Biblia Todo Logo
Mistari ya Biblia
- Matangazo -


62 Mistari Nzuri Zaidi ya Biblia

62 Mistari Nzuri Zaidi ya Biblia

Rafiki yangu, Yohana 3:16 ni mstari unaojulikana sana. Unasema, "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." Unaona upendo wa Mungu hapo? Uzima wa milele unatupatia sisi tukimwamini.

Na pia, Wafilipi 4:13 inasema, "Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu." Mstari huu umewatia moyo watu wengi sana kwa miaka mingi. Unanipa mimi nguvu pia.

Katika Biblia, kuna mistari mingi inayoonyesha moyo wa Mungu. Inatufundisha jinsi ya kuishi maisha yetu, inatupa moyo, na tunaweza kuitumia tunapoomba. Thamani yake hailinganishwi na kitu kingine chochote.

Mungu hutusahihisha kupitia Biblia. Lakini kama tunataka kuwa Wakristo imara, wanaokua na kumtukuza Mungu, tunapaswa kujilisha Neno lake kila siku. Tukariri na tumwombe Mungu atusaidie kuishi kulingana nalo. Sawa kabisa?


Waroma 6:23

Kwa maana mshahara wa dhambi ni kifo; lakini zawadi anayotoa Mungu ni uhai wa milele katika kuungana na Kristo Yesu, Bwana wetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 4:19

Basi, Mungu wangu, kwa utajiri wake mkuu kwa njia ya Kristo, atawapeni mahitaji yenu yote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 23:1

Mwenyezi-Mungu ni mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 3:16

Maana Mungu aliupenda ulimwengu hivi hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uhai wa milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 53:4

Hata hivyo alivumilia majonzi yetu, na kubeba huzuni zetu. Sisi tulifikiri amepata adhabu, amepigwa na Mungu na kuteswa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 23:1-2

Mwenyezi-Mungu ni mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. Hunipumzisha kwenye malisho mabichi; huniongoza kando ya maji matulivu,

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 23:4

Nijapopita katika bonde la giza kuu la kifo, sitaogopa hatari yoyote, maana wewe ee Mwenyezi-Mungu u pamoja nami; gongo lako na fimbo yako vyanilinda.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 13:34

Nawapeni amri mpya: Pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 1:12

Lakini wale waliompokea, wale waliomwamini, aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu,

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 54:17

Silaha zote zilizoundwa kukudhuru wewe hazitafaa chochote kile. Mtu akikushtaki mahakamani, utamshinda. Hilo ndilo fungu nililowapangia watumishi wangu. Hizo ndizo haki nilizowathibitishia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 6:20

Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 29:11

Maana, mimi Mwenyezi-Mungu ninajua mambo niliyowapangia. Nimewapangieni mema na si mabaya, ili mpate kuwa na tumaini la baadaye.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 6:33

Bali, shughulikeni kwanza juu ya ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo yote mtapewa kwa ziada.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 7:6

Lakini sasa tumekuwa huru kutoka vifungo vya sheria, kwa sababu tumekufa kuhusu lile jambo lililotufanya sisi watumwa. Sasa tunatumikia kufuatana na maisha mapya ya Roho, na si kufuatana na hali ile ya kale ya sheria iliyoandikwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 12:2

Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu na kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 5:8

Lakini Mungu amethibitisha kwamba anatupenda, maana wakati tulipokuwa bado wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 104:24

Ee Mwenyezi-Mungu, umetenda mambo mengi mno! Yote umeyafanya kwa hekima! Dunia imejaa viumbe vyako!

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:44

Lakini mimi nawaambieni, wapendeni maadui zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu nyinyi,

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 40:31

Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu, watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mabawa kama tai; watakimbia bila kuchoka; watatembea bila kulegea.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:28

Tunajua kwamba, katika mambo yote, Mungu hufanya kazi na kuifanikisha pamoja na wote wampendao, yaani wale aliowaita kadiri ya kusudi lake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 46:10

Asema: “Nyamazeni na kujua kuwa mimi ni Mungu! Mimi natukuka katika mataifa yote; mimi natukuzwa ulimwenguni kote!”

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 41:10

Basi, usiogope, mimi nipo pamoja nawe. Usifadhaike, mimi ni Mungu wako. Nitakuimarisha na kukusaidia; nitakulinda kwa mkono wangu wa ushindi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 4:13

Naweza kuikabili kila hali kwani Kristo hunipa nguvu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 4:4

Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu.’”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 27:1

Mwenyezi-Mungu ni mwanga wangu na wokovu wangu, ni nani nitakayemwogopa? Mwenyezi-Mungu ni ngome ya maisha yangu, sitamwogopa mtu yeyote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 11:28

Njoni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 34:8

Jaribuni mwone Mwenyezi-Mungu alivyo mwema. Heri mtu anayekimbilia usalama kwake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 11:28-30

Njoni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifungeni nira yangu, mkajifunze kwangu, maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtatulizwa rohoni mwenu. wamwulize: “Je, wewe ni yule anayekuja, au tumngoje mwingine?” Maana, nira niwapayo mimi ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 3:5-6

Mtumaini Mwenyezi-Mungu kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe. Umtambue Mungu katika kila ufanyalo, naye atazinyosha njia zako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 4:6-7

Msiwe na wasiwasi juu ya kitu chochote, ila kwa kila hali, mwombeni Mungu katika sala juu ya mahitaji yenu, kwa shukrani. Nayo amani ya Mungu ipitayo akili zote za watu italinda salama mioyo na akili zenu katika kuungana na Kristo Yesu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Timotheo 3:16

Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa katika kufundishia ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na kuwaongoza watu waishi maisha adili,

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:4

Uitafute furaha yako kwa Mwenyezi-Mungu, naye atakujalia unayotamani moyoni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 1:3

Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa; hakuna hata kiumbe kimoja kilichoumbwa pasipo yeye.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:38-39

Maana ninajua hakika kwamba hakuna kitu kiwezacho kututenganisha na upendo wake: Wala kifo, wala uhai; wala malaika au nguvu nyingine za mbinguni; wala yanayotokea sasa, wala yatakayotokea baadaye; wala mamlaka; wala ulimwengu wa juu, wala wa chini kabisa. Hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wimbo Ulio Bora 2:11-12

Tazama, majira ya baridi yamepita, nazo mvua zimekwisha koma; maua yamechanua kila mahali. Wakati wa kuimba umefika; sauti ya hua yasikika mashambani mwetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 46:1

Mungu ni kimbilio letu na nguvu yetu; yeye ni msaada wetu daima wakati wa taabu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 21:4

Yeye atayafuta machozi yao yote; maana kifo hakitakuwako tena, wala uchungu, wala kilio, wala maumivu; maana ile hali ya kale imepita!”

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 13:4-7

Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni. Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya, hafurahii uovu, bali hufurahia ukweli. Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 139:14

Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu, matendo yako ni ya ajabu; wewe wanijua kabisakabisa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 100:4-5

Pitieni milango ya hekalu lake kwa shukrani, ingieni katika nyua zake kwa sifa. Mshukuruni na kulisifu jina lake. Mwenyezi-Mungu ni mwema; fadhili zake zadumu milele, na uaminifu wake katika vizazi vyote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 5:22-23

Lakini matokeo ya kuongozwa na Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi. Hakuna sheria inayoweza kupinga mambo hayo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 14:27

“Nawaachieni amani; nawapeni amani yangu. Siwapi nyinyi kama vile ulimwengu ufanyavyo. Msiwe na wasiwasi, wala msifadhaike.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 5:17

Mtu yeyote akiungana na Kristo huwa kiumbe kipya, mambo ya kale yamepita, hali mpya imefika.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 15:13

Basi, Mungu aliye msingi wa matumaini, awajazeni furaha yote na amani kutokana na imani yenu; tumaini lenu lipate kuongezeka kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 2:8-9

Maana, kwa neema ya Mungu mmekombolewa kwa njia ya imani. Jambo hili si matokeo ya juhudi zenu, bali ni zawadi ya Mungu. Wala halitokani na matendo yenu wenyewe, asije mtu akajivunia kitu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 91:1-2

Anayekaa chini ya ulinzi wa Mungu Mkuu, anayeishi chini ya kivuli cha Mungu Mwenye Nguvu, Kwa hiyo, hutapatwa na maafa yoyote; nyumba yako haitakaribiwa na baa lolote. Maana Mungu atawaamuru malaika zake, wakulinde popote uendapo. Watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe. Utakanyaga simba na nyoka, utawaponda wana simba na majoka. Mungu asema: “Nitamwokoa yule anipendaye; nitamlinda anayenitambua! Akiniita, mimi nitamwitikia; akiwa taabuni nitakuwa naye; nitamwokoa na kumpa heshima. Nitamridhisha kwa maisha marefu, nitamjalia wokovu wangu.” ataweza kumwambia Mwenyezi-Mungu: “Wewe ni kimbilio langu na ngome yangu; Mungu wangu, ninayekutumainia!”

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:14-16

“Nyinyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika. Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa debe, ila huiweka juu ya kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 5:7

Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 136:1

Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake zadumu milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 121:1-2

Natazama juu milimani; msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu watoka kwa Mwenyezi-Mungu, aliyeumba mbingu na dunia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 43:2

Mkipita katika mafuriko, mimi nitakuwa pamoja nanyi; mkipita katika mito, haitawashinda nguvu. Mkitembea katika moto, hamtaunguzwa; mwali wa moto hautawaunguza.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 12:9

Lakini akaniambia: “Neema yangu inatosha kwa ajili yako; maana uwezo wangu hukamilishwa zaidi katika udhaifu.” Basi, ni radhi kabisa kujivunia udhaifu wangu ili uwezo wake Kristo ukae juu yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 55:22

Mwachie Mwenyezi-Mungu mzigo wako, naye atakutegemeza; kamwe hamwachi mwadilifu ashindwe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 19:14

Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yakubalike mbele yako, ee Mwenyezi-Mungu, mwamba wangu na mkombozi wangu!

Sura   |  Matoleo Nakili
Maombolezo 3:22-23

Kwamba fadhili za Mwenyezi-Mungu hazikomi, huruma zake hazina mwisho. Kila kunapokucha ni mpya kabisa, uaminifu wake ni mkuu mno.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wakolosai 3:2

Muwe na hamu ya mambo ya huko juu, na siyo mambo ya hapa duniani.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 31:25

Nguvu na heshima ndizo sifa zake, hucheka afikiriapo wakati ujao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 118:24

Hii ndiyo siku aliyoifanya Mwenyezi-Mungu; tushangilie na kufurahi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 13:5

Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema: “Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 3:20-21

Kwake yeye ambaye kwa nguvu yake ifanyayo kazi ndani yetu aweza kufanya mambo makuu zaidi ya yale tuwezayo kuomba au kufikiria; kwake Mungu uwe utukufu katika kanisa na katika Kristo Yesu, nyakati zote, milele na milele! Amina.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 56:3-4

Ee Mungu Mkuu, hofu inaponishika, mimi nakutumainia wewe. Namtumainia Mungu na kusifu neno lake; namtumainia Mungu, wala siogopi. Binadamu dhaifu atanifanya nini?

Sura   |  Matoleo Nakili

Maombi kwa Mungu

Ee Mungu wangu mwingi wa rehema, wa milele, ukuu wako na nguvu zako hazina kifani. Hakika, kwa moyo wangu wote nasema hakuna mwingine kama wewe, u mtukufu, umevikwa utukufu. Baba, nakushukuru kwa upendo wako na uaminifu wako, kwani hata kabla ya ulimwengu kuumbwa, mimi nilikuwa katika mipango yako, na ukanipa Mfariji, Roho Mtakatifu mpendwa, msaidizi wangu. Katika majaribu, yeye ndiye amenitia nguvu, wewe ndiye mlinzi wangu, umeniokoa kutoka katika hali nyingi, zingine ninazozijua na zingine unazozijua wewe pekee. Neno lako linasema: "Hakuna silaha iliyofanyika juu yangu itakayofanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yangu katika hukumu utauhukumu." Bwana, hakuna usalama mwingine kama kuwa mkononi mwako, na moyo wangu unafurahi kujua kwamba siko peke yangu, bali uwepo wako u pamoja nami popote ninapoenda, kwa maana njia zako ni bora, ni za juu na ni njema. Baba, uimarishe imani yangu, unifundishe kutii, kusikia na kusoma neno lako ili niwe mfano wa upendo wako katika maisha ya wengine. Kwa jina la Yesu. Amina!
Tufuate:

Matangazo


Matangazo