Methali 15:6 - Swahili Revised Union Version Katika nyumba ya mwenye haki mna akiba nyingi; Bali mapato ya mtu mbaya huwa taabu tu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyumbani mwa mwadilifu mna wingi wa mali, lakini mapato ya waovu huishia na balaa. Biblia Habari Njema - BHND Nyumbani mwa mwadilifu mna wingi wa mali, lakini mapato ya waovu huishia na balaa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyumbani mwa mwadilifu mna wingi wa mali, lakini mapato ya waovu huishia na balaa. Neno: Bibilia Takatifu Nyumba ya mwenye haki ina hazina kubwa, bali mapato ya waovu huwaletea taabu. Neno: Maandiko Matakatifu Nyumba ya mwenye haki ina hazina kubwa, bali mapato ya waovu huwaletea taabu. BIBLIA KISWAHILI Katika nyumba ya mwenye haki mna akiba nyingi; Bali mapato ya mtu mbaya huwa taabu tu. |
Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.
Kuna hazina ya thamani na mafuta katika maskani ya mwenye hekima; Bali mwanadamu aliye mpumbavu huyameza.
Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kufukuza upepo.
akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.