Biblia Todo Logo
Mistari ya Biblia
- Matangazo -


AYA ZA MATUKIO MAALUM

AYA ZA MATUKIO MAALUM

Tunamtukuza Mungu kwa kila tukio au siku maalum tunayoishi. Ni siku za furaha na sherehe. Mungu hufurahi tunapotembea kwa amani na furaha.

Bariki jina lake katika siku hizo, na kumbuka ni Yeye anayekupa nafasi ya kuishi nyakati hizi za baraka. Kama Zaburi 30:11-12 inavyosema, "Umegeuza maombolezo yangu kuwa ngoma, umevua gunia langu, ukanivika furaha, ili roho yangu ikuimbie sifa wala nyamaze. Ee Bwana, Mungu wangu, nitakushukuru milele."

Katika Biblia, utapata mistari mingi kuhusu matukio maalum. Sasa, ngoja tuangalie baadhi yake.


Hosea 9:5

Mtafanya nini katika sikukuu ile iliyopangwa, au katika karamu ya Mwenyezi-Mungu?

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Mambo ya Nyakati 30:23

watu waliamua kwa kauli moja kuziendeleza sherehe kwa muda wa siku saba zaidi. Basi, wakaendelea kusherehekea kwa furaha kuu kwa muda wa siku saba zaidi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 34:18

“Mtaiadhimisha sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu. Kwa muda wa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu wakati uliopangwa katika mwezi wa Abibu, kama nilivyowaamuru, kwa sababu katika mwezi huo wa Abibu mlitoka Misri.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 23:15

Mtaadhimisha sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu: Kama nilivyowaagiza, mtakula mikate isiyotiwa chachu kwa siku saba wakati uliopangwa katika mwezi wa Abibu, kwa sababu katika mwezi huo mlitoka Misri. Mtu yeyote asije mbele yangu mikono mitupu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 31:16

Kwa hiyo Waisraeli wataiadhimisha siku ya Sabato katika vizazi vyao vyote kama ishara ya agano la milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 118:24

Hii ndiyo siku aliyoifanya Mwenyezi-Mungu; tushangilie na kufurahi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Nehemia 8:14-15

Wakagundua kuwa, imeandikwa katika kitabu cha sheria kuwa Mwenyezi-Mungu alimwamuru Mose, kwamba watu wanapaswa kukaa vibandani wakati wa sikukuu ya mwezi wa saba. Hivyo wakatangaza katika miji yao yote na huko Yerusalemu, wakisema, “Nendeni milimani, mkalete matawi ya mizeituni, mizeituni mwitu, mihadasi, mitende na miti mingineyo ili kujengea vibanda, kama ilivyoandikwa.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Hosea 2:11

Nitazikomesha starehe zake zote, sikukuu zake za mwezi mwandamo na za Sabato, na sikukuu zote zilizoamriwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 1:13-14

Msiniletee tena matoleo yenu yasiyo na maana; ubani ni chukizo kwangu. Acheni kufanya sikukuu za mwezi mpya, Sabato na mikutano mikubwa ya ibada; sikubali ibada zilizochanganyika na dhambi. Sikukuu zenu za mwezi mpya na nyinginezo moyo wangu wazichukia. Zimekuwa mzigo mzito kwangu, nami nimechoka kuzivumilia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 32:5

Kisha Aroni akamjengea huyo ndama madhabahu, halafu akatangaza, “Kesho kutakuwa na sikukuu kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 66:23

Katika kila sikukuu ya mwezi mpya, na katika kila siku ya Sabato, binadamu wote watakuja kuniabudu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Sura   |  Matoleo Nakili
Hesabu 15:3

mkanitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka kutoka katika mifugo yenu, sadaka ya kuteketezwa au tambiko, ili mtu atimize nadhiri aliyoweka au kutoa sadaka ya hiari au sadaka ya wakati wa sikukuu zenu zilizowekwa, na kufanya harufu nzuri ya kunipendeza mimi Mwenyezi-Mungu,

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 31:10-11

Kisha akawaamuru akasema, “Kila mwaka wa saba utakuwa mwaka wa mafungulio. Katika sikukuu ya vibanda, mwaka huo, wakati watu wa Israeli wanapokuja mbele ya Mwenyezi-Mungu mahali pale atakapochagua mtawasomea watu wote wa Israeli sheria hii.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 23:18

“Usinitolee damu ya tambiko yangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala usiyaache mafuta ya sikukuu yangu yabaki mpaka asubuhi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 14:22-23

“Toeni sehemu moja ya kumi ya mazao yenu yote ya shambani kila mwaka. Halafu nendeni mahali ambapo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu amepachagua kuweka jina lake, na mkiwa mbele yake mtaila zaka ya nafaka yenu, ya divai yenu na ya mafuta, na ya wazaliwa wa kwanza wa ng'ombe na kondoo wenu; fanyeni hivi ili mjifunze kumcha Mwenyezi-Mungu Mungu wenu daima.

Sura   |  Matoleo Nakili
Amosi 8:10

Sherehe zenu nitazigeuza kuwa kilio, na nyimbo zenu za furaha kuwa maombolezo. Nitawafanya nyote mvae magunia kwa huzuni na kunyoa vipara vichwa vyenu, kama kuomboleza kifo cha mtoto wa pekee; na siku ya mwisho itakuwa ya uchungu mkubwa.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 25:8-9

“Mtahesabu miaka saba mara saba na jumla yake ni miaka arubaini na tisa. Kisha, katika siku ya kumi ya mwezi wa saba ambayo ni siku ya kufanyiwa upatanisho mtamtuma mtu kupiga tarumbeta katika nchi yote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 23:6

Siku ya kumi na tano ya mwezi huohuo, sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu itaanza. Kwa muda wa siku saba, mtakula mikate isiyotiwa chachu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ezekieli 45:25

“Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, na kwa muda wa siku saba za sikukuu, mtawala atatoa mahitaji kwa ajili ya sadaka za kuondoa dhambi, sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na mafuta.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ezekieli 45:21

“Siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, mtaadhimisha sikukuu ya Pasaka. Kwa muda wa siku saba, mtakula mikate isiyotiwa chachu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ezra 3:4

Waliiadhimisha sikukuu ya vibanda kama ilivyoandikwa katika sheria; kila siku walitoa sadaka za kuteketezwa zilizohitajika kwa ajili ya siku hiyo.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Mambo ya Nyakati 30:21

Waisraeli wote waliokuwa wamekusanyika mjini Yerusalemu waliiadhimisha sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu kwa muda wa siku saba, wakiwa na furaha kubwa. Walawi na makuhani walimsifu Mwenyezi-Mungu kila siku, walimwimbia kwa nguvu zao zote.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Mambo ya Nyakati 8:13

Alitoa tambiko hizo kadiri ilivyotakiwa na amri ya Mose kila siku takatifu, yaani siku za Sabato, sikukuu za mwezi mwandamo, na sikukuu tatu za kila mwaka – sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, sikukuu ya majuma na sikukuu ya vibanda.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 16:16

“Wanaume wote wa taifa lenu watakuja mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mara tatu kila mwaka, mahali atakapopachagua: Wakati wa sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, sikukuu ya kuvuna majuma na wakati wa sikukuu ya vibanda. Wasiende mbele ya Mwenyezi-Mungu mikono mitupu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Hesabu 28:16

“Siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza ni Pasaka ya Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Hesabu 9:2-3

“Waisraeli sharti waiadhimishe sikukuu ya Pasaka wakati uliopangwa. Wakati mwingine wingu hilo lilikaa juu ya hema kwa muda wa siku chache tu; lakini kila wakati Waisraeli walibaki kambini; walihama kama Mwenyezi-Mungu alivyowaamuru. Wakati mwingine wingu lilikaa juu ya hema tangu jioni mpaka asubuhi tu; na mara tu lilipoinuliwa, hao watu pia walifunga safari. Na ikiwa lilikaa juu ya hema mchana kutwa na usiku kucha, wao waliondoka tu wingu lilipoinuliwa. Ikiwa ni siku mbili, mwezi, mwaka au zaidi, muda wote wingu hilo lilipokuwa juu ya hema, Waisraeli hawakuhama; lakini lilipoinuliwa, nao pia walihama. Kwa agizo la Mwenyezi-Mungu walipiga kambi na kwa agizo la Mwenyezi-Mungu walisafiri. Walishika agizo la Mwenyezi-Mungu kama alivyotoa amri yake kwa njia ya Mose. Hii itakuwa siku ya kumi na nne ya mwezi huu; wakati wa jioni watafanya hivyo kufuatana na masharti na maagizo yake yote.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 23:39

“Baada ya kuvuna mashamba yenu mtafanya sikukuu kwa muda wa siku saba, tangu siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba. Siku ya kwanza itakuwa siku ya mapumziko na hata siku ya nane.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 23:34

“Waambie Waisraeli hivi: Tangu siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba mtamfanyia Mwenyezi-Mungu sikukuu ya vibanda kwa muda wa siku saba. Hiyo ni sikukuu ya Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 23:27

“Siku ya kumi ya mwezi huu wa saba ni siku ya upatanisho. Siku hiyo ni siku ya kuwa na mkutano mtakatifu. Mtafunga na kutoa sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 23:24

“Waambie watu wa Israeli hivi: Siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtaadhimisha siku ya mapumziko rasmi, siku ya ukumbusho itakayotangazwa kwa mlio wa tarumbeta na kufanya mkutano mtakatifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 23:15-16

“Mtahesabu majuma saba kamili tangu siku ile inayofuata Sabato ile ambapo mtaleta mganda wa sadaka ya kunitolea kwa ishara mimi Mwenyezi-Mungu. Mnamo siku ya hamsini, siku ya pili ya Sabato ya saba, mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka ya nafaka mpya.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 23:10-11

“Waambie Waisraeli hivi: Mtakapoingia katika nchi ambayo ninawapeni mkavuna mazao yake, mtamletea kuhani mganda wa mavuno ya kwanza. Kuhani atafanya nayo ishara ya kunitolea siku inayofuata siku ya Sabato ili mpate kukubaliwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 23:5

“Jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza mtaadhimisha kwa heshima yangu mimi Mwenyezi-Mungu sikukuu ya Pasaka.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 23:4

“Sikukuu zangu nyingine mimi Mwenyezi-Mungu ambazo mtakuwa na mkutano mtakatifu zitafanyika katika nyakati zifuatazo zilizopangwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 23:2

“Waambie Waisraeli hivi: Katika sikukuu zangu mimi Mwenyezi-Mungu ambazo zimepangwa mtakuwa na mkutano mtakatifu. Sikukuu ambazo nimepanga ni hizi:

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 13:10

Kwa hiyo, mtaadhimisha sikukuu hii kwa wakati uliopangwa, kila mwaka.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 12:24-27

Shikeni jambo hilo nyinyi na wazawa wenu kama agizo la milele. Mtakapoingia katika nchi ile ambayo mimi Mwenyezi-Mungu nitawapa, kama nilivyoahidi, ni lazima kulitekeleza. Kila wakati watoto wenu watakapowauliza, ‘Jambo hili lina maana gani?’ Nyinyi mtawajibu, ‘Hii ni tambiko ya Pasaka kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu, kwa sababu alizipita nyumba za Waisraeli nchini Misri alipowaua Wamisri, lakini sisi hakutuua.’” Waisraeli wakainamisha vichwa na kumwabudu Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Hesabu 28:17-18

Siku ya kumi na tano ya mwezi huohuo ni sikukuu. Kwa muda wa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu. Katika siku ya kwanza kutakuwa na mkutano mtakatifu. Siku hiyo hamtafanya kazi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Hesabu 29:1

“Siku ya kwanza ya mwezi wa saba, mtafanya mkutano mtakatifu. Msifanye kazi. Hiyo ni siku ya kupiga tarumbeta.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 12:14

Vizazi hata vizazi mtaadhimisha tukio hilo kwa sikukuu kubwa kwa heshima yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Hilo litakuwa agizo la milele kwenu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 16:1

“Adhimisheni mwezi wa Abibu na kufanya Pasaka kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Maana katika mwezi huo wa Abibu, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu aliwatoa Misri wakati wa usiku.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 34:22

Mtaadhimisha sikukuu ya majuma mwanzoni mwa majira ya mavuno ya ngano, na sikukuu ya kukusanya mavuno mwishoni mwa mwaka.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 23:14-16

“Mara tatu kila mwaka mtafanya sikukuu kwa heshima yangu. Mtaadhimisha sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu: Kama nilivyowaagiza, mtakula mikate isiyotiwa chachu kwa siku saba wakati uliopangwa katika mwezi wa Abibu, kwa sababu katika mwezi huo mlitoka Misri. Mtu yeyote asije mbele yangu mikono mitupu. Mtaadhimisha sikukuu ya mavuno ya kwanza ya kazi zenu na ya mavuno ya mashamba yenu. Mtaadhimisha sikukuu ya kukusanya mavuno mwishoni mwa mwaka mnapokusanya mazao ya kazi zenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 16:13-14

“Baada ya kupura nafaka yenu yote na kukamua zabibu zenu, adhimisheni sikukuu ya vibanda kwa muda wa siku saba. Mtafanya sherehe hiyo, nyinyi na watoto wenu wa kiume na wa kike, watumishi wenu, Walawi, wageni, yatima na wajane ambao huishi katika miji yenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 16:10

Halafu mtaadhimisha sikukuu ya majuma kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa kutoa sadaka ya hiari, mtakayotoa kadiri awabarikiavyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zekaria 14:16

Kisha, kila mtu aliyesalimika kati ya mataifa yote yaliyokuja kuushambulia mji wa Yerusalemu, atakuwa akija Yerusalemu mwaka hata mwaka, kumwabudu Mwenyezi-Mungu wa majeshi aliye mfalme, na kuadhimisha sikukuu ya vibanda.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 7:2

Sikukuu ya Wayahudi ya vibanda ilikuwa imekaribia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 2:13

Sikukuu ya Wayahudi ya Pasaka ilikuwa imekaribia; hivyo Yesu akaenda juu Yerusalemu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 6:4

Sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka ilikuwa imekaribia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 2:1

Siku ya Pentekoste ilipofika, waumini wote walikuwa wamekusanyika mahali pamoja.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 12:3-4

Alipoona kuwa kitendo hicho kiliwapendeza Wayahudi, aliendelea, akamkamata Petro. (Hiyo ilifanyika wakati wa sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu). Baada ya kutiwa nguvuni, Petro alifungwa gerezani, akawekwa chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari wannewanne. Herode alikusudia kumtoa hadharani baada ya sikukuu ya Pasaka.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 25:10

Mwaka wa hamsini mtauheshimu kwa kutangaza uhuru kwa watumwa wote nchini. Mwaka huo utakuwa ni sikukuu ya ukumbusho wa miaka hamsini. Kila mmoja wenu atairudia mali yake na jamaa yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 33:20

Tazameni Siyoni tunamofanya sikukuu zetu; tazameni mji Yerusalemu, makao matulivu, hema imara; vigingi vyake havitangolewa kamwe, kamba zake hazitakatwa hata moja.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 11:55

Sikukuu ya Wayahudi ya Pasaka ilikuwa karibu, na watu wengi walikwenda Yerusalemu ili wajitakase kabla ya sikukuu hiyo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 23:44

Mose akawatangazia Waisraeli sikukuu za Mwenyezi-Mungu zilizopangwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Hesabu 29:12

“Siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtafanya mkutano mtakatifu. Hamtafanya kazi siku hiyo. Mtaadhimisha sikukuu kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu kwa siku saba.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ezra 6:22

Kwa muda wa siku saba watu walisherehekea kwa furaha sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, kwa sababu Mwenyezi-Mungu aliwajalia furaha na kumpa mfalme wa Ashuru moyo wa upendo kwao, akawasaidia katika kazi za ujenzi wa nyumba ya Mungu wa Israeli.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 10:22

Huko Yerusalemu kulikuwa na sikukuu ya kutabaruku. Wakati huo ulikuwa wa baridi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Hesabu 10:10

Hali kadhalika katika siku zenu za furaha, kama vile sikukuu za mwandamo wa mwezi na sikukuu nyinginezo, mtazipiga tarumbeta hizi wakati mnapotoa sadaka zenu za kuteketezwa na tambiko za sadaka zenu za amani. Hapo mimi Mungu wenu nitawakumbukeni. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Hesabu 29:7

“Siku ya kumi ya mwezi wa saba mtafanya mkutano mtakatifu. Siku hiyo ni lazima mfunge na msifanye kazi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 35:2

Kwa siku sita mtafanya kazi zenu; lakini siku ya saba ni Sabato siku ya mapumziko ambayo ni wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Yeyote atakayefanya kazi siku hiyo lazima auawe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 20:6

Sisi, baada ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, tulipanda meli kutoka Filipi na baada ya siku tatu tukawafikia kule Troa. Huko tulikaa kwa muda wa juma moja.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wafalme 23:21

Kisha mfalme aliwaamuru watu wote, akisema, “Mfanyieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, Pasaka, kama ilivyoandikwa katika kitabu hiki cha agano.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Esta 9:22

Wayahudi waliwashinda maadui zao katika siku hizo, na katika mwezi huo huzuni yao iligeuzwa kuwa furaha, na misiba yao kuwa sikukuu. Waliagizwa wawe wakizikumbuka siku hizo kwa kufanya karamu na sherehe, kupelekeana zawadi za chakula na kuwapa maskini vitu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 23:32

Siku hiyo, itakuwa kwenu Sabato ya mapumziko rasmi na mtafunga. Siku ya Sabato ni siku ya kumi ya mwezi huo tangu jioni hadi jioni inayofuata.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 12:17

Mtaadhimisha sikukuu hii ya mikate isiyotiwa chachu kama ukumbusho wa siku nilipowatoa nyinyi, vikundi vya Israeli, kutoka Misri. Sikukuu hiyo itaadhimishwa na vizazi vyenu vyote vijavyo, kama agizo la milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 7:37

Siku ya mwisho ya sikukuu hiyo ilikuwa siku maalumu. Yesu alisimama, akasema kwa sauti kubwa, “Aliye na kiu na aje kwangu anywe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zekaria 8:19

“Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema hivi: Siku za mfungo za mwezi wa nne, mwezi wa tano, mwezi wa saba na mwezi wa kumi, zitakuwa nyakati za furaha na shangwe; zitakuwa sikukuu za sherehe kwa watu wa Yuda. Basi, pendeni ukweli na amani.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Hesabu 9:13

Lakini mtu yeyote ambaye ni safi au hayumo safarini, asipoiadhimisha sikukuu ya Pasaka, atatengwa na watu wake kwa kuwa hakunitolea sadaka kwa wakati uliopangwa. Ni lazima aadhibiwe kwa ajili ya dhambi yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Mambo ya Nyakati 35:17

Wakati huo watu wote wa Israeli waliohudhuria waliiadhimisha sikukuu hiyo ya Pasaka na sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, kwa muda wa siku saba.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 25:6

Juu ya mlima Siyoni, Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawafanyia watu wote karamu ya vinono na divai nzuri, nyama tamu na mafuta, pamoja na divai safi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 30:29

Lakini nyinyi watu wa Yerusalemu mtaimba kwa furaha kama mfanyavyo wakati wa mkesha wa sikukuu. Mtajaa furaha kama watu wanaotembea kwa mdundo wa muziki wa filimbi kwenda mlimani kwa Mwenyezi-Mungu, Mwamba wa Israeli.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Mambo ya Nyakati 30:26

Kukawa na furaha kuu mno Yerusalemu, maana tangu enzi ya mfalme Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli, jambo kama hilo lilikuwa halijatokea Yerusalemu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 122:1

Nilifurahi waliponiambia: “Twende nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 42:4

Nakumbuka tena mambo haya kwa majonzi moyoni mwangu: Jinsi nilivyokwenda na umati wa watu, nikawaongoza kwenda nyumbani kwa Mungu wakipiga vigelegele vya shukrani; umati wa watu wakifanya sherehe!

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 27:9

Muda mrefu ulikuwa umepita, na hata siku ya kufunga ilikuwa imekwisha pita. Sasa ilikuwa hatari sana kusafiri kwa meli. Basi, Paulo aliwapa onyo:

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 7:8

Nyinyi nendeni kwenye sikukuu hiyo. Mimi siendi kwenye sikukuu hiyo, maana saa yangu ifaayo haijafika.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 26:5

Lakini wakaamua jambo hilo lisifanyike wakati wa sikukuu, kusije kukatokea ghasia kati ya watu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 5:1

Baada ya hayo kulikuwa na sikukuu ya Wayahudi, naye Yesu akaenda Yerusalemu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ezekieli 46:9

Watu wanapokuja kumwabudu Mwenyezi-Mungu wakati wa sikukuu yoyote, wale walioingia kwa njia ya lango la kaskazini, watatoka kwa njia ya lango la kusini; na wale walioingia kwa lango la kusini, watatoka kwa njia ya lango la kaskazini. Mtu asirudi kwa njia ya lango aliloingilia, bali atatoka kwa njia ya lango lililo mbele yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 23:37

“Hizo ndizo sikukuu za Mwenyezi-Mungu zilizopangwa ambazo mtatoa ilani kuwe na mkutano mtakatifu wa kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka zitolewazo kwa moto, sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji, kila moja katika siku yake maalumu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 81:3

Pigeni tarumbeta kutangaza mwezi mwandamo, na pia mwezi mpevu, wakati wa sikukuu yetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Nehemia 8:18

Kila siku, tangu siku ya kwanza hadi ya mwisho, Ezra aliwasomea watu kitabu cha sheria ya Mungu. Waliadhimisha sikukuu hiyo kwa muda wa siku saba, na siku ya nane wakafanya mkutano mkubwa wa kufunga sikukuu, kama ilivyoagizwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Esta 9:27-28

Wayahudi waliifanya kuwa sheria rasmi kwao, kwa wazawa wao na kwa mtu yeyote ambaye angejiunga nao, kwamba katika wakati maalumu kila mwaka, bila kukosa, siku hizo mbili ziadhimishwe kulingana na maagizo ya Mordekai. Pia walikubaliana kwamba kila jamaa ya Kiyahudi, kizazi baada ya kizazi, katika kila mkoa na mji, sharti ikumbuke siku za Purimu na kuzisherehekea daima.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 25:11

Kwa kuwa mwaka huo, ni wa sikukuu ya ukumbusho wa miaka hamsini, msipande mbegu au kuvuna chochote kiotacho chenyewe wala kuchuma zabibu kutoka miti msiyoipogoa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Hesabu 10:2

“Tengeneza tarumbeta mbili kwa fedha iliyofuliwa. Utazitumia tarumbeta hizo wakati wa kuwaita watu na wakati wa kuvunja kambi.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wafalme 12:32

Yeroboamu pia aliamuru siku ya kumi na tano ya mwezi wa nane iwe sikukuu sawa na ile sikukuu iliyokuwa inafanyika huko Yuda. Alitoa tambiko kwenye madhabahu aliyotengeneza huko Betheli mbele ya zile sanamu za ndama alizozitengeneza, akaweka wale makuhani aliowateua wahudumu kila mahali pa kutolea tambiko alikotengeneza vilimani.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ezekieli 45:17

Itakuwa ni wajibu wa mtawala kuhakikisha kuwa sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji zinazotolewa wakati wa sikukuu, mwezi mwandamo, sabato, na sikukuu zozote zilizowekwa zinapatikana kwa Waisraeli. Mtawala mwenyewe ataandaa sadaka za kuondoa dhambi, sadaka za nafaka, sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani ili kuwafanyia upatanisho watu wote wa Israeli.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yoeli 2:15

Pigeni tarumbeta huko Siyoni! Toeni amri watu wafunge; itisheni mkutano wa kidini.

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 25:12

Mwaka huo ni wa sikukuu kwenu; utakuwa mwaka mtakatifu. Hivyo mtakula yale yanayoota yenyewe mashambani.

Sura   |  Matoleo Nakili
Marko 14:12

Siku ya kwanza ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, wakati ambapo mwanakondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wake walimwuliza, “Wataka tukuandalie wapi karamu ya Pasaka?”

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 22:7

Basi, siku ya mikate isiyotiwa chachu ikafika. Hiyo ndiyo siku ambayo mwanakondoo wa Pasaka huchinjwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 22:1

Sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, iitwayo Pasaka, ilikuwa inakaribia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 26:17

Siku ya kwanza kabla ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi walimwendea Yesu wakamwuliza, “Unataka tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?”

Sura   |  Matoleo Nakili

Maombi kwa Mungu

Ee Mungu wetu wa milele, mkuu na mwenye nguvu, Wewe pekee ndiye unayestahili utukufu na heshima yote! Siku hii ya leo, iliyo muhimu sana kwetu wengi tuliopo hapa, tunakushukuru kwa afya njema na amani unayotupa ili tuweze kufurahia pamoja na marafiki na familia zetu. Bariki wote watakaoshiriki katika mkutano huu, tujifunze kusikilizana, kuelewana, kuzungumza na kuheshimiana maoni, ili shughuli hii iwe pia kwa utukufu wako na Roho wako Mtakatifu ajidhihirishe mioyoni mwetu, nasi tupokee kutoka mkononi mwako kile unachotutaka. Neno lako linasema: "Tazama, mimi nakuamuru uwe hodari na mshujaa; usiogope wala usikate tamaa; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako." Tutumie, Ee Bwana, neema na nguvu zako ili upendo wako uongoze hatua zetu zote; tuweze kuweka uwezo wetu katika utumishi wako. Njoo, Bwana, uchukue udhibiti wa maisha yetu na uwezo wetu. Bariki na urejeshe nguvu za wale walioshiriki katika kuandaa mkutano huu, linda mioyo yao na uwape fanaka. Kwa jina la Yesu. Amina.
Tufuate:

Matangazo


Matangazo