Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 15:25 - Swahili Revised Union Version

25 BWANA ataing'oa nyumba ya mwenye kiburi; Bali atauthibitisha mpaka wa mjane.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Mwenyezi-Mungu huyabomoa makao ya wenye kiburi, lakini huilinda mipaka ya makao ya mjane.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Mwenyezi-Mungu huyabomoa makao ya wenye kiburi, lakini huilinda mipaka ya makao ya mjane.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Mwenyezi-Mungu huyabomoa makao ya wenye kiburi, lakini huilinda mipaka ya makao ya mjane.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Mwenyezi Mungu hubomoa nyumba ya mtu mwenye kiburi, bali huilinda mipaka ya mjane isiguswe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 bwana hubomoa nyumba ya mtu mwenye kiburi, bali huilinda mipaka ya mjane isiguswe.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

25 BWANA ataing'oa nyumba ya mwenye kiburi; Bali atauthibitisha mpaka wa mjane.

Tazama sura Nakili




Methali 15:25
20 Marejeleo ya Msalaba  

Naam, yeye huwala walio tasa wasiozaa; Wala hamtendei mema mwanamke mjane.


Umeona, maana unaangalia matatizo na dhiki, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima.


Ingawa BWANA yuko juu, anamjali mnyenyekevu, Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali.


BWANA huwahifadhi wageni; Huwategemeza yatima na mjane; Bali njia ya wasio haki huiharibu.


Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote.


Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung'oa katika nchi ya walio hai.


Waovu huangamia, hata hawako tena; Bali nyumba ya mwenye haki itasimama.


Nyumba ya mtu mwovu itabomolewa; Bali hema la mwenye haki litafanikiwa.


Ushauri mbaya ni chukizo kwa BWANA; Bali maneno yapendezayo ni safi.


Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani; Wala usiingie katika mashamba ya yatima;


jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.


Kwa maana kutakuwa siku ya BWANA wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini.


Wamenenepa sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji.


Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, alishushwa katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake.


Usiiondoe alama ya mpaka wa jirani yako, waliouweka watu wa kale katika urithi wako, utakaorithi ndani ya nchi akupayo BWANA, Mungu wako, uimiliki.


Dini iliyo safi, isiyo na dosari mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.


Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo