Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 17:3 - Swahili Revised Union Version

3 Kalibu ni kwa fedha, na tanuri kwa dhahabu; Bali BWANA huijaribu mioyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Ubora wa dhahabu ama fedha hupimwa kwa moto, lakini Mwenyezi-Mungu ndiye apimaye mioyo ya watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Ubora wa dhahabu ama fedha hupimwa kwa moto, lakini Mwenyezi-Mungu ndiye apimaye mioyo ya watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Ubora wa dhahabu ama fedha hupimwa kwa moto, lakini Mwenyezi-Mungu ndiye apimaye mioyo ya watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Kalibu husafisha fedha na tanuru husafisha dhahabu, bali Mwenyezi Mungu huujaribu moyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu, bali bwana huujaribu moyo.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Kalibu ni kwa fedha, na tanuri kwa dhahabu; Bali BWANA huijaribu mioyo.

Tazama sura Nakili




Methali 17:3
21 Marejeleo ya Msalaba  

Nami ninajua, Mungu wangu, ya kuwa wewe wajaribu moyo, nawe wapendezwa na unyofu. Nami katika unyofu wa moyo wangu nimeyatoa haya yote kwa hiari yangu mwenyewe; nami sasa nimeona kwa furaha watu wako, waliopo hapa, wakikutolea kwa hiari yao.


Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.


Hakika kuna shimo wachimbako fedha, Na mahali wapatapo dhahabu waisafishayo.


Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu;


Ee BWANA, unijaribu na kunipima; Unisafishe akili yangu na moyo wangu.


Kwa maana umetupima, Ee Mungu, Umetujaribu inavyojaribiwa fedha.


Kuzimu na Uharibifu viko wazi mbele za BWANA; Si zaidi basi, mioyo ya wanadamu?


Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huzipima roho za watu.


Mtumwa atendaye kwa busara atamtawala mwana atendaye mambo ya aibu; Tena atapata sehemu ya urithi kati ya ndugu.


Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huipima mioyo.


Kalibu ni kwa fedha, na tanuri kwa dhahabu; Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake.


Tazama, nimekusafisha, lakini si kama fedha; nimekuchagua katika tanuri ya mateso.


Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.


Mwanadamu, nyumba ya Israeli imekuwa taka za fedha kwangu; wote wamekuwa shaba, na bati, na chuma, na risasi, katika tanuri; wamekuwa taka za fedha.


Na baadhi yao wenye hekima wataanguka, ili kuwatakasa, na kuwasafisha, na kuwafanya weupe, hata wakati wa mwisho; kwa maana ni kwa wakati ulioamriwa, ambao haujaja.


Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.


aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako.


Nawe utaikumbuka njia ile yote BWANA, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arubaini katika jangwa, ili akunyenyekeze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.


ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.


nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye fikira na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo