Biblia Todo Logo
Mistari ya Biblia
- Matangazo -


MISTARI KUHUSU YESU

MISTARI KUHUSU YESU

Rafiki yangu, Yesu ndiye mwokozi wako. Alijitoa mhanga msalabani kwa ajili ya upendo wake kwako. Yeye ni mwana mpendwa wa Mungu, na kupitia kwake, tunaokolewa na kupata uzima wa milele. Yesu ni Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana. Aliteseka kwa ajili ya dhambi zako.

Anataka ukaribie kwake kila siku, umjue, na uzungumze naye. Anataka kuwa rafiki yako wa karibu. Upendo wake kwako ni mkuu sana kiasi cha kujitoa mhanga ili kukuokoa. Kama Biblia inavyosema katika Luka 19:10, "Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea."

Ni kupitia Yesu pekee tunaweza kupata wokovu na uzima wa milele, na kuwa huru kutoka katika utumwa wa ulimwengu huu wa kupita. Matendo 4:12 yanatukumbusha, "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."


Yoeli 2:31

Jua litatiwa giza, na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, kabla ya kufika siku ya Mwenyezi-Mungu, siku iliyo kuu na ya kutisha.

Sura   |  Matoleo Nakili
Amosi 5:18

Ole wenu nyinyi mnaoingojea kwa hamu siku ya Mwenyezi-Mungu! Kwa nini mnaitaka sana siku hiyo? Siku hiyo, itakuwa siku ya giza na sio ya mwanga!

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 13:6

Lieni maana siku ya Mwenyezi-Mungu imekaribia; inakuja kama maafa kutoka kwa Mungu Mwenye Nguvu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zekaria 14:1

Tazama, siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu inakuja. Siku hiyo, enyi watu wa Yerusalemu, mali yenu itagawanywa mbele ya macho yenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Malaki 4:5

“Tazama, kabla ya kufika siku ile kuu na ya kutisha, nitamtuma nabii Elia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Sefania 1:14-15

Ile siku kubwa ya Mwenyezi-Mungu imekaribia, iko karibu na inakuja mbio. Mlio wa siku ya Mwenyezi-Mungu ni wa uchungu; hapo, shujaa atalia kwa sauti. Siku hiyo itakuwa siku ya ghadhabu, ni siku ya dhiki na uchungu, siku ya giza na huzuni; siku ya uharibifu na maangamizi, siku ya mawingu na giza nene.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ezekieli 30:3

Kwa maana, siku hiyo imekaribia; siku ile ya Mwenyezi-Mungu iko karibu. Hiyo itakuwa siku ya mawingu, siku ya maangamizi kwa mataifa.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Petro 3:10

Siku ya Bwana itakuja kama mwizi. Siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu; vitu vyake vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia itatoweka pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 1:10

Basi, wakati mmoja, siku ya Bwana, nilikumbwa na Roho, nikasikia nyuma yangu sauti kubwa kama sauti ya tarumbeta.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 5:2

Maana nyinyi wenyewe mwajua kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 2:20

jua litatiwa giza, na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, kabla ya kutokea ile siku kuu na tukufu ya Bwana.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 1:8

Yeye atawaimarisheni nyinyi mpaka mwisho mpate kuonekana bila hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 2:12

Naam, yaja siku ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi dhidi ya wenye kiburi na majivuno, dhidi ya wote wanaojikweza;

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 4:16-17

Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai wakati huo tutakusanywa pamoja nao katika mawingu kumlaki Bwana hewani. Na hivyo tutakuwa daima pamoja na Bwana.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 6:17

Maana siku maalumu ya ghadhabu yao imefika. Nani awezaye kuikabili?”

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 34:8

Maana Mwenyezi-Mungu anayo siku ya kisasi; mwaka wa kulipiza maadui wa Siyoni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 24:42

Basi, kesheni, kwa maana hamjui siku atakayokuja Bwana wenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yoeli 2:11

Mwenyezi-Mungu anaamuru jeshi lake kwa sauti; askari wake ni wengi mno, wanaomtii hawahesabiki. 2Siku ya Mwenyezi-Mungu kweli ni kuu na ya kutisha sana! Nani atakayeweza kuistahimili?

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 13:9

Siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja, siku kali, ya ghadhabu na hasira kali. Itaifanya nchi kuwa uharibifu, itawaangamiza wenye dhambi wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 19:15

Upanga mkali hutoka kinywani mwake, na kwa upanga huo atawashinda watu wa mataifa. Yeye ndiye atakayetawala kwa fimbo ya chuma na kuikamua divai katika chombo cha kukamulia zabibu za ghadhabu kuu ya Mungu Mwenye Nguvu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 1:14

maana mpaka sasa mmenielewa kiasi fulani tu. Tunajua kwamba katika ile siku ya Bwana Yesu mtaweza kutuonea sisi fahari kama nasi tunavyowaonea nyinyi fahari.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 66:15-16

Mwenyezi-Mungu atakuja kama moto, na magari yake ya vita ni kimbunga. Ataiacha hasira yake ifanye kazi yake kwa ukali, na onyo lake litekelezwe kwa miali ya moto. Mwenyezi-Mungu atatoa hukumu kwa moto, atawaadhibu watu wote kwa upanga; nao atakaowaangamiza watakuwa wengi.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 4:7

Mwisho wa vitu vyote umekaribia. Kwa hiyo mnapaswa kuwa na utaratibu na kukesha ili muweze kusali.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zekaria 12:10

Wazawa wa Daudi na wakazi wa mji wa Yerusalemu nitawajaza roho ya huruma na maombi, nao watamtazama yeye waliyemtoboa; watamlilia kama mtu amliliavyo mtoto wake wa pekee, au kama mtu amliliavyo kwa uchungu mzaliwa wake wa kwanza.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 25:13

Kisha Yesu akasema, “Kesheni basi, kwa maana hamjui siku wala saa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 2:16

Hivyo, kufuatana na hii Habari Njema ninayohubiri, ndivyo itakavyokuwa wakati Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya binadamu kwa njia ya Yesu Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Sefania 2:3

Mtafuteni Mwenyezi-Mungu enyi wanyenyekevu wote nchini, enyi mnaozitii amri zake. Tafuteni uadilifu, tafuteni unyenyekevu; labda mtaiepa siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 17:31

Kwa maana amekwisha weka siku ambayo atauhukumu ulimwengu kwa haki kwa njia ya mtu mmoja aliyemteua. Mungu amewathibitishia wote jambo hili kwa kumfufua mtu huyo kutoka kwa wafu!”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 10:25

Tusiache ile desturi ya kukutana pamoja, kama vile wengine wanavyofanya. Bali tunapaswa kusaidiana kwani, kama mwonavyo, siku ile ya Bwana inakaribia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 16:14

Hawa ndio roho za pepo wafanyao miujiza. Ndio wanaokwenda kwa wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya pamoja kwa ajili ya vita ya ile siku kubwa ya Mungu Mwenye Nguvu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 118:24

Hii ndiyo siku aliyoifanya Mwenyezi-Mungu; tushangilie na kufurahi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 24:30

Kisha, ishara ya Mwana wa Mtu itaonekana angani, na hapo makabila yote duniani yatalalamika; watamwona Mwana wa Mtu akija juu ya mawingu ya angani mwenye nguvu na utukufu mwingi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yoeli 2:1

Pigeni tarumbeta huko Siyoni; pigeni baragumu juu ya mlima mtakatifu! Tetemekeni enyi wakazi wa Yuda, maana siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja, naam, siku hiyo iko karibu!

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 13:11

Zaidi ya hayo, nyinyi mnajua tumo katika wakati gani: Sasa ndio wakati wa kuamka usingizini; naam, wokovu wetu uko karibu zaidi sasa kuliko wakati ule tulipoanza kuamini.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 24:21-22

Siku ile Mwenyezi-Mungu ataliadhibu jeshi la angani kadhalika na wafalme wa duniani. Wote watakusanywa kama wafungwa shimoni; watafungwa gerezani pamoja kwa miaka mingi, na baada ya muda huo atawaadhibu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 3:19-21

Basi, tubuni, mkamrudie Mungu ili yeye afute dhambi zenu. Wakati huo watu walikuwa wanambeba mtu mmoja kiwete tangu kuzaliwa. Watu hao walikuwa wakimweka huyo mtu kila siku kwenye mlango wa hekalu uitwao “Mlango Mzuri,” ili aombe chochote kwa wale waliokuwa wakiingia hekaluni. Fanyeni hivyo ili Bwana awape nyakati za kuburudika rohoni na kuwaletea yule Kristo aliyemteua ambaye ndiye Yesu. Ni lazima yeye abaki huko mbinguni mpaka utakapofika wakati wa kurekebishwa vitu vyote, kama Mungu alivyosema kwa njia ya manabii wake watakatifu wa tangu zamani.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wathesalonike 2:2-3

msifadhaike upesi moyoni, na wala msitiwe wasiwasi kwa sababu ya madai kwamba siku ya Bwana imekwisha fika. Labda inadhaniwa kwamba jambo hili limetokana na uaguzi fulani, mahubiri au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu. Msikubali kudanganywa na mtu yeyote kwa namna yoyote ile. Maana siku hiyo haitakuja mpaka kwanza ule uasi utokee na yule Mwovu aonekane, ambaye mwisho wake ni kuangamizwa kabisa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 7:21-23

“Si kila aniambiaye, ‘Bwana, Bwana’, ataingia katika ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza matakwa ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile ya hukumu: ‘Bwana, Bwana! Kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi’. Hapo nitawaambia: ‘Sikuwajua nyinyi kamwe; ondokeni mbele yangu, enyi watenda maovu.’

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 21:36

Muwe waangalifu basi, na salini daima ili muweze kupata nguvu ya kupita salama katika mambo haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele ya Mwana wa Mtu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Amosi 5:20

Siku ya Mwenyezi-Mungu itakuwa giza, na sio mwanga; itakuwa huzuni bila uangavu wowote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 13:13

Nitazitetemesha mbingu nayo nchi itatikisika katika misingi yake kwa sababu ya ghadhabu yangu Mwenyezi-Mungu siku ile ya hasira yangu kali.

Sura   |  Matoleo Nakili
Sefania 1:7

Nyamazeni mbele ya Bwana Mwenyezi-Mungu, kwani siku ya Mwenyezi-Mungu iko karibu. Mwenyezi-Mungu ameandaa tambiko, nao aliowaalika amewateua.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 46:10

Siku hiyo ni siku ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ni siku ya kulipiza kisasi; naam, siku ya kuwaadhibu maadui zake. Upanga utawamaliza hao na kutosheka, utainywa damu yao na kushiba. Maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi anayo kafara huko kaskazini karibu na mto Eufrate.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 2:19-21

Ingieni katika mapango miambani, katika mashimo ardhini, kuiepa hasira ya Mwenyezi-Mungu, mbali na utukufu wa enzi yake, atakapokuja kuitia hofu dunia. Siku zijazo mlima wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu utaimarishwa kupita milima yote, utainuliwa juu ya vilima vyote. Mataifa yote yatamiminika huko, Siku hiyo, watu watawatupia panya na popo vinyago vyao vya fedha na dhahabu walivyojitengenezea ili kuviabudu. Nao wataingia katika mapango miambani na kwenye nyufa za miamba, kuiepa hasira ya Mwenyezi-Mungu, mbali na utukufu wa enzi yake, atakapokuja kuitia hofu dunia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 4:7

Mungu aliweka siku nyingine ambayo inaitwa “Leo,” akasema baadaye kwa njia ya Daudi maneno yaliyokwisha tajwa: “Kama mkisikia sauti ya Mungu leo, msiwe wakaidi.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Sefania 3:8

“Kwa hiyo ningojeni mimi Mwenyezi-Mungu, ngoja siku nitakapoinuka kutoa mashtaka. Nimeamua kuyakusanya mataifa na falme, kuyamwagia ghadhabu yangu, kadhalika na ukali wa hasira yangu. Dunia yote itateketezwa kwa moto wa ghadhabu yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Petro 3:12-13

mkiingojea siku ile ya Mungu na kuifanya ije upesi – siku ambayo mbingu zitateketezwa kwa moto na kuharibiwa, na vitu vyake vya asili vitayeyushwa kwa joto. Lakini sisi, kufuatana na ahadi yake, twangojea mbingu mpya na dunia mpya ambayo imejaa uadilifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 20:12

Kisha nikawaona watu wakubwa na wadogo, wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa. Halafu kitabu kingine, yaani kitabu cha uhai, kikafunguliwa pia. Wafu wakahukumiwa kadiri ya matendo yao, kama ilivyoandikwa ndani ya vitabu hivyo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 96:13

mbele ya Mwenyezi-Mungu anayekuja; naam, anayekuja kuihukumu dunia. Ataihukumu dunia kwa haki, na mataifa kwa uaminifu wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 60:2

Tazama, giza litaifunika dunia, giza nene litayafunika mataifa; lakini wewe, Mwenyezi-Mungu atakuangazia, utukufu wake utaonekana kwako.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 2:28

Naam, watoto, kaeni ndani yake kusudi wakati atakapotokea tuwe hodari bila kuwa na sababu ya kujificha kwa aibu siku ya kuja kwake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 30:7

Kweli, siku hiyo ni kubwa, hakuna nyingine kama hiyo; ni siku ya huzuni kwa watu wa Yakobo; hata hivyo, wataokolewa humo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:18-19

Naona kuwa mateso ya wakati huu wa sasa si kitu kamwe kama tukiyalinganisha na ule utukufu utakaodhihirishwa kwetu. Viumbe vyote vinangojea kwa hamu Mungu awadhihirishe watoto wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 1:11

wakasema, “Enyi wananchi wa Galilaya! Mbona mnasimama mkitazama angani? Yesu huyu ambaye amechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni atakuja tena namna hiyohiyo mlivyomwona akienda mbinguni.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 17:24

Kwa maana kama vile umeme unavyotokea ghafla na kuangaza anga upande mmoja hadi mwingine, ndivyo Mwana wa Mtu atakavyokuwa siku ile yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yoeli 3:14

Wanafika makundi kwa makundi kwenye bonde la Hukumu, maana siku ya Mwenyezi-Mungu imekaribia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zekaria 14:6-7

Wakati huo hakutakuwa baridi wala baridi kali. Mchana utaendelea bila giza kuingia. Wakati huo wajulikana kwa Mwenyezi-Mungu peke yake. Hakutakuwa mchana wala usiku, kwa maana hata saa za jioni mwanga utaendelea kuwapo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 11:10-12

Siku ile chipukizi wa Yese atakuwa ishara kwa mataifa; mataifa yatamtafuta na makazi yake yatatukuka. Siku hiyo, Bwana ataunyosha mkono wake tena kuwarejesha watu wake waliosalia huko Ashuru, Misri, Pathrosi, Kushi, Elamu, Shinari, Hamathi na sehemu za pwani. Naye atatweka bendera kuwaashiria mataifa, kuwakusanya Waisraeli waliodharauliwa, kuwaleta pamoja watu wa Yuda waliotawanywa, na kuwarudisha toka pembe nne za dunia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 21:4

Yeye atayafuta machozi yao yote; maana kifo hakitakuwako tena, wala uchungu, wala kilio, wala maumivu; maana ile hali ya kale imepita!”

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 5:4-6

Lakini nyinyi, ndugu, hamko gizani, na siku hiyo haipaswi kuwajieni ghafla kama vile mwizi. Nyinyi nyote ni watu mnaoishi katika mwanga, watu wa mchana. Sisi si watu wa usiku, wala wa giza. Basi, tusilale usingizi kama wengine; tunapaswa kukesha na kuwa na kiasi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 24:3-5

Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni, wanafunzi walimwendea faraghani, wakamwuliza, “Tuambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonesha kuja kwako na mwisho wa nyakati?” Kisha, ishara ya Mwana wa Mtu itaonekana angani, na hapo makabila yote duniani yatalalamika; watamwona Mwana wa Mtu akija juu ya mawingu ya angani mwenye nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika wake wenye tarumbeta la kuvuma sana, nao watawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, toka mwisho huu wa mbingu hadi mwisho huu. “Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa mavuno umekaribia. Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo haya yote yakitendeka, jueni kwamba yuko karibu sana. Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo yote kutukia. Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe. “Lakini, juu ya siku au saa hiyo, hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye. Kwa maana kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu. Maana nyakati hizo, kabla ya gharika kuu, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka Noa alipoingia ndani ya ile safina. Hawakujua kuna nini mpaka ile gharika ilipotokea, ikawakumba wote. Ndivyo itakavyokuwa wakati Mwana wa Mtu atakapokuja. Yesu akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa na mtu. Wakati huo watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa. Kina mama wawili watakuwa wanasaga nafaka, mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa. Basi, kesheni, kwa maana hamjui siku atakayokuja Bwana wenu. Lakini kumbukeni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua siku mwizi atakapofika, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe. Kwa hiyo, nanyi pia muwe tayari, kwa maana Mwana wa Mtu atakuja saa msiyoitazamia.” Yesu akaendelea kusema, “Ni nani basi mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watu wake, awape chakula kwa wakati wake? Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakapokuja atamkuta akifanya hivyo. Kweli nawaambieni, atamweka mtumishi huyo aisimamie mali yake yote. Lakini kama mtumishi mbaya akijisemea moyoni: ‘Bwana wangu amekawia kurudi,’ kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, akaanza kula na kunywa pamoja na walevi, Maana wengi watatokea wakisema kila mmoja kwamba yeye ndiye Kristo nao watawapotosha watu wengi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yuda 1:14-15

Naye Henoki, ambaye ni babu wa saba tangu Adamu, alibashiri hivi juu ya watu hao: “Sikilizeni! Bwana anakuja pamoja na maelfu ya malaika wake watakatifu kuwahukumu watu wote, na kuwaadhibu wote wasiomcha Mungu kwa ajili ya matendo yao yote maovu waliyotenda bila kumjali Mungu, na kwa ajili ya maneno yote mabaya ambayo watu waovu walimkashifu nayo.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 3:3

Kumbuka, basi, yale uliyofundishwa na jinsi ulivyoyasikia, uyatii na kutubu. Usipokesha nitakujia ghafla kama mwizi, na wala hutaijua saa nitakapokujia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 50:3

Mungu wetu anakuja, na sio kimyakimya: Moto uunguzao wamtangulia, na dhoruba kali yamzunguka.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mika 4:1-2

Utakuja wakati ambapo mlima wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu utakuwa mkubwa kuliko milima yote. Naam, utakwezwa juu ya vilima vyote. Watu wengi watamiminika huko, Enyi watu wa Siyoni, lieni na kugaagaa kama mama anayejifungua! Maana sasa mtaondoka katika mji huu mwende kukaa nyikani, mtakwenda mpaka Babuloni. Lakini huko, mtaokolewa. Huko Mwenyezi-Mungu atawakomboa makuchani mwa adui zenu. Mataifa mengi yamekusanyika kuwashambulia. Yanasema: “Acheni mji wao utiwe najisi, nasi tuyaone magofu ya Siyoni!” Lakini wao hawafahamu mawazo ya Mwenyezi-Mungu wala hawaelewi mpango wake: Kwamba amewakusanya pamoja, kama miganda mahali pa kupuria. Mwenyezi-Mungu asema, “Enyi watu wa Siyoni, inukeni mkawaadhibu adui zenu! Nitawapeni nguvu kama fahali mwenye pembe za chuma na kwato za shaba. Mtawasaga watu wa mataifa mengi; mapato yao mtaniwekea wakfu mimi, mali zao mtanitolea mimi Bwana wa dunia yote.” mataifa mengi yataujia na kusema: “Twendeni juu kwenye mlima wa Mwenyezi-Mungu, twende katika nyumba ya Mungu wa Yakobo, ili atufundishe njia zake, nasi tufuate nyayo zake. Maana mwongozo utatoka huko Siyoni; neno la Mwenyezi-Mungu huko Yerusalemu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 14:10-12

Kwa nini basi, wewe wamhukumu ndugu yako? Nawe, kwa nini wamdharau ndugu yako? Sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. Maana Maandiko yanasema: “Kama niishivyo, asema Bwana, kila mtu atanipigia magoti, na kila mmoja atakiri kwamba mimi ni Mungu.” Kwa hiyo, kila mmoja wetu atatoa hoja juu yake mwenyewe mbele ya Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 15:52-53

wakati wa mbiu ya mwisho, kwa nukta moja, kufumba na kufumbua. Maana tarumbeta ya mwisho itakapolia, wafu watafufuliwa katika hali ya kutoweza kufa tena, na sisi tutageuzwa. Maana ni lazima kila kiharibikacho kijivalie hali ya kutoharibika, mwili uwezao kufa ujivalie hali ya kutokufa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zekaria 9:14

Mwenyezi-Mungu atawatokea watu wake; atafyatua mishale yake kama umeme. Bwana Mwenyezi-Mungu atapiga tarumbeta; atafika pamoja na kimbunga cha kusini.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 4:2-6

Siku ile, tawi atakalochipusha Mwenyezi-Mungu litakuwa zuri na tukufu, nayo matunda ya nchi yatakuwa ya fahari na utukufu kwa wale Waisraeli watakaosalia. Waisraeli watakaobaki watayaonea fahari na kujivunia mazao ya nchi yao. Wale watakaosalia hai mjini Yerusalemu, naam, wale watakaobaki huko Siyoni, wataitwa “Wateule wa Mungu;” hao ndio wale wote watakaokuwa wameandikwa kitabuni mwake waishi huko Yerusalemu. Kwa roho yake, Bwana atawaweka sawa na kuwatakasa. Na atakapokwisha kuwatakasa wanawake wa Siyoni uchafu wao na kufuta madoa ya damu yaliyomo humo Yerusalemu, hapo atafanya kila mahali juu ya mlima Siyoni na juu ya mikutano ya watu kuwe na wingu wakati wa mchana, na moshi na moto uwakao vizuri wakati wa usiku. Zaidi ya hayo utukufu wa Mungu utaufunika na kuulinda mji wote. Utukufu wake utakuwa kwao kivuli kuwakinga na joto la mchana; na kimbilio na kinga yao wakati wa dhoruba na mvua.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 5:5

mkabidhini mtu huyo kwa Shetani ili mwili wake uharibiwe na roho yake iweze kuokolewa siku ile ya Bwana.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 22:12

“Sikiliza!” Asema Yesu, “Naja upesi pamoja na tuzo nitakalompa kila mmoja kufuatana na matendo yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 1:10

na sasa mwamngojea Mwanae ashuke kutoka mbinguni, yaani Yesu, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu na ambaye anatuokoa katika ghadhabu ya Mungu inayokuja.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 25:8-9

Bwana Mungu atakiangamiza kifo milele! Atayafuta machozi katika nyuso za watu wote na kuwaondolea watu wake aibu duniani kote. Bwana Mwenyezi-Mungu ametamka. Siku ile, watu wote watasema, “Huyu ndiye Mungu wetu! Tumemngojea atuokoe. Huyu ndiye Mwenyezi-Mungu tuliyemtazamia. Njoni tufurahi na kushangilia kwa kuwa ametuokoa.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 12:40

Nanyi, kadhalika muwe tayari, maana Mwana wa Mtu atakuja saa msiyoitazamia.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 14:7

Naye akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumtukuza! Maana saa imefika ya kutoa hukumu yake. Mwabuduni yeye aliyeumba mbingu na dunia, bahari na chemchemi za maji.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Yoeli 2:13

Msirarue mavazi yenu kuonesha huzuni bali nirudieni kwa moyo wa toba.” Mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; yeye amejaa neema na huruma; hakasiriki upesi, ni mwingi wa fadhili; daima yu tayari kuacha kuadhibu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Timotheo 4:1

Nakuamuru mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu atakayewahukumu watu walio hai na wafu, na kwa sababu anakuja kutawala akiwa Mfalme:

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 1:5-7

Hizo zitakuwa zenu nyinyi ambao kwa imani mnalindwa salama kwa nguvu ya Mungu kwa ajili ya wokovu ambao uko tayari kufunuliwa mwishoni mwa nyakati. Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka, majaribio ambayo shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe, ambayo huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu, ambayo ni ya thamani kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate kuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Danieli 12:1-2

“ ‘Wakati huo, Mikaeli, malaika mkuu, aliye mlinzi wa watu wako, atatokea. Ndipo kutakuwa na wakati wa taabu sana kuliko nyakati nyingine zote tangu mataifa yalipoanza kuwako duniani. Lakini, wakati huo, kila mmoja wa watu wako ambaye jina lake limeandikwa katika kitabu cha uhai, ataokolewa. Watu wengi wataondolewa uchafu, watatakaswa na kusafishwa. Lakini watu waovu wataendelea kutenda uovu. Hakuna hata mmoja wa hao waovu atakayeelewa; wenye hekima ndio watakaoelewa. “ ‘Tangu wakati wa kukomeshwa kwa sadaka za kuteketezwa kila siku, yaani kutoka wakati ule chukizo haribifu litakaposimamishwa itakuwa muda wa siku 1,290. Heri yao watakaostahimili mpaka siku zile 1,335 zitakapotimia. “ ‘Lakini wewe, ee Danieli, jiendee, ukapumzike kaburini, na wakati huo utakapotimia, utafufuka na kupata tuzo lako.’” Wengi wa wale ambao wamekwisha kufa, watafufuka; wengine watapata uhai wa milele, na wengine watapata uhai na kudharauliwa milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 35:10

Waliokombolewa na Mwenyezi-Mungu watarudi, watakuja Siyoni wakipiga vigelegele. Watakuwa wenye furaha ya milele, watajaliwa furaha na shangwe; huzuni na kilio vitatoweka kabisa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 22:20

Naye anayetoa ushahidi wake juu ya mambo haya asema: “Kweli naja upesi.” Amina. Njoo Bwana Yesu!

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 65:17

“Sasa, naumba mbingu mpya na dunia mpya. mambo ya zamani hayatakumbukwa tena.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 19:28

Yesu akawaambia, “Nawaambieni kweli, Mwana wa Mtu atakapoketi katika kiti chake cha enzi kitukufu katika ulimwengu mpya, nyinyi mlionifuata mtaketi katika viti kumi na viwili mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:13

Lakini Mwenyezi-Mungu humcheka mwovu, kwani ajua mwisho wake u karibu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 21:25-28

“Kutakuwa na ishara katika jua na mwezi na nyota. Mataifa duniani yatakuwa na dhiki kwa sababu ya wasiwasi kutokana na mshindo wa mawimbi ya bahari. Watu watazirai kwa sababu ya woga, wakitazamia mambo yatakayoupata ulimwengu; kwa maana nguvu za mbingu zitatikiswa. Halafu, watamwona Mwana wa Mtu akija katika wingu, mwenye nguvu na utukufu mwingi. Wakati mambo hayo yatakapoanza kutukia, simameni na kuinua vichwa vyenu juu, kwa maana ukombozi wenu umekaribia.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 9:28

vivyo hivyo Kristo naye alijitoa tambiko mara moja tu kwa ajili ya kuziondoa dhambi za wengi. Atakapotokea mara ya pili, si kwa ajili ya kupambana na dhambi, bali ni kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaomngojea.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 2:4

Mungu atasuluhisha mizozo ya mataifa atakata mashauri ya watu wengi. Watu watafua panga za vita kuwa majembe na mikuki yao kuwa miundu ya kupogolea. Taifa halitapigana na taifa lingine wala hayatafanya tena mazoezi ya vita.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 5:10

Umewafanya ufalme wa makuhani wamtumikie Mungu wetu, nao watatawala duniani.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Malaki 3:2

Lakini ni nani atakayestahimili siku hiyo atakapokuja? Ni nani atakayesimama kustahimili atakapotokea? Yeye ni kama moto mkali usafishao chuma; ni kama sabuni ya dobi.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wathesalonike 1:10

wakati atakapokuja siku ile kupokea utukufu kutoka kwa watu wake na heshima kutoka kwa wote wanaoamini. Nyinyi pia mtakuwa miongoni mwao, kwani mmeuamini ule ujumbe tuliowaletea.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:23

Wala si hivyo viumbe peke yake, bali hata sisi tulio na huyo Roho, aliye wa kwanza wa zawadi za Mungu; sisi pia tunalalamika ndani yetu, tukingojea tufanywe watoto wa Mungu, nazo nafsi zenu zikombolewe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 33:22

Maana Mwenyezi-Mungu ni hakimu wetu, yeye ni mtawala wetu; Mwenyezi-Mungu ni mfalme wetu, yeye ndiye anayetuokoa.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 4:17

Upendo umekamilika ndani yetu kusudi tuweze kuwa na ujasiri siku ile ya hukumu; kwani maisha yetu hapa duniani ni kama yale ya Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 3:13

Iwe iwavyo, ubora wa kazi ya kila mmoja utaonekana wakati siku ile ya Kristo itakapoifichua. Maana, siku hiyo itatokea na moto, na huo moto utaipima na kuonesha ubora wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 11:4-5

Atawapatia haki watu maskini, atawaamulia sawasawa wanyonge nchini. Kwa neno lake ataiadhibu dunia, kwa tamko lake atawaua waovu. Haki itakuwa kama mkanda wa kujifunga, uaminifu utakaa naye kama mkanda kiunoni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 19:11-16

Kisha, nikaona mbingu zimefunguliwa; na huko alikuwako farasi mmoja mweupe, na mpandafarasi wake aliitwa “Mwaminifu” na “Kweli”. Huyo huhukumu na kupigana kwa ajili ya haki. Macho yake ni kama mwali wa moto, na alikuwa amevaa taji nyingi kichwani. Alikuwa ameandikwa jina ambalo hakuna mtu alijuaye isipokuwa tu yeye mwenyewe. Alikuwa amevaa vazi lililokuwa limelowekwa katika damu. Na jina lake huyo ni “Neno la Mungu”. Majeshi ya mbinguni yalimfuata yakiwa yamepanda farasi weupe na yamevaa mavazi ya kitani, meupe na safi. Upanga mkali hutoka kinywani mwake, na kwa upanga huo atawashinda watu wa mataifa. Yeye ndiye atakayetawala kwa fimbo ya chuma na kuikamua divai katika chombo cha kukamulia zabibu za ghadhabu kuu ya Mungu Mwenye Nguvu. Juu ya vazi lake, na juu ya paja lake, alikuwa ameandikwa jina: “Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 24:15

Mimi namtumainia Mungu, na wao wanalo tumaini hilo, kwamba watu, wema na wabaya, watafufuka.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mika 7:15-16

Kama wakati ulipotutoa nchini Misri, utuoneshe tena maajabu yako. Nao watu wa mataifa watakapoona hayo, watajaa fedheha hata kama wana nguvu. Watashikwa na bumbuazi na kukosa cha kusema na kuwa kama viziwi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 11:18

Watu wa mataifa waliwaka hasira, lakini ghadhabu yako imefika, naam wakati wa kuwahukumu wafu. Ndio wakati wa kuwatuza watumishi wako manabii, watakatifu na wote wanaolitukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo. Ni wakati wa kuwaangamiza waangamizi wa dunia.”

Sura   |  Matoleo Nakili

Maombi kwa Mungu

Ee Mungu Mkombozi! Leo nakulilia na kutafuta uso wako ili nikupatie utukufu na heshima, nakupa utukufu wote na heshima kwa ajili ya sadaka yako kwani ulinikomboa kwa damu yako iliyomwagika msalabani Kalvari. Asante kwa agano jipya, ambalo kwaye ninao ufikiaji mbele ya kiti cha enzi cha neema. Ulituokoa kutoka katika nguvu za giza, Yesu wewe ni Mwana wa Mungu, mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu, asante kwa kujitoa kwa ajili ya upendo kwa wanadamu ukilipia gharama kubwa kwa ajili ya dhambi zetu. Neno lako linasema: "ambaye ndani yake tunao ukombozi katika damu yake, yaani, msamaha wa dhambi, sawasawa na utajiri wa neema yake". Asante, kwa sababu ulipigwa kwa ajili ya uasi wangu na kusagwa kwa ajili ya dhambi zangu na adhabu ya amani yangu ilikuwa juu yako. Kwako utukufu wote na heshima. Kwa jina la Yesu. Amina!
Tufuate:

Matangazo


Matangazo