Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Petro 5:7 - Biblia Habari Njema

7 Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema - BHND

7 Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye anajishughulisha sana na mambo yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

7 Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni.

Tazama sura Nakili




1 Petro 5:7
23 Marejeleo ya Msalaba  

Mwenyezi-Mungu huwaangalia waadilifu, na kusikiliza malalamiko yao;


Mkabidhi Mwenyezi-Mungu maisha yako; mtumainie yeye naye atafanya kitu.


Mimi ni maskini na fukara, ee Bwana; lakini ee Bwana wewe wanikumbuka. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu; uje, ee Mungu wangu, usikawie!


Mwachie Mwenyezi-Mungu mzigo wako, naye atakutegemeza; kamwe hamwachi mwadilifu ashindwe.


Mwekee Mwenyezi-Mungu kazi yako, nayo mipango yako itafanikiwa.


Ni nani miongoni mwenu kwa kuwa na wasiwasi sana anaweza kuuongeza muda wa maisha yake?


“Na kuhusu mavazi, ya nini kuwa na wasiwasi? Tazameni maua ya porini jinsi yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayasokoti.


“Basi, msiwe na wasiwasi: ‘Tutakula nini, tutakunywa nini, tutavaa nini!’


Yesu alikuwa sehemu ya nyuma ya mashua, amelala juu ya mto. Basi, wanafunzi wakamwamsha na kumwambia, “Mwalimu, je, hujali kwamba sisi tunaangamia?”


Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kwa sababu hiyo nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula mnachohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu.


Basi, kama hamwezi kufanya jambo dogo kama hilo, kwa nini kuwa na wasiwasi juu ya yale mengine?


Yeye hajali kitu juu ya kondoo kwa sababu yeye ni mtu wa mshahara tu.


Msiwe na wasiwasi juu ya kitu chochote, ila kwa kila hali, mwombeni Mungu katika sala juu ya mahitaji yenu, kwa shukrani.


Sasa, Daudi alikuwa katika matatizo makubwa kwa kuwa watu wake walikuwa na uchungu rohoni mwao kwa kupoteza watoto wao; hivyo wakawa wanamtishia kumpiga mawe. Lakini Daudi alijipa moyo kwa kumtegemea Mwenyezi-Mungu, Mungu wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo