuatana naye mara hiyo, Kama vile ng'ombe aendavyo machinjoni; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu;


Mwanzo wa maneno ya kinywa chake ni upuuzi; na mwisho wa usemi wake ni wazimu wenye hatari.


Yule punda akamwona malaika wa BWANA, akajilaza chini ya Balaamu; hasira yake Balaamu ikawaka, akampiga punda kwa fimbo yake.


Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu?


jitengeni na ubaya wa kila namna.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo