Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Methali 13:22 - Swahili Revised Union Version

22 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Mtu mwema huwaachia urithi uzao wake, lakini mali ya mwenye dhambi imerundikiwa waadilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Mtu mwema huwaachia urithi uzao wake, lakini mali ya mwenye dhambi imerundikiwa waadilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Mtu mwema huwaachia urithi uzao wake, lakini mali ya mwenye dhambi imerundikiwa waadilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi, bali mali ya wenye dhambi imehifadhiwa kwa ajili ya wenye haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi, bali mali ya wenye dhambi imehifadhiwa kwa ajili ya wenye haki.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

22 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.

Tazama sura Nakili

Methali 13:22
11 Marejeleo ya Msalaba  

Basi, msiwape wana wao binti zenu, wala msitwae binti zao kuwa wake za wana wenu, wala msiwatakie amani wala kufanikiwa milele; ili mpate kuwa hodari, na kula wema wa nchi hiyo, na kuwaachia watoto wenu iwe urithi wa milele.

Wana wa watumishi wako watakaa, Na wazawa wao wataimarishwa mbele zako.

Wazawa wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.

Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.

Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzawa wake akiomba chakula.

Wana wa wana ndio taji la wazee, Na utukufu wa watoto ni baba zao.

Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.

Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo