Methali 16:2 - Swahili Revised Union Version Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huzipima roho za watu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Matendo ya mtu huonekana kwake kuwa sawa, lakini Mwenyezi-Mungu hupima nia ya mtu. Biblia Habari Njema - BHND Matendo ya mtu huonekana kwake kuwa sawa, lakini Mwenyezi-Mungu hupima nia ya mtu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Matendo ya mtu huonekana kwake kuwa sawa, lakini Mwenyezi-Mungu hupima nia ya mtu. Neno: Bibilia Takatifu Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe, bali makusudi hupimwa na Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe, bali makusudi hupimwa na bwana. BIBLIA KISWAHILI Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huzipima roho za watu. |
Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri.
Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye? Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?
Kwa maana njia za mwanadamu ziko mbele ya macho ya BWANA, Na mienendo yake yote huitafakari.
Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.
Malaika wa BWANA akamwambia, Mbona umempiga punda wako mara tatu hizi? Tazama mimi nimekuja ili kukupinga, kwa sababu njia yako imepotoka mbele zangu,
Akawaambia, Ninyi ndinyi mnaojidai haki mbele ya wanadamu, lakini Mungu awajua mioyo yenu; kwa kuwa lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu.
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama muali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.
nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye fikira na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli; kila mtu alifanya hayo aliyoyaona kuwa ni mema machoni pake mwenyewe.
Na hesabu ya hao waliokunywa kwa kuramba-ramba, wakipeleka mkono kinywani, ilikuwa watu mia tatu; bali watu wengine wote walipiga magoti kunywa maji.
Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.
Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa, Naye huyapima matendo kwa mizani.