Kwa kuwa jamii ya hao wasiomcha Mungu watakuwa tasa, Na moto utateketeza mahema yenye rushwa.
Methali 14:11 - Swahili Revised Union Version Nyumba ya mtu mwovu itabomolewa; Bali hema la mwenye haki litafanikiwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyumba ya mtu mwovu itabomolewa, lakini hema ya wanyofu itaimarishwa. Biblia Habari Njema - BHND Nyumba ya mtu mwovu itabomolewa, lakini hema ya wanyofu itaimarishwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyumba ya mtu mwovu itabomolewa, lakini hema ya wanyofu itaimarishwa. Neno: Bibilia Takatifu Nyumba ya mwovu itaangamizwa, bali hema la mnyofu litastawi. Neno: Maandiko Matakatifu Nyumba ya mwovu itaangamizwa, bali hema la mnyofu litastawi. BIBLIA KISWAHILI Nyumba ya mtu mwovu itabomolewa; Bali hema la mwenye haki litafanikiwa. |
Kwa kuwa jamii ya hao wasiomcha Mungu watakuwa tasa, Na moto utateketeza mahema yenye rushwa.
Ikiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa.
Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Katika nyumba yako. Wanao watakuwa kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako.
Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo, Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo.
Kuna hazina ya thamani na mafuta katika maskani ya mwenye hekima; Bali mwanadamu aliye mpumbavu huyameza.
Nitaituma itokee, asema BWANA wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi, na katika nyumba ya yeyote aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katika nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.