Mungu ni mwezaji wa yote na ameahidi kuwa nawe. Anafanya miujizi na anakutunza, mwamini tu. Yeye ndiye mwokozi wako, ndiyo maana alimtuma mwanawe wa pekee kufa kwa ajili ya dhambi zako.
Kwa Mungu, mambo yote yanawezekana kwa imani yako. Ili kumjua Mungu, unatakiwa kumkaribia kupitia maombi na neno lake. Bwana anatamani umkaribie.
Njia ya Mungu ni kamilifu; neno la Bwana limepimwa. Yeye ni ngao kwa wote wanaomkimbilia. (2 Samweli 22:31)
Mungu akaona kila kitu alichokifanya kuwa ni chema kabisa. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya sita.
Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, uwezo wake wa milele na uungu wake, ingawa havionekani kwa macho, vinafahamika wazi. Watu wanaweza kuyajua mambo hayo kutokana na vitu hivyo alivyoumba Mungu. Kwa hiyo hawana njia yoyote ya kujitetea!
Nikiangalia mbingu, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizozisimika huko, mtu ni nini, ee Mungu, hata umfikirie, binadamu ni nini hata umjali?
Ee Mwenyezi-Mungu, umetenda mambo mengi mno! Yote umeyafanya kwa hekima! Dunia imejaa viumbe vyako! Mbali kule iko bahari - kubwa na pana, ambamo kumejaa viumbe visivyohesabika, viumbe hai, vikubwa na vidogo.
Inueni macho yenu juu mbinguni! Je, ni nani aliyeziumba nyota hizo? Ni yule aziongozaye kama jeshi lake, anayeijua idadi yake yote, aziitaye kila moja kwa jina lake. Kwa sababu yeye ni mwenye nguvu nyingi, hakuna hata moja inayokosekana.
Mbingu ziliumbwa kwa neno la Mwenyezi-Mungu, na vyote vilivyomo kwa pumzi ya mdomo wake.
Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu, matendo yako ni ya ajabu; wewe wanijua kabisakabisa.
Dunia na vyote vilivyomo ni vyake Mwenyezi-Mungu; ulimwengu na wote waishio humo ni mali yake. Ni nani huyo Mfalme mtukufu? Ni Mwenyezi-Mungu, wa majeshi, yeye ndiye Mfalme mtukufu. Maana yeye aliweka misingi ya dunia juu ya bahari; aliisimika imara juu ya mito ya maji.
“Mtatoka Babuloni kwa furaha; mtaongozwa mwende kwa amani. Milima na vilima mbele yenu vitapaza sauti na kuimba, na miti yote mashambani itawapigia makofi. Badala ya michongoma kutamea misonobari, na badala ya mbigili kutamea mihadasi. Hilo litakuwa jambo litakalowakumbusha watu juu ya mambo niliyotenda mimi Mwenyezi-Mungu; ishara ya milele ambayo haitafutwa.”
Mwenyezi-Mungu aliiumba dunia kwa nguvu zake; kwa hekima yake aliuimarisha ulimwengu, kwa akili yake alizitandaza mbingu. Anapotoa sauti yake, maji hunguruma mbinguni, huzusha ukungu kutoka mipaka ya dunia. Huufanya umeme umulike wakati wa mvua, na kuutoa upepo katika ghala zake.
Furahini enyi mbingu na dunia! Bahari na ivume pamoja na vyote vilivyomo! Furahini enyi mashamba na vyote vilivyomo! Ndipo miti yote misituni itaimba kwa furaha,
Kwa hekima Mwenyezi-Mungu aliweka misingi ya dunia, kwa akili aliziimarisha mbingu. Maana yatakupa wingi wa siku, maisha marefu na fanaka kwa wingi. Kwa maarifa yake vilindi vilipasuka, na mawingu yakadondosha umande.
Ezra akaomba kwa sala ifuatayo: “Wewe peke yako ndiwe Mwenyezi-Mungu; ndiwe uliyefanya mbingu na jeshi lake lote, dunia na vyote vilivyomo, bahari na vyote vilivyomo; nawe ndiwe unayevihifadhi hai, na jeshi lote la mbinguni lakuabudu wewe.
Umsifu Mwenyezi-Mungu, ee nafsi yangu! Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, wewe ni mkuu mno! Umejivika utukufu na fahari. Umetokeza chemchemi mabondeni, na mikondo yake ipite kati ya vilima. Hizo zawapatia maji wanyama wote porini. Humo pundamwitu huzima kiu zao. Ndege hujenga viota vyao katika miti ya hapo, hutua katika matawi yake na kuimba. Toka juu angani wainyeshea milima mvua, nayo dunia waitosheleza kwa baraka yako. Waotesha nyasi kwa ajili ya mifugo, na mimea kwa matumizi ya binadamu ili naye ajipatie chakula chake ardhini: Divai ya kumchangamsha, mafuta ya zeituni ya kumfurahisha, na mkate wa kumpa nguvu. Miti mikubwa ya Mwenyezi-Mungu yapata maji ya kutosha; naam, mierezi ya Lebanoni aliyoiotesha. Humo, ndege hujenga viota vyao; korongo hufanya maskani yao katika misonobari. Milima mirefu ni makao ya mbuzimwitu; na pelele hupata maficho yao miambani. Umeuumba mwezi utupimie majira; jua nalo lajua wakati wa kutua. Umejizungushia mwanga kama vazi, umezitandaza mbingu kama hema;
Maana kwake vitu vyote viliumbwa kila kitu duniani na mbinguni, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana: Wenye enzi, watawala, wakuu na wenye nguvu. Vyote viliumbwa kwake na kwa ajili yake.
Mungu, aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo, ni Bwana wa mbingu na dunia; yeye hakai katika hekalu zilizojengwa na watu. Wala hatumikiwi kwa mikono ya watu kana kwamba anahitaji chochote kile, kwa maana yeye mwenyewe ndiye anayewapa watu uhai, anawawezesha kupumua na kuwapa kila kitu.
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Msifuni Mwenyezi-Mungu kutoka mbinguni, msifuni kutoka huko juu mbinguni. Msifuni enyi wanyama wa porini na wafugwao, viumbe vitambaavyo na ndege wote! Msifuni enyi wafalme na mataifa yote; viongozi na watawala wote duniani! Msifuni enyi wavulana na wasichana; wazee wote na watoto pia! Nyote lisifuni jina la Mwenyezi-Mungu, maana jina lake peke yake latukuka; utukufu wake wapita dunia na mbingu. Amewapa watu wake nguvu; heshima kwa watu wote waaminifu, watu wa Israeli wapenzi wake. Msifuni Mwenyezi-Mungu! Msifuni, enyi malaika wake wote, msifuni, enyi majeshi yake yote. Msifuni, enyi jua na mwezi, msifuni, enyi nyota zote zingaazo. Msifuni, enyi mbingu za juu, na maji yaliyo juu ya mbingu. Vyote vilisifu jina la Mwenyezi-Mungu, maana yeye aliamuru, na vyote vikawa. Yeye aliviweka mahali pao daima, kwa amri ambayo haiwezi kubatilishwa.
“Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya dunia? Niambie, kama una maarifa. wanapojificha mapangoni mwao, au kulala mafichoni wakiotea? Ni nani awapaye kunguru chakula chao, makinda yao yanaponililia mimi Mungu, na kurukaruka huku na huko kwa njaa? Ni nani aliyeweka vipimo vyake, wajua bila shaka! Au nani aliyelaza kamba juu yake kuipima? Je, nguzo za dunia zimesimikwa juu ya nini, au nani aliyeliweka jiwe lake la msingi, nyota za asubuhi zilipokuwa zikiimba pamoja, na wana wa Mungu wakapaza sauti za shangwe?
Ndiye aliyeziumba mbingu kwa hekima; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyeitengeneza nchi juu ya vilindi vya maji; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyeumba jua, mwezi na nyota; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Jua liutawale mchana; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Mwezi na nyota vitawale usiku; kwa maana fadhili zake zadumu milele.
Matendo ya Mwenyezi-Mungu ni makuu mno! Wote wanaoyafurahia huyatafakari. Kila afanyacho kimejaa utukufu na fahari; uadilifu wake wadumu milele.
Utukufu wa Mwenyezi-Mungu udumu milele; Mwenyezi-Mungu apendezwe na matendo yake mwenyewe.
Mungu amekifanya kila kitu kiwe kizuri kwa wakati wake. Amempa binadamu hamu ya kujua mambo ya baadaye, lakini hajamjalia fursa ya kuelewa matendo yake Mungu tangu mwanzo mpaka mwisho.
Vilindi vyote vya dunia vimo mikononi mwake, vilele vya milima ni vyake. Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya; kwa mikono yake aliiumba nchi kavu.
Ni mimi niliyeifanya dunia, na kuumba binadamu aishiye humo. Mikono yangu ndiyo iliyozitandaza mbingu, na jeshi lote la nyota liko kwa amri yangu.
Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, vyote vipo kwa uwezo wake na kwa ajili yake. Utukufu na uwe kwake hata milele! Amina.
“Wastahili ee Bwana na Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na nguvu. Maana wewe uliumba vitu vyote, na kwa matakwa yako viliumbwa na vipo.”
Mungu hutandaza kaskazini mahali patupu, na hutundika dunia mahali pasipo na kitu, huyafunga maji mawinguni yawe mazito, nayo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.
Yeye hulifunika anga kwa mawingu, huitengenezea nchi mvua, na kuchipusha nyasi vilimani. Huwapa wanyama chakula chao, na kuwalisha makinda ya kunguru yanapolia.
“Yobu, tangu uzaliwe umewahi kuamuru kupambazuke? na kulifanya pambazuko lijue mahali pake, ili lipate kuikamata dunia kwa pembe zake na kuwatimulia mbali waovu waliomo?
maana wanyama wote porini ni mali yangu, na maelfu ya wanyama milimani ni wangu. Ndege wote wa mwitu ni mali yangu, na viumbe vyote hai mashambani ni vyangu.
Mbona hamniogopi? Nauliza mimi Mwenyezi-Mungu! Kwa nini hamtetemeki mbele yangu? Mimi niliweka mchanga uwe mpaka wa bahari, kizuizi cha daima ambacho bahari haiwezi kuvuka. Ingawa mawimbi yanaupiga, hayawezi kuupita; ingawa yananguruma, hayawezi kuuruka.
Dunia iliumbwa na huyo aketiye juu ya mbingu; kutoka huko wakazi wa dunia ni kama panzi! Yeye amezitandaza mbingu kama pazia, na kuzikunjua kama hema la kuishi.
“Na kuhusu mavazi, ya nini kuwa na wasiwasi? Tazameni maua ya porini jinsi yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayasokoti. Lakini nawaambieni, hata Solomoni mwenyewe na fahari zake zote hakupata kuvikwa vizuri kama ua mojawapo.
Natazama juu milimani; msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu watoka kwa Mwenyezi-Mungu, aliyeumba mbingu na dunia.
Kwa imani sisi tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu; vitu vinavyoonekana kutoka vitu visivyoonekana.
Nilikuwako wakati alipoziweka mbingu, wakati alipopiga duara juu ya bahari; wakati alipoimarisha mawingu mbinguni, alipozifanya imara chemchemi za bahari; wakati alipoiwekea bahari mpaka wake, maji yake yasije yakavunja amri yake; wakati alipoiweka misingi ya dunia.
Nani awezaye kupima maji ya bahari kwa konzi yake, kuzipima mbingu kwa mikono yake? Nani awezaye kuutia udongo wa dunia kikombeni; kuipima milima kwa mizani au vilima kwa kipimo cha uzani?
Ulimpa madaraka juu ya kazi zako zote; uliviweka viumbe vyote chini ya mamlaka yake: Kondoo, ng'ombe, na wanyama wa porini; ndege, samaki, na viumbe vyote vya baharini.
Hata hivyo, Mungu hakuacha kujidhihirisha kwa mambo mema anayowatendea: Huwanyeshea mvua toka angani, huwapa mavuno kwa wakati wake, huwapa chakula na kuijaza mioyo yenu furaha.”
Wanyama wa porini wataniheshimu, kina mbweha na kina mbuni, maana nitaweka maji nyikani, na kububujisha mito jangwani, ili kuwanywesha watu wangu wateule, watu niliowaumba kwa ajili yangu mwenyewe, ili wazitangaze sifa zangu!’
Fadhili zako ee Mwenyezi-Mungu zaenea hata mbinguni; uaminifu wako wafika mawinguni. Uadilifu wako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama vilindi vya bahari. Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, wawalinda wanadamu na wanyama
Aliamuru, akazusha dhoruba kali, ikarusha juu mawimbi ya bahari. Walitupwa juu angani, kisha chini vilindini; uhodari wao ukawaishia katika mkasa huo. Waliyumbayumba na kupepesuka kama walevi; maarifa yao ya uanamaji yakawaishia. Ndipo katika taabu zao wakamlilia Mwenyezi-Mungu, naye akawaokoa katika mateso zao. Aliifanya ile dhoruba kali itulie, nayo mawimbi yakanyamaza.
Maana Mwenyezi-Mungu, ni Mungu mkuu; yeye ni Mfalme mkuu juu ya miungu yote. Vilindi vyote vya dunia vimo mikononi mwake, vilele vya milima ni vyake.
Mungu akasema, “Mianga na iweko angani, itenge mchana na usiku, ioneshe nyakati, majira, siku na miaka, na ingae angani na kuiangazia dunia.” Ikawa hivyo.
Waotesha nyasi kwa ajili ya mifugo, na mimea kwa matumizi ya binadamu ili naye ajipatie chakula chake ardhini: Divai ya kumchangamsha, mafuta ya zeituni ya kumfurahisha, na mkate wa kumpa nguvu.
Nyote lisifuni jina la Mwenyezi-Mungu, maana jina lake peke yake latukuka; utukufu wake wapita dunia na mbingu.
Bahari na ivume na vyote vilivyomo; dunia na wote waishio ndani yake. Enyi mito pigeni makofi; enyi vilima imbeni pamoja kwa shangwe.
Nitabubujisha mito kwenye milima mikavu, na chemchemi katika mabonde. Nitaigeuza nyika kuwa bwawa la maji, na nchi kame kuwa chemchemi za maji. Nitapanda miti huko nyikani: Mierezi, mikakaya, mijohoro, na mizeituni; nitaweka huko jangwani: Miberoshi, mivinje na misonobari. “Nani, ila mimi, aliyemwita shujaa toka mashariki, mtu ambaye hupata ushindi popote aendako? Mimi huyatia mataifa makuchani mwake, naye huwaponda wafalme chini ya miguu yake! Upanga wake huwafanya kuwa kama vumbi, kwa upinde wake huwapeperusha kama makapi. Watu wataona jambo hilo, nao watatambua na kuelewa kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nimetenda hayo, mimi Mtakatifu wa Israeli nimefanya jambo hilo.”
“Sasa, naumba mbingu mpya na dunia mpya. mambo ya zamani hayatakumbukwa tena. Furahini, mkashangilie milele, kwa ajili ya vitu hivi ninavyoumba. Yerusalemu nitaufanya mji wa shangwe, na watu wake watu wenye furaha.
Ee Mwenyezi-Mungu, ni wewe ambaye kwa nguvu zako nyingi na uwezo wako mkuu, umeziumba mbingu na dunia; hakuna kisichowezekana kwako.
Yeye hupeleka amri yake duniani, na neno lake hufikia lengo lake haraka. Hutandaza theluji kama pamba, hutawanya umande kama majivu. Huleta mvua ya mawe kama kokoto na kwa ubaridi wake maji huganda. Kisha hutoa amri, maji hayo yakayeyuka; huvumisha upepo wake, nayo yakatiririka.
Nilikuwa pamoja naye kama fundi stadi, nilikuwa furaha yake kila siku, nikishangilia mbele yake daima, nikifurahia dunia na wakazi wake, na kupendezwa kuwa pamoja na wanadamu.
Amechora duara juu ya uso wa bahari, penye mpaka kati ya mwanga na giza. Mungu akitoa sauti ya kukemea, nguzo za mbingu hutetemeka na kustaajabu. Kwa nguvu zake aliituliza bahari; kwa maarifa yake alimwangamiza dude Rahabu. Kwa pumzi yake aliisafisha anga; mkono wake ulilichoma joka lirukalo. Yamkini haya ni machache tu ya matendo yake, ni minongono tu tunayosikia juu yake. Nani awezaye kujua ukuu wa nguvu yake?”
Mbwamwitu ataishi pamoja na mwanakondoo, chui watapumzika pamoja na mwanambuzi. Ndama na wanasimba watakula pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. Ngombe na dubu watakula pamoja, ndama wao watapumzika pamoja; na simba atakula majani kama ng'ombe. Mtoto mchanga atacheza kwenye shimo la nyoka mtoto ataweza kutia mkono shimoni mwa nyoka wa sumu. Katika mlima mtakatifu wa Mungu hakutakuwa na madhara wala uharibifu. Maana kumjua Mwenyezi-Mungu kutaenea pote nchini, kama vile maji yajaavyo baharini.
ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu wanyofu na waovu.
Nao waliposikia habari hizo waliungana pamoja katika kumwomba Mungu wakisema, “Bwana, wewe ni Muumba wa mbingu na dunia, bahari na vyote vilivyomo!
Viumbe vyote vinangojea kwa hamu Mungu awadhihirishe watoto wake. Maana, sheria ya Roho iletayo uhai kwa kuungana na Kristo Yesu imenikomboa kutoka katika sheria ya dhambi na kifo. Kwa maana, viumbe viliwekwa katika hali ya kutojiweza kabisa, si kwa hiari yao, ila vilifanywa hivyo kwa mapenzi ya Mungu. Hata hivyo yapo matumaini, maana hivyo viumbe navyo vitaokolewa kutoka katika utumwa wa uharibifu, vishiriki uhuru mtukufu wa watoto wa Mungu.
Milima mirefu ni makao ya mbuzimwitu; na pelele hupata maficho yao miambani. Umeuumba mwezi utupimie majira; jua nalo lajua wakati wa kutua. Umejizungushia mwanga kama vazi, umezitandaza mbingu kama hema; Waleta giza, usiku waingia; nao wanyama wote wa porini wanatoka: Wanasimba hunguruma wapate mawindo, humngojea Mungu awape chakula chao. Jua lichomozapo hurudi makwao, na kujipumzisha mapangoni mwao.
Wewe umeniumba, mwili wangu wote; ulinitengeneza tumboni mwa mama yangu. Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu, matendo yako ni ya ajabu; wewe wanijua kabisakabisa. Umbo langu halikufichika kwako nilipotungwa kwa siri na ustadi ndani ya dunia.
“Unapaswa kusikiliza Yobu; nyamaza, usikilize maajabu ya Mungu. Je, wajua jinsi Mungu anavyovipa amri yake, na kufanya umeme wa mawingu yake ungae? Je, wajua jinsi mawingu yanavyoelea angani? Ndizo kazi za ajabu za yule aliye mkamilifu wa maarifa!
Mwenyezi-Mungu, Mkombozi wako, aliyekuumba tangu tumboni mwa mama yako, asema: “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu niliyeumba vitu vyote. Mimi peke yangu nilizitandaza mbingu, niliiumba dunia kwa nguvu yangu mwenyewe!
Ulimwengu wote washangazwa na matendo yako. Wasababisha furaha kila mahali, toka mashariki hata magharibi.
Viumbe vyote vinakutazama kwa hamu, nawe wavipa chakula chao kwa wakati wake. Waufumbua mkono wako kwa ukarimu, watosheleza mahitaji ya kila kiumbe hai.
Kuna mto ambao maji yake hufurahisha mji wa Mungu, makao matakatifu ya Mungu Mkuu. Mungu yumo mjini humo, nao hauwezi kutikiswa; Mungu ataupa msaada alfajiri na mapema.
Ee dunia yote; tetemeka mbele yake! Ameuweka ulimwengu imara, hautatikisika. Furahini enyi mbingu na dunia! Yaambieni mataifa, “Mwenyezi-Mungu anatawala!” Bahari na ivume, pamoja na vyote vilivyomo! Furahini enyi mashamba na vyote vilivyomo! Ndipo miti yote msituni itaimba kwa furaha mbele ya Mwenyezi-Mungu anayekuja naam, anayekuja kuihukumu dunia. Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake zadumu milele!
Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu aliyeziumba mbingu, akazitandaza kama hema, yeye aliyeiunda nchi na vyote vilivyomo, yeye awapaye watu waliomo pumzi, na kuwajalia uhai wote waishio humo:
Kisha, nikaona mbingu mpya na dunia mpya. Mbingu ile ya kwanza na dunia ile ya kwanza vilikuwa vimetoweka, nayo bahari pia haikuwako tena. Basi, Roho akanikumba, naye malaika akanipeleka juu ya mlima mrefu sana. Akanionesha mji mtakatifu, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni, uking'aa kwa utukufu wa Mungu. Mwangaza wake ulikuwa kama wa jiwe la thamani kubwa kama yaspi, angavu kama kioo. Ulikuwa na ukuta mrefu na mkubwa, wenye milango kumi na miwili, na kila mmoja ulilindwa na malaika. Juu ya kila mlango paliandikwa mojawapo ya majina ya makabila kumi na mawili ya Israeli. Kila upande ulikuwa na milango mitatu: Upande wa mashariki milango mitatu, kaskazini milango mitatu, kusini milango mitatu na magharibi milango mitatu. Kuta za mji huo zilikuwa zimejengwa juu ya mawe ya msingi kumi na mawili, na juu ya kila jiwe palikuwa pameandikwa mojawapo ya majina ya wale mitume kumi na wawili wa Mwanakondoo. Basi, yule malaika aliyekuwa anasema nami alikuwa na kijiti cha dhahabu cha kupimia, kwa ajili ya kuupima huo mji, milango yake na kuta zake. Mji wenyewe ulikuwa wa mraba, upana na urefu wake sawa. Basi, malaika akaupima mji huo kwa kijiti chake: Ulikuwa na urefu, upana na kimo cha kama kilomita 2,400. Kisha akaupima ukuta wake pia; nao ulikuwa mita 60 kwa kipimo cha macho cha kibinadamu ambacho malaika alitumia. Ukuta huo ulikuwa umejengwa kwa mawe mekundu ya thamani, na mji wenyewe ulikuwa umejengwa kwa dhahabu safi, angavu kama kioo. Mawe ya msingi wa ukuta huo yalikuwa yamepambwa kwa kila aina ya mawe ya thamani. Jiwe la kwanza la msingi lilikuwa jiwe la thamani jekundu, la pili johari ya rangi ya samawati, la tatu kalkedoni, la nne zumaridi, Nikaona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni. Ulikuwa umetayarishwa vizuri kama bibi arusi aliyepambwa tayari kukutana na mumewe.
Umetokeza chemchemi mabondeni, na mikondo yake ipite kati ya vilima. Hizo zawapatia maji wanyama wote porini. Humo pundamwitu huzima kiu zao. Ndege hujenga viota vyao katika miti ya hapo, hutua katika matawi yake na kuimba.
Yenyewe ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini ikisha ota huwa kubwa kuliko mimea yote. Hukua ikawa mti, hata ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake.”
Ee Mwenyezi-Mungu, Bwana wetu, kweli jina lako latukuka duniani kote! Utukufu wako waenea mpaka juu ya mbingu! Kwa sifa za watoto wadogo na wanyonyao, umejiwekea ngome dhidi ya adui zako, uwakomeshe waasi na wapinzani wako.
Wanaubadili ukweli juu ya Mungu kwa uongo; wanaheshimu na kuabudu kiumbe badala ya Muumba mwenyewe, ambaye ndiye astahiliye sifa milele! Amina.
Ndiye akipaye kila kiumbe chenye uhai chakula; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Mungu wa mbinguni; kwa maana fadhili zake zadumu milele!
Jua lachomoza na kutua; laharakisha kwenda machweoni. Upepo wavuma kusini, wazunguka hadi kaskazini. Wavuma na kuvuma tena, warudia mzunguko wake daima. Mito yote hutiririkia baharini, lakini bahari kamwe haijai; huko ambako mito hutiririkia ndiko huko inakotoka tena.
Sauti ya Mwenyezi-Mungu yasikika juu ya maji; Mungu mtukufu angurumisha radi, sauti ya Mwenyezi-Mungu yasikika juu ya bahari! Sauti ya Mwenyezi-Mungu ina nguvu, sauti ya Mwenyezi-Mungu imejaa fahari.
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mbingu ni kiti changu cha enzi, dunia ni kiti cha kuwekea miguu yangu. Mtanijengea nyumba ya namna gani basi, Mahali nitakapoweza kupumzika? Shangilieni na kufurahi pamoja na Yerusalemu enyi mnaoupenda! Shangilieni pamoja nao enyi nyote mlioulilia! Kama mama, Yerusalemu utawanyonyesha, nanyi mtashiba kwa riziki zake; mtakunywa shibe yenu na kufurahi, kutokana na wingi wa fahari yake. Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nitakuletea fanaka nyingi kama mto, utajiri wa mataifa kama mto uliofurika. Nanyi mtanyonya na kubebwa kama mtoto mchanga, mtabembelezwa kama mtoto magotini mwa mama yake. Kama mama amtulizavyo mwanawe, kadhalika nami nitawatuliza; mtatulizwa mjini Yerusalemu. Mtayaona hayo na mioyo yenu itafurahi; mifupa yenu itapata nguvu kama majani mabichi. Hapo itajulikana kuwa mimi Mwenyezi-Mungu huwalinda watumishi wangu, lakini nikikasirika huwaadhibu maadui zangu.” Mwenyezi-Mungu atakuja kama moto, na magari yake ya vita ni kimbunga. Ataiacha hasira yake ifanye kazi yake kwa ukali, na onyo lake litekelezwe kwa miali ya moto. Mwenyezi-Mungu atatoa hukumu kwa moto, atawaadhibu watu wote kwa upanga; nao atakaowaangamiza watakuwa wengi. Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wapo watu wanaojitakasa na kutawadha wapate kuingia kwenye bustani za ibada za sanamu; wanafanya maandamano na kuhani akiwa kati yao. Watu hao hula nguruwe, panya na vyakula vingine haramu. Watu hao hakika watakufa wote pamoja. Nayajua matendo yao na mawazo yao. Naja kuwakusanya watu wa mataifa yote na lugha zote, wajumuike pamoja na kuuona utukufu wangu. Nitaweka kati yao alama ya uwezo wangu. Watakaosalimika kati yao nitawapeleka kwa watu wa mataifa huko Tarshishi, Puti, Ludi, nchi zenye wapiga upinde stadi; watakwenda pia Tubali na Yowani na nchi ambapo watu hawajapata kusikia umaarufu wangu wala kuuona utukufu wangu. Hao wajumbe wangu watautangaza utukufu wangu katika mataifa hayo. Mimi mwenyewe nilivifanya vitu hivi vyote, na hivi vyote ni mali yangu. Lakini ninachojali mimi ni mtu mnyenyekevu na mwenye majuto, mtu anayetetemeka asikiapo neno langu.
Ee Mwenyezi-Mungu, umetenda mambo mengi mno! Yote umeyafanya kwa hekima! Dunia imejaa viumbe vyako!
Mungu aliigeuza mito kuwa jangwa, chemchemi akazikausha kabisa. Ardhi yenye rutuba akaifanya udongo wa chumvi, kwa sababu ya uovu wa wakazi wake.
Watu hao, kwa makusudi, husahau kwamba zamani Mungu alinena, nazo mbingu na dunia zikaumbwa. Dunia iliumbwa kutoka katika maji na kwa maji;
Kila kitu alichoumba Mungu ni chema, wala hakuna kinachohitaji kukataliwa, bali vyote vipokelewe kwa sala ya shukrani, kwa sababu neno la Mungu na sala hukifanya kitu hicho kikubalike kwa Mungu.
Uinamishe mbingu zako, ee Mwenyezi-Mungu, ushuke chini! Uiguse milima nayo itoe moshi! Lipusha umeme, uwatawanye maadui; upige mishale yako, uwakimbize!
Mwenyezi-Mungu ameumba kila kitu kwa kusudi lake; hata waovu kwa ajili ya siku ya maangamizi.
Kisha malaika akanionesha mto wa maji ya uhai maangavu kama kioo, yakitoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu na Mwanakondoo. Tena akaniambia, “Usiyafiche kama siri maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, maana wakati wa kutimizwa kwake umekaribia. Kwa sasa anayetenda mabaya na aendelee kutenda mabaya, na aliye mchafu aendelee kuwa mchafu. Mwenye kutenda mema na azidi kutenda mema, na aliye mtakatifu na azidi kuwa mtakatifu.” “Sikiliza!” Asema Yesu, “Naja upesi pamoja na tuzo nitakalompa kila mmoja kufuatana na matendo yake. Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho.” Heri yao wale wanaoosha mavazi yao, wapate kuwa na haki ya kula tunda la mti wa uhai, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milango yake. Lakini mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu na wote wanaopenda kusema uongo, watakaa nje ya mji. “Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!” Roho na Bibi arusi waseme, “Njoo!” Kila mtu asikiaye hili, na aseme, “Njoo!” Aliye na kiu na aje; anayependa, na achukue maji ya uhai bila malipo. Mimi Yohane nawapa onyo wote wanaosikia maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki: Mtu yeyote akiongeza chochote katika mambo haya, Mungu atamwongezea mabaa yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu yeyote akipunguza chochote katika maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, Mungu atamnyang'anya sehemu yake katika ule mti wa uhai, na sehemu yake katika mji mtakatifu, ambavyo vimeelezwa katika kitabu hiki. Mto huo ulitiririka kupitia katikati ya barabara kuu ya mji. Kandokando ya mto huo kulikuwa na mti wa uhai unaozaa matunda mara kumi na mbili kwa mwaka, yaani kila mwezi; na majani yake ni dawa ya kuwaponya watu wa mataifa.
Msifuni enyi wafalme na mataifa yote; viongozi na watawala wote duniani! Msifuni enyi wavulana na wasichana; wazee wote na watoto pia! Nyote lisifuni jina la Mwenyezi-Mungu, maana jina lake peke yake latukuka; utukufu wake wapita dunia na mbingu.
niwape wale wanaoomboleza katika Siyoni taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya moyo mzito. Nao wataitwa mialoni madhubuti, aliyopanda Mwenyezi-Mungu kuonesha utukufu wake.
Msifuni Mwenyezi-Mungu enyi viumbe vyake vyote; msifuni popote mlipo katika milki yake. Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu!
Ee Mwenyezi-Mungu, wewe umenichunguza; wewe wanijua mpaka ndani. hata huko upo kuniongoza; mkono wako wa kulia utanitegemeza. Kama ningeliomba giza linifunike, giza linizunguke badala ya mwanga, kwako giza si giza hata kidogo, na usiku wangaa kama mchana; kwako giza na mwanga ni mamoja. Wewe umeniumba, mwili wangu wote; ulinitengeneza tumboni mwa mama yangu. Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu, matendo yako ni ya ajabu; wewe wanijua kabisakabisa. Umbo langu halikufichika kwako nilipotungwa kwa siri na ustadi ndani ya dunia. Wewe uliniona hata kabla sijazaliwa, uliandika kila kitu kitabuni mwako; siku zangu zote ulizipanga, hata kabla ya kuweko ile ya kwanza. Ee Mungu, mawazo yako ni makuu mno; hayawezi kabisa kuhesabika. Ningeyahesabu yangekuwa mengi kuliko mchanga. Niamkapo, bado nipo pamoja nawe. Laiti, ee Mungu, ungewaua watu waovu! Laiti watu wauaji wangeondoka kwangu! Nikiketi au nikisimama, wewe wajua; wajua kutoka mbali kila kitu ninachofikiria. Wanasema vibaya juu yako; wanasema maovu juu ya jina lako! Ee Mwenyezi-Mungu, nawachukia wanaokuchukia; nawadharau sana wale wanaokuasi! Maadui zako ni maadui zangu; ninawachukia kabisakabisa. Unichunguze, ee Mungu, unijue moyo wangu, unipime, uyajue mawazo yangu. Uangalie kama mwenendo wangu ni mbaya, uniongoze katika njia ya milele. Watambua nikienda au nikipumzika; wewe wazijua shughuli zangu zote.
Umkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijaja siku na miaka ambapo utasema: “Sifurahii tena vitu hivyo!”
Tazama, mbingu hata mbingu za mbingu ni mali yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; dunia na vyote vilivyomo ni mali yake.
Mbwamwitu na kondoo watakula pamoja, simba watakula nyasi kama ng'ombe, nao nyoka chakula chao kitakuwa vumbi. Katika mlima wangu wote mtakatifu, hakuna atakayeumiza au kuharibu kitu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Amewapa watu wake nguvu; heshima kwa watu wote waaminifu, watu wa Israeli wapenzi wake. Msifuni Mwenyezi-Mungu!
Wala hawasemi mioyoni mwao; ‘Na tumche Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, anayetujalia mvua kwa wakati wake, anayetupatia mvua za masika na mvua za vuli; na kutupa majira maalumu ya mavuno.’
Wewe uliniona hata kabla sijazaliwa, uliandika kila kitu kitabuni mwako; siku zangu zote ulizipanga, hata kabla ya kuweko ile ya kwanza. Ee Mungu, mawazo yako ni makuu mno; hayawezi kabisa kuhesabika.
“Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari? au kutembea juu ya sakafu ya kilindi cha bahari?
hata hivyo, sauti yao yaenea duniani kote, na maneno yao yafika kingo za ulimwengu. Mungu ameliwekea jua makao yake angani; nalo hutoka kama bwana arusi chumbani mwake, lafurahi kama shujaa aliye tayari kushindana.
Naona kuwa mateso ya wakati huu wa sasa si kitu kamwe kama tukiyalinganisha na ule utukufu utakaodhihirishwa kwetu. Viumbe vyote vinangojea kwa hamu Mungu awadhihirishe watoto wake.
Nyika na nchi kavu vitachangamka, jangwa litafurahi na kuchanua maua. Waliokombolewa na Mwenyezi-Mungu watarudi, watakuja Siyoni wakipiga vigelegele. Watakuwa wenye furaha ya milele, watajaliwa furaha na shangwe; huzuni na kilio vitatoweka kabisa. Litachanua maua kwa wingi kama waridi, litashangilia na kuimba kwa furaha. Mungu atalijalia fahari ya milima ya Lebanoni, uzuri wa mlima Karmeli na wa bonde la Sharoni. Watu watauona utukufu wa Mwenyezi-Mungu, watauona ukuu wa Mungu wetu.
Mbali kule iko bahari - kubwa na pana, ambamo kumejaa viumbe visivyohesabika, viumbe hai, vikubwa na vidogo. Ndimo zinamosafiri meli, na lile dude Lewiyathani uliloliumba licheze humo.
Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nitakuletea fanaka nyingi kama mto, utajiri wa mataifa kama mto uliofurika. Nanyi mtanyonya na kubebwa kama mtoto mchanga, mtabembelezwa kama mtoto magotini mwa mama yake. Kama mama amtulizavyo mwanawe, kadhalika nami nitawatuliza; mtatulizwa mjini Yerusalemu.
“Je, waweza kumwindia simba mawindo yake au kuishibisha hamu ya wana simba; “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya dunia? Niambie, kama una maarifa. wanapojificha mapangoni mwao, au kulala mafichoni wakiotea? Ni nani awapaye kunguru chakula chao, makinda yao yanaponililia mimi Mungu, na kurukaruka huku na huko kwa njaa?
Jambo moja nimemwomba Mwenyezi-Mungu, nalo ndilo ninalolitafuta: Nikae nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu siku zote za maisha yangu; niuone uzuri wake Mwenyezi-Mungu, na kutafuta maongozi yake hekaluni mwake.
Andika jambo hili kwa ajili ya vizazi vijavyo; watakaozaliwa baadaye wamsifu Mwenyezi-Mungu. Kwamba aliangalia chini kutoka patakatifu pake juu, Mwenyezi-Mungu aliangalia dunia kutoka mbinguni, Usijifiche mbali nami wakati wa taabu! Unitegee sikio lako, unijibu upesi wakati ninapokuomba! akasikia lalamiko la wafungwa; akawaachilia huru waliohukumiwa kuuawa. Hivyo watu watatangaza jina la Mwenyezi-Mungu huko Siyoni; sifa zake zitatangazwa huko Yerusalemu, wakati mataifa yatakapokusanyika pamoja na falme zitakutana kumwabudu Mwenyezi-Mungu.
Kwa matendo yako makuu watuitikia na kutuokoa, ewe Mungu wa wokovu wetu; wewe ndiwe tumaini la viumbe vyote, duniani kote na mbali baharini. Kwa nguvu yako uliisimika milima mahali pake. Wewe una nguvu mno! Watuliza mshindo wa bahari na wa mawimbi yake, wakomesha ghasia za watu.
Mbingu ni zako na dunia ni yako pia; ulimwengu na vitu vyote vilivyomo wewe uliviumba. Wewe uliumba kaskazini na kusini; milima Tabori na Hermoni inakusifu kwa furaha.
Aligeuza majangwa kuwa mabwawa ya maji, na nchi kame kuwa chemchemi za maji. Akawahamishia huko wenye njaa, nao wakajenga mji wa kukalika. Walilima mashamba na kupanda mizabibu, wakavuna mazao kwa wingi. Aliwabariki watu wake, wakaongezeka; na idadi ya wanyama wao akaizidisha.
“Je, umewahi kuingia katika bohari za theluji, au kuona bohari za mvua ya mawe ambavyo nimevihifadhi kwa ajili ya wakati wa fujo, kwa ajili ya siku ya mapigano na vita?
Waleta giza, usiku waingia; nao wanyama wote wa porini wanatoka: Wanasimba hunguruma wapate mawindo, humngojea Mungu awape chakula chao. Jua lichomozapo hurudi makwao, na kujipumzisha mapangoni mwao. Hapo naye binadamu huenda kwenye shughuli zake; na kufanya kazi zake mpaka jioni.
Dunia yote na imwogope Mwenyezi-Mungu! Wakazi wote duniani, wamche! Maana alisema na ulimwengu ukawako; alitoa amri nao ukajitokeza.
akaapa kwa jina la Mungu aishiye milele na milele, Mungu aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, bahari na vyote vilivyomo, dunia na vyote vilivyomo. Akasema, “Wakati wa kusubiri zaidi umekwisha!
Enyi watu wote duniani mshangilieni Mungu! Umetupima, ee Mungu, umetujaribu kama madini motoni. Umetuacha tunaswe wavuni; umetubebesha taabu nzito. Umewaacha watu watukanyage; tumepitia motoni na majini. Lakini sasa umetuleta kwenye usalama. Nitakuja nyumbani kwako na sadaka za kuteketezwa, nitakutimizia nadhiri zangu, nilizotamka na kukuahidi mimi mwenyewe nilipokuwa taabuni. Nitakutolea sadaka za kuteketezwa nononono, tambiko za kuteketezwa za kondoo madume; nitatoa sadaka za ng'ombe na mbuzi. Enyi mnaomcha Mungu, njoni nyote mkasikilize, nami nitawasimulieni aliyonitendea. Mimi nilimlilia msaada kwa sauti, sifa zake nikazitamka. Kama ningalinuia maovu moyoni, Mwenyezi-Mungu hangalinisikiliza. Lakini kweli Mungu amenisikiliza; naam, amesikiliza maneno ya sala yangu. Imbeni juu ya utukufu wa jina lake, mtoleeni sifa tukufu!
Shomoro wawili huuzwa kwa sarafu moja ndogo. Lakini hata mmoja wao haanguki chini bila kibali cha Baba yenu. Filipo na Bartholomayo, Thoma na Mathayo aliyekuwa mtozaushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo; Lakini kwa upande wenu, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Kwa hiyo msiogope; nyinyi mna thamani kuliko shomoro wengi.
Mwenyezi-Mungu ana enzi kuu juu mbinguni, ana nguvu kuliko mlio wa bahari, ana nguvu kuliko mawimbi ya maji.
Je miungu ya uongo ya mataifa yaweza kuleta mvua? Au, je, mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je, si wewe ee Mwenyezi-Mungu uliye Mungu wetu? Tunakuwekea wewe tumaini letu, maana wewe unayafanya haya yote.
Sauti za furaha ya ushindi zasikika hemani mwao waadilifu: “Mkono wa Mwenyezi-Mungu umetenda mambo makuu! Mkono wa nguvu wa Mwenyezi-Mungu umeleta ushindi! Mkono wa Mwenyezi-Mungu umetenda mambo makuu!”