Mistari ya Biblia

Matangazo


Vikundi Vidogo

AYA MAARUFU

Neno la Mungu lina nguvu na linatubadilisha. Kuna mistari mingi ambayo tunasikia mara kwa mara na yenye uwezo wa kutubadilisha. Inaweza kubadilisha mawazo yetu, jinsi tunavyoishi. Ni mistari ambayo tunajifunza ili tuitendee kazi katika kila hali.

"Ninaweza kufanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu." (Wafilipi 4:13). Huu ni mmoja wa mistari ambao tunajifunza mara kwa mara, na tunautumia wakati tunahisi tumekata tamaa. Unatupa nguvu ya kusonga mbele.

"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." (Yohana 3:16). Huu ni moja wapo wa mistari muhimu sana, na ni miongoni mwa mistari ya kwanza unayosikia unapojua kumhusu Bwana wetu Yesu. Ni msitari unaotuonyesha upendo mkubwa wa Mungu kwetu.

Kuna mistari mingine mingi sana ambayo inasemwa mara kwa mara, na hapa utaipata.


Mwanzo 12:3

Anayekubariki, nitambariki; anayekulaani, nitamlaani. Kwako wewe, nitayabariki mataifa yote ya dunia.”

Sura   |  Matoleo
Luka 6:28

Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale wanaowatendea vibaya.

Sura   |  Matoleo
Kumbukumbu la Torati 11:27

Baraka, kama mtatii amri za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ambazo nawapeni hivi leo;

Sura   |  Matoleo
Kumbukumbu la Torati 11:26

“Angalieni, leo hii nawawekea mbele yenu baraka na laana:

Sura   |  Matoleo
Zekaria 8:13

Enyi watu wa Yuda na watu wa Israeli! Wakati uliopita nyinyi mlionekana kuwa watu waliolaaniwa kati ya watu wa mataifa. Lakini sasa mimi nitawaokoeni, nanyi mtakuwa watu waliobarikiwa. Basi, msiogope tena, bali jipeni moyo!”

Sura   |  Matoleo
Yoshua 8:34

Kisha, Yoshua akawasomea sheria zote, pamoja na baraka na laana kama ilivyoandikwa katika kitabu cha sheria.

Sura   |  Matoleo
Yakobo 3:10

Maneno ya kubariki na ya kulaani hutoka katika kinywa kimoja. Ndugu zangu, mambo haya hayapaswi kuwa hivyo.

Sura   |  Matoleo
Yakobo 3:9

Kwa ulimi sisi twamshukuru Bwana na Baba yetu. Kwa ulimi huhuo twawalaani watu, watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu.

Sura   |  Matoleo
Wagalatia 3:13

Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kujitwalia laana hiyo kwa ajili yetu; maana Maandiko yanasema: “Yeyote aliyetundikwa msalabani amelaaniwa.”

Sura   |  Matoleo
Methali 3:33

Mwenyezi-Mungu huapiza nyumba za waovu, lakini huyabariki makao ya waadilifu.

Sura   |  Matoleo
Nehemia 13:2

Maana watu wa Israeli, walipokuwa wanasafiri toka Misri, hawakuwapa chakula wala maji ya kunywa, badala yake walimkodisha Balaamu kuwalaani watu wa Israeli, lakini Mungu wetu aligeuza laana yao kuwa baraka.

Sura   |  Matoleo
Kumbukumbu la Torati 28:1-2

“Kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu na kuzingatia kwa uangalifu amri ambazo ninawaamuru leo, yeye atawaweka juu ya mataifa yote duniani.

Mataifa yote duniani yakiona kwamba nyinyi mnaitwa kwa jina la Mwenyezi-Mungu yatawaogopa.

Mwenyezi-Mungu atawafanikisha kwa wingi: Watoto, mifugo na mavuno shambani katika nchi aliyowaapia wazee wenu kuwa atawapeni,

Mwenyezi-Mungu atawafungulieni hazina yake nzuri kutoka mbinguni na kunyesha mvua katika nchi kwa wakati wake, na kubariki kazi zenu. Mtayakopesha mataifa mengi, lakini nyinyi hamtakopa.

Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawafanya kuwa wa kwanza kwa nguvu na sio wa mwisho. Mtaendelea mbele na sio kurudi nyuma kama mkishika amri zake ambazo ninawapeni leo na kuwa waangalifu kuzitekeleza,

bila kugeuka kulia au kushoto kuifuata miungu mingine na kuitumikia.

“Lakini kama hamtaitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, au msipokuwa waangalifu kutekeleza amri zake zote na masharti ninayowaamuru leo, basi mtapatwa na laana hizi zote:

Mtapata laana katika miji yenu na mashamba yenu.

Vikapu vyenu vya nafaka vitalaaniwa na vyombo vyenu vya kukandia mkate.

Watoto wenu watalaaniwa na mazao yenu ya nchi; mifugo yenu italaaniwa isiongezeke.

Mtalaaniwa mnapoingia na mnapotoka.

Kama mkitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mtapewa baraka zifuatazo;

Sura   |  Matoleo
Kumbukumbu la Torati 28:15

“Lakini kama hamtaitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, au msipokuwa waangalifu kutekeleza amri zake zote na masharti ninayowaamuru leo, basi mtapatwa na laana hizi zote:

Sura   |  Matoleo
Kumbukumbu la Torati 30:19-20

Naziita mbingu na dunia zishuhudie juu yenu leo hii, kwamba nimewapeni uchaguzi kati ya uhai na kifo, kati ya baraka na laana. Basi, chagueni uhai nyinyi na wazawa wenu mpate kuishi,

mkamrudia Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, nyinyi na watoto wenu, mkatii kwa moyo wote na roho yote neno lake ninalowaamuru leo,

mkimpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mkiitii sauti yake na kuambatana naye. Maana kufanya hivyo kunamaanisha kwamba mtapata maisha marefu na kuishi katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu aliwaahidi wazee wenu, Abrahamu, Isaka na Yakobo, kwamba atawapeni.”

Sura   |  Matoleo
Zaburi 37:22

Waliobarikiwa na Mwenyezi-Mungu wataimiliki nchi, lakini waliolaaniwa naye watafutiliwa mbali.

Sura   |  Matoleo
Kumbukumbu la Torati 30:1

Mose akaendelea kusema, “Nimewapeni uchaguzi kati ya baraka na laana. Mambo hayo yote yakiwapata nanyi mkiyatafakari popote mlipo miongoni mwa mataifa ambamo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atakuwa amewatawanya,

Sura   |  Matoleo
1 Wakorintho 4:12

Tena twataabika na kufanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa, tunawatakia baraka; tukidhulumiwa, tunavumilia;

Sura   |  Matoleo
Kumbukumbu la Torati 11:26-28

“Angalieni, leo hii nawawekea mbele yenu baraka na laana:

Baraka, kama mtatii amri za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ambazo nawapeni hivi leo;

na laana, kama hamtazitii amri za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kuiacha njia ninayowaamuru, mkaabudu miungu mingine ambayo hata hamjawahi kuijua.

Sura   |  Matoleo
Kumbukumbu la Torati 28:2

Kama mkitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mtapewa baraka zifuatazo;

Sura   |  Matoleo
Mwanzo 3:17

Kisha akamwambia huyo mwanamume, “Kwa kuwa wewe umemsikiliza mkeo, ukala matunda ya mti ambayo nilikuamuru usile; kwa hiyo, kwa kosa lako ardhi imelaaniwa. Kwa jasho utajipatia humo riziki yako, siku zote za maisha yako.

Sura   |  Matoleo
Wagalatia 6:7

Msidanganyike; Mungu hafanyiwi dhihaka. Alichopanda mtu ndicho atakachovuna.

Sura   |  Matoleo
Kumbukumbu la Torati 30:19

Naziita mbingu na dunia zishuhudie juu yenu leo hii, kwamba nimewapeni uchaguzi kati ya uhai na kifo, kati ya baraka na laana. Basi, chagueni uhai nyinyi na wazawa wenu mpate kuishi,

Sura   |  Matoleo
Zaburi 62:4

Mmepanga kuniangusha toka mahali pangu pa heshima; furaha yenu ni kusema uongo. Kwa maneno, mnabariki, lakini moyoni mnalaani.

Sura   |  Matoleo
Hesabu 22:6

Njoo sasa uwalaani watu hawa kwa ajili yangu maana wana nguvu kuliko mimi. Labda nitaweza kuwashinda na kuwafukuza wasiingie katika nchi yangu, kwa maana najua kuwa wewe ukimbariki mtu hubarikiwa, ukimlaani mtu hulaaniwa.”

Sura   |  Matoleo
Methali 10:22

Baraka za Mwenyezi-Mungu ndizo ziletazo fanaka, juhudi za mtu haziongezi hapo chochote.

Sura   |  Matoleo
Methali 26:12

Wamwona mtu ajionaye kuwa mwenye hekima? Nakuambia mpumbavu ni nafuu kuliko huyo.

Sura   |  Matoleo
Walawi 20:9

Mtu yeyote amlaaniye baba yake au mama yake, ni lazima auawe. Amemlaani baba au mama yake, kwa hiyo damu yake itakuwa juu yake.

Sura   |  Matoleo
Malaki 2:2

Ni lazima mniheshimu mimi kwa matendo yenu, msiponisikiliza nitawaleteeni laana, vitu vyote mnavyopewa kwa mahitaji yenu nitavilaani. Na kweli nimekwisha kuvilaani, kwa sababu hamuyatilii maanani maagizo yangu.

Sura   |  Matoleo
Kutoka 21:17

“Amlaaniye baba yake au mama yake lazima auawe.

Sura   |  Matoleo
Hesabu 6:24-26

‘Mwenyezi-Mungu awabariki na kuwalinda;

Mwenyezi-Mungu awaangalie kwa wema, na kuwafadhili;

Mwenyezi-Mungu awaoneshe wema wake na kuwapa amani.’

Sura   |  Matoleo
Zaburi 1:1-3

Heri mtu asiyefuata shauri la waovu, asiyeshiriki njia za wenye dhambi, wala kujumuika na wenye dharau;

bali huifurahia sheria ya Mwenyezi-Mungu, na kuitafakari mchana na usiku.

Huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito, unaozaa matunda kwa wakati wake, na majani yake hayanyauki. Kila afanyalo hufanikiwa.

Sura   |  Matoleo
Waroma 12:14

Watakieni baraka wote wanaowadhulumu nyinyi; naam, watakieni baraka na wala msiwalaani.

Sura   |  Matoleo
Waefeso 4:29

Maneno mabaya hata yasisikike kamwe miongoni mwenu; kila mara maneno yenu yawe ya kufaa na ambayo hujenga na kuwasaidia wengine, ili yawaneemeshe wasikilizaji wenu.

Sura   |  Matoleo
Wagalatia 3:13-14

Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kujitwalia laana hiyo kwa ajili yetu; maana Maandiko yanasema: “Yeyote aliyetundikwa msalabani amelaaniwa.”

Jambo hili lilifanyika kusudi ile baraka aliyopewa Abrahamu iwashukie watu wa mataifa mengine kwa njia ya Kristo, na ili kwa imani, tumpokee yule Roho ambaye Mungu alituahidia.

Sura   |  Matoleo
Zaburi 112:1-3

Msifuni Mwenyezi-Mungu! Heri mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu, anayefurahia sana kutii amri zake.

Watu waovu huona hayo na kuudhika; husaga meno kwa chuki na kutoweka, matazamio ya mtu mbaya huishia patupu.

Wazawa wake watakuwa wenye nguvu nchini; watoto wa wanyofu watapata baraka.

Nyumbani kwake kutakuwa na mali nyingi; uadilifu wake wadumu milele.

Sura   |  Matoleo
Kumbukumbu la Torati 28:1-14

“Kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu na kuzingatia kwa uangalifu amri ambazo ninawaamuru leo, yeye atawaweka juu ya mataifa yote duniani.

Mataifa yote duniani yakiona kwamba nyinyi mnaitwa kwa jina la Mwenyezi-Mungu yatawaogopa.

Mwenyezi-Mungu atawafanikisha kwa wingi: Watoto, mifugo na mavuno shambani katika nchi aliyowaapia wazee wenu kuwa atawapeni,

Mwenyezi-Mungu atawafungulieni hazina yake nzuri kutoka mbinguni na kunyesha mvua katika nchi kwa wakati wake, na kubariki kazi zenu. Mtayakopesha mataifa mengi, lakini nyinyi hamtakopa.

Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawafanya kuwa wa kwanza kwa nguvu na sio wa mwisho. Mtaendelea mbele na sio kurudi nyuma kama mkishika amri zake ambazo ninawapeni leo na kuwa waangalifu kuzitekeleza,

bila kugeuka kulia au kushoto kuifuata miungu mingine na kuitumikia.

Sura   |  Matoleo
Mathayo 5:6

Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.

Sura   |  Matoleo
Methali 18:21

Ulimi una nguvu ya kufanya hai na kuua; wanaopenda kuutumia watakula matunda yake.

Sura   |  Matoleo
Zaburi 94:23

Uovu wao atawarudishia wao wenyewe, atawafutilia mbali kwa sababu ya ubaya wao. Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, atawafutilia mbali!

Sura   |  Matoleo
Zaburi 34:8

Jaribuni mwone Mwenyezi-Mungu alivyo mwema. Heri mtu anayekimbilia usalama kwake.

Sura   |  Matoleo
Yobu 1:21

Akasema, “Uchi nilikuja duniani, uchi nitaondoka duniani; Mwenyezi-Mungu amenipa, Mwenyezi-Mungu amechukua; litukuzwe jina lake Mwenyezi-Mungu.”

Sura   |  Matoleo
Yakobo 3:10-12

Maneno ya kubariki na ya kulaani hutoka katika kinywa kimoja. Ndugu zangu, mambo haya hayapaswi kuwa hivyo.

Je, chemchemi moja yaweza kutoa maji matamu na maji machungu pamoja?

Ndugu zangu, je, mtini waweza kuzaa zeituni? Au, mzabibu waweza kuzaa tini? Chemchemi ya maji ya chumvi haiwezi kutoa maji matamu.

Sura   |  Matoleo
1 Petro 3:9

Msiwalipe watu ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi; bali watakieni baraka, maana nyinyi mliitwa na Mungu mpate kupokea baraka.

Sura   |  Matoleo
Zaburi 30:5

Hasira yake hudumu kitambo kidogo, wema wake hudumu milele. Kilio chaweza kuwapo hata usiku, lakini asubuhi huja furaha.

Sura   |  Matoleo
Wagalatia 6:7-8

Msidanganyike; Mungu hafanyiwi dhihaka. Alichopanda mtu ndicho atakachovuna.

Apandaye katika tamaa za kidunia, atavuna humo uharibifu; lakini akipanda katika Roho, atavuna kutoka kwa Roho uhai wa milele.

Sura   |  Matoleo
Zaburi 65:4

Heri wale unaowachagua na kuwaleta karibu, waishi katika maskani yako. Sisi tutatoshelezwa na mema ya nyumba yako; mema ya hekalu lako takatifu.

Sura   |  Matoleo
Mathayo 25:34

“Kisha Mfalme atawaambia wale walio upande wake wa kulia, ‘Njoni enyi mliobarikiwa na Baba yangu; pokeeni ufalme mliotayarishiwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Sura   |  Matoleo
Zaburi 107:38

Aliwabariki watu wake, wakaongezeka; na idadi ya wanyama wao akaizidisha.

Sura   |  Matoleo
Zaburi 112:1

Msifuni Mwenyezi-Mungu! Heri mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu, anayefurahia sana kutii amri zake.

Sura   |  Matoleo
Zaburi 119:35

Uniongoze katika njia ya amri zako, maana humo napata furaha yangu.

Sura   |  Matoleo
Kutoka 20:5

Usiisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha hao wanichukiao.

Sura   |  Matoleo
Kutoka 23:25-26

Mtanitumikia mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, nami nitawabariki kwa chakula na maji na kuyaondoa magonjwa kati yenu.

Hakutakuwa na mwanamke yeyote atakayepoteza mimba wala kuwa tasa katika nchi yenu. Nami nitawajalia maisha marefu.

Sura   |  Matoleo
Methali 19:17

Anayemsaidia maskini anamkopesha Mwenyezi-Mungu; Mwenyezi-Mungu atamlipa kwa tendo lake jema.

Sura   |  Matoleo
Luka 6:38

Wapeni wengine wanavyohitaji, nanyi mtapewa. Naam, mtapokea mikononi mwenu kipimo kilichojaa, kikashindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika. Kwa maana kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho atakachotumia Mungu kwenu.”

Sura   |  Matoleo
Zaburi 128:1-2

Heri wote wamchao Mwenyezi-Mungu, wanaoishi kufuatana na amri zake.

Utapata matunda ya jasho lako, utafurahi na kupata fanaka.

Sura   |  Matoleo
Waroma 15:29

Najua ya kuwa nikija kwenu nitawaletea wingi wa baraka za Kristo.

Sura   |  Matoleo
Waebrania 11:20

Kwa imani Isaka aliwabariki Yakobo na Esau, wapate baraka zitakazokuja baadaye.

Sura   |  Matoleo
Zaburi 119:17

Unitendee mimi mtumishi wako kwa ukarimu, nipate kuishi na kushika neno lako.

Sura   |  Matoleo
Waebrania 11:6

Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa maana kila mtu anayemwendea Mungu ni lazima aamini kwamba Mungu yuko, na kwamba huwatuza wale wanaomtafuta.

Sura   |  Matoleo
Methali 11:11

Mji hufanikishwa kwa baraka za wanyofu, lakini huangamizwa kwa mdomo wa waovu.

Sura   |  Matoleo
Mhubiri 3:13

Sote inatupasa kula na kunywa na kufurahia matunda ya kazi zetu. Hayo ni majaliwa ya Mungu.

Sura   |  Matoleo
Kumbukumbu la Torati 26:2

baadhi ya malimbuko ya mazao utakayovuna katika nchi anayokupa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, utayachukua katika kikapu mpaka pale mahali ambapo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amepachagua pawe makao yake.

Sura   |  Matoleo
Methali 22:9

Mtu mkarimu atabarikiwa, maana chakula chake humgawia maskini.

Sura   |  Matoleo
Zaburi 16:5-6

Wewe ee Mwenyezi-Mungu ndiwe riziki yangu kuu, majaliwa yangu yamo mikononi mwako.

Umenipimia sehemu nzuri sana; naam, urithi wangu ni wa kupendeza.

Sura   |  Matoleo
Isaya 65:16

Basi, mwenye kujitakia baraka nchini, atajitakia baraka kwa Mungu wa kweli. Mwenye kuapa katika nchi hii, ataapa kwa Mungu wa kweli. Maana taabu za zamani zimepita zimetoweka kabisa mbele yangu.

Sura   |  Matoleo
Yeremia 17:7-8

“Abarikiwe mtu anayemtegemea Mwenyezi-Mungu, mtu ambaye Mwenyezi-Mungu ndiye tegemeo lake.

Huyo ni kama mti uliopandwa kando ya maji, upenyezao mizizi yake karibu na chemchemi. Hauogopi wakati wa joto ufikapo, majani yake hubaki mabichi. Hauhangaiki katika mwaka wa ukame, na hautaacha kuzaa matunda.

Sura   |  Matoleo
Zaburi 68:19

Mwenyezi-Mungu asifiwe siku kwa siku! Yeye hutubebea mizigo yetu; yeye ndiye Mungu wa wokovu wetu.

Sura   |  Matoleo
Methali 21:21

Anayepania uadilifu na huruma, ataishi maisha marefu na kuheshimiwa.

Sura   |  Matoleo
Methali 4:7

Jambo la msingi ni kujipatia hekima; toa vyote ulivyonavyo ujipatie akili.

Sura   |  Matoleo
Mwanzo 12:2-3

Nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, nitakubariki na kulikuza jina lako, nawe uwe baraka.

Kisha Farao aliwaamuru watu wake, nao wakamsindikiza Abramu njiani akiwa na mke wake na mali yake yote.

Anayekubariki, nitambariki; anayekulaani, nitamlaani. Kwako wewe, nitayabariki mataifa yote ya dunia.”

Sura   |  Matoleo

Maombi kwa Mungu

Asante Mungu wangu, wewe ndiye mponyaji wangu, mpaji wangu, mlinzi wangu, wewe ndiye upigana vita vyangu na unayenipeleka kutoka utukufu hadi utukufu. Katika jina la Yesu, nakushukuru kwa neno lako, ndio chakula changu bora na ndani yake ndimo ukuaji wangu wa kiroho ulivyo. Neno lako ndilo taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu, linalonilinda nisiteleze. Nipe hekima yako nijue na nikuelewe kupitia hilo. Wewe ndiye unayenishikilia na kuniambia, "Usiogope, mimi nitakusaidia." Leo nakuomba usimamishe ufalme wako maishani mwangu na katika familia yangu. Asante kwa kuwa neno lako linasema, "Wewe ndiwe kimbilio langu na nguvu zangu, msaada wangu wa haraka wakati wa taabu." Katika wakati huu mgumu, najua unanilinda na ninatangaza kwamba hata nipitapo katika bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya. Tawanya giza lote, acha nuru ya Kristo iangaze maishani mwangu na nyumbani mwangu. Katika jina la Yesu. Amina!