Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 3:33 - Swahili Revised Union Version

33 Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Mwenyezi-Mungu huapiza nyumba za waovu, lakini huyabariki makao ya waadilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Mwenyezi-Mungu huapiza nyumba za waovu, lakini huyabariki makao ya waadilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Mwenyezi-Mungu huapiza nyumba za waovu, lakini huyabariki makao ya waadilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 Laana ya Mwenyezi Mungu i juu ya nyumba ya mwovu, lakini yeye huibariki nyumba ya mwenye haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 Laana ya bwana i juu ya nyumba ya mwovu, lakini yeye huibariki nyumba ya mwenye haki.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

33 Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki.

Tazama sura Nakili




Methali 3:33
20 Marejeleo ya Msalaba  

Sanduku la BWANA akalitia katika nyumba ya Obed-edomu, Mgiti, muda wa miezi mitatu; naye BWANA akambariki Obed-edomu, na nyumba yake yote.


Mwasema, Yeye ni mwepesi juu ya uso wa gharika; Sehemu yao inalaaniwa duniani; Hageuki kwenda njia ya mizabibuni.


Kwa kuwa ni moto uteketezao hata Uharibifu, Nao ungeyang'oa mavuno yangu yote.


Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.


Maana waliobarikiwa na BWANA watairithi nchi, Nao waliolaaniwa naye watakatiliwa mbali.


Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.


Baraka humkalia mwenye haki kichwani; Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu.


Nyumba ya mtu mwovu itabomolewa; Bali hema la mwenye haki litafanikiwa.


Katika nyumba ya mwenye haki mna akiba nyingi; Bali mapato ya mtu mbaya huwa taabu tu.


Mwenye haki huitafakari nyumba ya mtu mbaya; Jinsi wabaya waangushwavyo wakaangamia.


Kama hamtaki kusikia, na kama hamtaki kuitia moyoni, ili kulitukuza jina langu, asema BWANA wa majeshi, basi nitawaleteeni laana, nami nitazilaani baraka zenu; naam, nimekwisha kuzilaani, kwa sababu hamyatii haya moyoni.


na laana ni hapo msipotii maagizo ya BWANA, Mungu wenu, mkapotoka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.


na usitie kitu kilicho haramu ndani ya nyumba yako, usije ukalaaniwa kama haramu hiyo; ukichukie kabisa na kukikataa kabisa, kwa kuwa ni kitu kilicholaaniwa.


Na ninyi, msikose kujiepusha na kitu kilichowekwa wakfu; msije mkakitwaa kitu kilichowekwa wakfu, baada ya kukiweka wakfu; nanyi hivyo mtaifanya kambi ya Israeli kuwa imelaaniwa na kuifadhaisha.


Haya! Inuka, uwatakase watu, ukaseme, Jitakaseni, muwe tayari kesho; maana BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi; Kitu kilichowekwa wakfu kiko katikati yako, Ee Israeli; huwezi kusimama mbele ya adui zako, hata mtakapokiondoa kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo