Biblia Todo Logo
Mistari ya Biblia
- Matangazo -


AYA KUHUSU MAUTI

AYA KUHUSU MAUTI

Najua kifo si adui tena kwetu sisi tunaomwamini Yesu Kristo, lakini bado ni jambo gumu sana tunapowapoteza wapendwa wetu. Biblia inatufundisha kuhusu aina mbili za kifo: kifo cha kimwili na kifo cha dhambi. Tunapokubali kumpokea Bwana Yesu kama mwokozi wetu, tunakufa kwa dhambi. Kifo cha kimwili ndicho kinachotutenganisha na ulimwengu huu.

Inauma sana kufiwa na mpendwa, lakini tuna tumaini katika Mungu kwamba wamepata uzima wa milele na wako mahali pazuri zaidi. Kwa hivyo, usiruhusu huzuni ikuzidi; furahini kwa sababu mpendwa wako amepata wokovu. Roho Mtakatifu ndiye mfariji wako katika wakati huu mgumu. Mwache akuondolee huzuni na akujaze amani na faraja.

Neno la Mungu linatuhakikishia kwamba hakuna kinachoweza kututenganisha na upendo wa Mungu, hata kifo chenyewe. (Warumi 8:38-39) “Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.” Ni furaha kujua kwamba hata tukifa, tumeshinda, kwa sababu tutakuwa na Baba yetu wa Mbinguni na tutakuwa tumeshinda katika mashindano haya ya maisha.


Yohana 5:24

“Kweli nawaambieni, anayesikia neno langu, na kumwamini yule aliyenituma, anao uhai wa milele. Hatahukumiwa kamwe, bali amekwisha pita kutoka kifoni na kuingia katika uhai.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 25:46

Basi, hawa watakwenda kwenye adhabu ya milele, lakini wale waadilifu watakwenda kwenye uhai wa milele.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 34:22

Mwenyezi-Mungu huokoa maisha ya watumishi wake, wote wanaomkimbilia hawataadhibiwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 6:23

Kwa maana mshahara wa dhambi ni kifo; lakini zawadi anayotoa Mungu ni uhai wa milele katika kuungana na Kristo Yesu, Bwana wetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 1:7

Lakini tukiishi katika mwanga, kama naye alivyo katika mwanga, basi, tutakuwa na umoja sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwanae, inatutakasa dhambi zote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 5:28-29

Msistaajabie jambo hili; maana wakati unakuja ambapo wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake, nao watafufuka: Wale waliotenda mema watafufuka na kuishi, na wale waliotenda maovu watafufuka na kuhukumiwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 5:1

Sasa, kwa vile tumefanywa kuwa waadilifu kwa imani, basi tunayo amani naye Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 3:6

Mtu ambaye hajakomaa bado katika imani asifanywe kuwa kiongozi katika kanisa, asije akajaa majivuno na kuhukumiwa kama vile Ibilisi alivyohukumiwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 14:10-12

Kwa nini basi, wewe wamhukumu ndugu yako? Nawe, kwa nini wamdharau ndugu yako? Sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. Maana Maandiko yanasema: “Kama niishivyo, asema Bwana, kila mtu atanipigia magoti, na kila mmoja atakiri kwamba mimi ni Mungu.” Kwa hiyo, kila mmoja wetu atatoa hoja juu yake mwenyewe mbele ya Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wathesalonike 1:9

Adhabu yao itakuwa kuangamizwa milele na kutengwa mbali na utukufu wake mkuu,

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 8:12

Nitawasamehe makosa yao, wala sitakumbuka tena dhambi zao.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Marko 9:43-48

Mkono wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia katika uhai bila mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili na kwenda katika moto wa Jehanamu. [ Humo, wadudu wake hawafi na moto hauzimiki.] Na mguu wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia katika uhai bila mguu mmoja, kuliko kuwa na miguu yote miwili na kutupwa katika moto wa Jehanamu. [ Humo, wadudu wake hawafi na moto hauzimiki.] Na jicho lako likikukosesha, lingoe! Afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja tu, kuliko kuwa na macho yako yote mawili na kutupwa katika moto wa Jehanamu. Humo wadudu wake hawafi, na huo moto hauzimiki.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 5:16

Kuna tofauti baina ya zawadi ya Mungu na dhambi ya mtu yule mmoja. Maana, baada ya kosa la mtu mmoja, Mungu alitoa hukumu; lakini baada ya makosa ya watu wengi, Mungu aliwapa zawadi yake kwa kuwasamehe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 55:7

Waovu na waache njia zao mbaya, watu wabaya waachane na mawazo yao mabaya; wamrudie Mwenyezi-Mungu apate kuwahurumia, wamwendee Mungu wetu maana atawasamehe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 3:18

“Anayemwamini Mwana hahukumiwi; asiyemwamini amekwisha hukumiwa, kwa sababu hakumwamini Mwana wa pekee wa Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 20:10

Naye Ibilisi aliyekuwa anawapotosha, akatupwa ndani ya ziwa linalowaka madini ya kiberiti, walimo yule mnyama na yule nabii wa uongo, nao watateswa mchana na usiku, milele na milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 3:17

Maana Mungu hakumtuma Mwanae ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali aukomboe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 20:14-15

Kisha Kifo na Kuzimu vikatupwa ndani ya ziwa la moto. Ziwa hili la moto ndicho kifo cha pili. Mtu yeyote ambaye jina lake halikupatikana limeandikwa katika kitabu cha uhai, alitupwa katika ziwa la moto.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 23:40

Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake akisema: “Wewe humwogopi Mungu hata kidogo? Wewe umepata adhabu hiyohiyo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 13:41-42

Mwana wa Mtu atawatuma malaika wake wawakusanye kutoka katika ufalme wake wale wote wenye kusababisha dhambi, na wote wenye kutenda maovu, na kuwatupa katika tanuri ya moto, na huko watalia na kusaga meno.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:34

Ni nani atakayewahukumu? Hakuna! Maana Kristo ndiye aliyekufa, tena alifufuka kutoka kwa wafu na anakaa upande wa kulia wa Mungu. Yeye anatuombea!

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 7:13-14

“Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba. Kwa maana njia inayoongoza kwenye maangamizi ni pana, na mlango wa kuingilia humo ni mpana; waendao njia hiyo ni wengi. Lakini njia inayoongoza kwenye uhai ni nyembamba, na mlango wa kuingilia humo ni mwembamba; ni watu wachache tu wanaoweza kuigundua njia hiyo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 3:1

Ndugu zangu, wengi wenu msiwe waalimu. Kama mjuavyo, sisi waalimu tutapata hukumu kubwa zaidi kuliko wengine.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 16:23-24

Huyo tajiri, akiwa na mateso makali huko kuzimu, akainua macho yake, akamwona Abrahamu kwa mbali na Lazaro karibu naye. Basi, akaita kwa sauti: ‘Babu Abrahamu, nionee huruma; umtume Lazaro angalau achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe ulimi wangu, maana ninateseka mno katika moto huu.’

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 3:16

Maana Mungu aliupenda ulimwengu hivi hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uhai wa milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 10:27

Linalobaki ni kungojea tu kwa hofu hukumu ya Mungu na moto mkali utakaowaangamiza wote wanaompinga.

Sura   |  Matoleo Nakili
Marko 16:16

Anayeamini na kubatizwa ataokolewa. Asiyeamini atahukumiwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Petro 2:4

Malaika walipotenda dhambi, Mungu hakuwahurumia, bali aliwatupa katika moto wa Jehanamu ambako wamefungwa wakingojea siku ile ya hukumu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:1

Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu kwa wale ambao katika maisha yao wameungana na Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yuda 1:7

Kumbukeni pia Sodoma na Gomora, na miji ya kandokando yake; wenyeji wake walifanya kama wale malaika; walifanya uzinzi na mambo yaliyo kinyume cha maumbile, wakapewa hukumu ya moto wa milele, iwe onyo kwa watu wote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 12:2

Mtu mwema hufadhiliwa na Mwenyezi-Mungu, lakini mwenye nia mbaya hulaaniwa na Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 25:41

“Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni mbele yangu enyi mliolaaniwa! Nendeni katika moto wa milele aliotayarishiwa Ibilisi na malaika wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 11:7

Kwa imani Noa alionywa na Mungu juu ya mambo ya baadaye ambayo hayakuwa yameonekana bado. Alimtii Mungu, akajenga ile safina ambamo aliokolewa yeye pamoja na jamaa yake. Kutokana na hayo ulimwengu ulihukumiwa, naye Noa akapokea uadilifu unaotokana na imani.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 2:5-8

Lakini unao ugumu na ukaidi wa moyo, na hivyo unajirundikia adhabu kwa siku ile ya ghadhabu wakati hukumu ya haki ya Mungu itakapodhihirishwa. Siku hiyo Mungu atamlipa kila mmoja kufuatana na matendo yake. Wale wanaozingatia kutenda mema, kutafuta utukufu na heshima ya Mungu na kutokufa, watapata uhai wa milele. Lakini wale wengine wenye ubinafsi, wenye kukataa mambo ya haki na kufuata uovu, wataangukiwa na ghadhabu na hasira ya Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 5:18

Basi, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta hukumu kwa binadamu wote, kadhalika kitendo kiadilifu cha mtu mmoja kinawapa wote uadilifu na uhai.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 3:9

Ikiwa basi, kulikuwa na utukufu katika huduma ile iliyoleta hukumu, ni wazi kwamba huduma iletayo uadilifu itakuwa na utukufu mkuu zaidi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 9:17

Waovu wataishia kuzimu; naam, mataifa yote yanayomsahau Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:3

Mungu ametekeleza jambo lile ambalo sheria haikuweza kutekeleza kwa sababu ya udhaifu wa binadamu. Mungu alimtuma Mwanae akiwa mwenye mwili sawa na miili yetu sisi wenye dhambi, ili aikabili dhambi, na kwa mwili huo akaiangamiza dhambi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Tito 3:10-11

Mtu anayesababisha mafarakano mpe onyo la kwanza na la pili, kisha achana naye. Wajua kwamba mtu wa namna hiyo amepotoka kabisa, na dhambi zake zathibitisha kwamba amekosea.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 66:24

“Kisha watakwenda kuziona maiti za wale walioniasi. Wadudu watakaowala hawatakufa, na moto utakaowachoma hautazimika kamwe. Watakuwa chukizo kwa watu wote.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 3:18-19

“Anayemwamini Mwana hahukumiwi; asiyemwamini amekwisha hukumiwa, kwa sababu hakumwamini Mwana wa pekee wa Mungu. Na hukumu yenyewe ndiyo hii: Mwanga umekuja ulimwenguni lakini watu wakapenda giza kuliko mwanga, kwani matendo yao ni maovu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 12:5

Nitawaonesheni yule ambaye ni lazima kumwogopa: Mwogopeni yule ambaye baada ya kuua ana uwezo wa kumtupa mtu katika moto wa Jehanamu. Naam, ninawaambieni, mwogopeni huyo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 5:19-21

Basi, matendo ya kidunia yanajulikana: Uzinzi, uasherati, ufisadi; Sikilizeni! Ni mimi Paulo ninayesema nanyi! Kama mkikubali kutahiriwa, Kristo hatawafaidia chochote. kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, choyo, mabishano, mafarakano; husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine kama hayo. Nawaambieni tena kama nilivyokwisha sema: Watu wanaotenda mambo hayo hawataupata ufalme wa Mungu uwe wao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 21:8

Lakini watu waoga, wasioamini, wapotovu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, na waongo wote, mahali pao patakuwa ndani ya lile ziwa linalowaka moto na madini ya kiberiti; hicho ndicho kifo cha pili.”

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 5:11-12

Na, ushahidi wenyewe ndio huu: Mungu alitupatia uhai wa milele, na uhai huo uko kwa Bwana. Yeyote aliye na Mwana wa Mungu anao uhai huo; asiye na Mwana wa Mungu, hana uhai.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 1:18-20

Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi na uovu wote wa binadamu ambao kwa njia zao mbaya wanaupinga ukweli usijulikane. Kwa maana, yote yanayoweza kujulikana juu ya Mungu ni wazi kwao; maana Mungu mwenyewe ameyadhihirisha. Hapo kale, Mungu aliwaahidi watu hii Habari Njema kwa njia ya manabii wake katika Maandiko Matakatifu. Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, uwezo wake wa milele na uungu wake, ingawa havionekani kwa macho, vinafahamika wazi. Watu wanaweza kuyajua mambo hayo kutokana na vitu hivyo alivyoumba Mungu. Kwa hiyo hawana njia yoyote ya kujitetea!

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:20

Lakini waovu wataangamia, maadui za Mwenyezi-Mungu watanyauka kama maua nyikani; naam, watatoweka kama moshi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 73:27

Anayejitenga nawe, hakika ataangamia. Anayekukana, utamwangamiza.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 14:32

Mwovu huangamizwa kwa matendo yake maovu, lakini mwadilifu hupata usalama kwa unyofu wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 10:28

Msiwaogope wale wauao mwili, lakini hawawezi kuiua roho. Afadhali zaidi kumwogopa yule awezaye kuuangamiza mwili pamoja na roho katika moto wa Jehanamu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 2:3

Basi, sisi tutaokokaje kama hatuujali wokovu mkuu kama huu? Kwanza Bwana mwenyewe aliutangaza wokovu huu, na wale waliomsikia walituthibitishia kwamba ni kweli.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 22:13

Hapo mfalme akawaambia watumishi, ‘Mfungeni miguu na mikono mkamtupe nje gizani; huko atalia na kusaga meno.’”

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 3:17

Yeye anacho mikononi mwake chombo cha kupuria nafaka aipure nafaka yake, akusanye ngano katika ghala, na makapi ayachome kwa moto usiozimika.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 11:22

Ona, basi, jinsi Mungu alivyo mwema na mkali. Yeye ni mkali kwa wale walioanguka, na ni mwema kwako wewe ikiwa utaendelea katika wema wake; la sivyo, nawe pia utakatwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wakolosai 3:6

Kwa sababu ya mambo hayo hasira ya Mungu huwajia wote wanaomwasi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 3:5

“Mshindi atavikwa hivyo kwa mavazi meupe. Nami sitalifuta jina lake kutoka katika kitabu cha uhai; tena nitamkiri kwamba ni wangu mbele ya Baba yangu na mbele ya malaika wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 3:36

Anayemwamini Mwana anao uhai wa milele; asiyemwamini Mwana hatakuwa na uhai wa milele, bali ghadhabu ya Mungu hubaki juu yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 1:32

Wanajua kwamba sheria ya Mungu yasema kwamba watu wanaoishi mithili hiyo, wanastahili kifo. Zaidi ya hayo, siyo tu kwamba wanafanya mambo hayo wao wenyewe, bali hata huwapongeza wale wanaofanya mambo hayohayo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 18:34-35

“Basi, huyo bwana alikasirika sana, akamtoa huyo mtumishi aadhibiwe mpaka hapo atakapolipa deni lote. Na baba yangu aliye mbinguni atawafanyieni vivyo hivyo kama kila mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake kwa moyo wake wote.”

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wathesalonike 2:12

Matokeo yake ni kwamba wote wasioamini ukweli, bali wanafurahia dhambi, watahukumiwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 4:17

Wakati wa hukumu umefika, na hukumu hiyo inaanza na watu wake Mungu mwenyewe. Ikiwa hukumu hiyo inaanzia kwetu sisi, basi, mwisho wake utakuwa namna gani kwa wale wasioamini Habari Njema ya Mungu?

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 6:16

Mnajua kwamba mkijitolea nyinyi wenyewe kama watumwa na kumtii fulani, mnakuwa kweli watumwa wake mtu huyo – au watumwa wa dhambi na matokeo yake ni kifo, au wa utii na matokeo yake ni kufanywa kuwa waadilifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 12:28

Uadilifu ni njia ya uhai, lakini uovu huongoza katika mauti.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:155

Waovu hawataokolewa kamwe, maana hawajali juu ya masharti yako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 48:22

Lakini Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu waovu sitawapa amani.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 146:9

Mwenyezi-Mungu huwalinda wageni, huwategemeza wajane na yatima; lakini huipotosha njia ya waovu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 53:5

Lakini alijeruhiwa kwa sababu ya dhambi zetu, aliumizwa kwa sababu ya maovu yetu. Kwa kuadhibiwa kwake sisi tumepata uhai; kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Petro 3:9

Bwana hakawii kutimiza yale aliyoahidi kama watu wengine wanavyofikiri kuwa atakawia. Yeye ana saburi kwa ajili yenu, maana hapendi hata mmoja wenu apotee, bali huwavuta wote wapate kutubu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 12:36-37

“Basi, nawaambieni, siku ya hukumu watu watapaswa kujibu juu ya kila neno lisilofaa wanalosema. Maana kwa maneno yako utakubaliwa kuwa mwadilifu, na kwa maneno yako utahukumiwa kuwa na hatia.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 5:6

Msikubali kudanganywa na mtu kwa maneno matupu; maana, kwa sababu ya mambo kama hayo ghadhabu ya Mungu huwajia wote wasiomtii.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 21:27

Lakini hakuna chochote kilicho najisi kitakachoingia humo; wala mtu yeyote atendaye mambo ya kuchukiza au ya uongo hataingia humo. Ni wale tu walioandikwa katika kitabu cha uhai cha Mwanakondoo ndio watakaoingia ndani.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 6:7

Msidanganyike; Mungu hafanyiwi dhihaka. Alichopanda mtu ndicho atakachovuna.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 1:4-6

Lakini waovu sivyo walivyo; wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. Kwa hiyo watu waovu wataanguka wakati wa hukumu, wenye dhambi hawatakaa na kusanyiko la waadilifu. Maana Mwenyezi-Mungu huziongoza njia za waadilifu; lakini njia za waovu zitaishia katika maangamizi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 23:33

Enyi kizazi cha nyoka wenye sumu! Mnawezaje kuiepa hukumu ya moto wa Jehanamu?

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 2:8

Lakini wale wengine wenye ubinafsi, wenye kukataa mambo ya haki na kufuata uovu, wataangukiwa na ghadhabu na hasira ya Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 15:22-23

Kama vile watu wote wanavyokufa kwa kujiunga na Adamu, vivyo hivyo wote watafufuliwa kwa kuungana na Kristo. Lakini kila mmoja kwa mpango wake: Kristo kwanza; halafu wale walio wake Kristo wakati Kristo atakapokuja.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 24:51

Atamwadhibu vibaya na kumweka kundi moja na wanafiki. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 10:29

Je, mtu yule anayempuuza Mwana wa Mungu na kuidharau damu ya agano la Mungu iliyomtakasa, mtu anayemtukana Roho wa Mungu, anastahili kupata adhabu kali ya namna gani?

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 13:27-28

Lakini yeye atasema: ‘Sijui nyinyi mmetoka wapi; ondokeni mbele yangu, enyi nyote watenda maovu.’ Ndipo kutakuwa na kulia na kusaga meno, wakati mtakapowaona Abrahamu, Isaka na Yakobo na manabii wote wapo katika ufalme wa Mungu, lakini nyinyi wenyewe mmetupwa nje!

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 8:24

Ndiyo maana niliwaambieni mtakufa katika dhambi zenu. Kama msipoamini kwamba ‘Mimi Ndimi Niliye’, mtakufa katika dhambi zenu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Petro 3:7

Lakini mbingu na dunia ya sasa zahifadhiwa kwa neno la Mungu kwa ajili ya kuharibiwa kwa moto. Zimewekwa kwa ajili ya siku ile ambapo watu wasiomcha Mungu watahukumiwa na kuangamizwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:29-30

Basi, kama jicho lako la kulia linakukosesha, lingoe ukalitupe mbali. Afadhali zaidi kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote kutupwa katika moto wa Jehanamu. “Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao. Na kama mkono wako wa kulia unakukosesha, ukate ukautupe mbali. Afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote uende katika moto wa Jehanamu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 5:12

Kwa njia ya mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, nayo ikasababisha kifo. Hivyo kifo kimeenea katika jumuiya yote ya binadamu, kwa maana wote wametenda dhambi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 4:12

Mungu peke yake ndiye mwenye kuweka sheria na kuhukumu. Ni yeye peke yake anayeweza kuokoa na kuangamiza. Basi, wewe ni nani hata umhukumu binadamu mwenzako?

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 2:11

“Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Mshindi hataumizwa na kifo cha pili.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 22:15

Lakini mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu na wote wanaopenda kusema uongo, watakaa nje ya mji.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 25:30

Na kuhusu huyu mtumishi asiye na faida, mtupeni nje gizani! Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.’

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 12:48

Asiyeyashika maneno yangu anaye wa kumhukumu: Neno lile nililosema ni hakimu wake siku ya mwisho.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 1:18

Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi na uovu wote wa binadamu ambao kwa njia zao mbaya wanaupinga ukweli usijulikane.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 1:6

Tukisema kwamba tuna umoja naye, na papo hapo tunaishi gizani, tutakuwa tumesema uongo wala hatuishi kwa ukweli kwa maneno na matendo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 9:26

Mtu akinionea aibu mimi na mafundisho yangu, Mwana wa Mtu atamwonea aibu mtu huyo wakati atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 7:21-23

“Si kila aniambiaye, ‘Bwana, Bwana’, ataingia katika ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza matakwa ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile ya hukumu: ‘Bwana, Bwana! Kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi’. Hapo nitawaambia: ‘Sikuwajua nyinyi kamwe; ondokeni mbele yangu, enyi watenda maovu.’

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 3:23

Watu wote wametenda dhambi na wametindikiwa utukufu wa Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:38

Lakini wakosefu wote wataangamizwa; na wazawa wao watafutiliwa mbali.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 6:4-6

Maana watu waliokwisha kuangaziwa, wakaonja zawadi za mbinguni, wakashirikishwa Roho Mtakatifu na kuonja wema wa neno la Mungu na nguvu za ulimwengu ujao, kisha wakaiasi imani yao, haiwezekani kuwarudisha hao watubu tena. Hao wanamsulubisha tena Mwana wa Mungu kwa makusudi na kumwaibisha hadharani.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 55:15

Acha kifo kiwafumanie maadui zangu; washuke chini Kuzimu wangali hai; maana uovu umewajaa moyoni mwao.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 3:15

lakini kama alichojenga kitaunguzwa, basi, atapoteza tuzo lake; lakini yeye mwenyewe ataokolewa kana kwamba ameponyoka kutoka motoni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 20:15

Mtu yeyote ambaye jina lake halikupatikana limeandikwa katika kitabu cha uhai, alitupwa katika ziwa la moto.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 12:47-48

Mtumishi ambaye anajua matakwa ya bwana wake lakini hajiweki tayari kufanya anavyotakiwa, atapigwa sana. Lakini yule afanyaye yanayostahili adhabu bila kujua, atapigwa kidogo. Aliyepewa vingi atadaiwa vingi; aliyepewa vingi zaidi atadaiwa vingi zaidi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 14:12

Kwa hiyo, kila mmoja wetu atatoa hoja juu yake mwenyewe mbele ya Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 7:19

Kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 5:20-21

kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, choyo, mabishano, mafarakano; husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine kama hayo. Nawaambieni tena kama nilivyokwisha sema: Watu wanaotenda mambo hayo hawataupata ufalme wa Mungu uwe wao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 15:10

Adhabu kali ipo kwa wanaoacha mwenendo mwema; yeyote achukiaye kuonywa atakufa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 10:32-33

“Kila mtu anayekiri hadharani kwamba yeye ni wangu, mimi pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni. Lakini yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 16:26

Licha ya hayo, kati yetu na nyinyi kumewekwa shimo kubwa, ili wanaotaka kuja kwenu kutoka huku wasiweze, na wanaotaka kutoka kwenu kuja kwetu wasiweze.’

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Petro 2:9

Kwa hiyo, basi, Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa katika majaribu watu wanaomcha Mungu, na jinsi ya kuwaweka waovu katika adhabu hadi siku ile ya hukumu,

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 5:14

Kuzimu inawangoja kwa hamu kubwa, imepanua kinywa chake mpaka mwisho. Waheshimiwa pamoja na raia wa Yerusalemu wanaingia humo makundi kwa makundi, kadhalika na wote wanaousherehekea.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 24:12

Kwa sababu ya ongezeko la uhalifu, upendo wa watu wengi utafifia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 5:5

Jueni wazi kwamba mwasherati yeyote au mchafu au mchoyo, (ambao ni sawa na kuabudu sanamu), au mtu yeyote wa aina hiyo hataambulia chochote katika ufalme wa Kristo na wa Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 20:14

Kisha Kifo na Kuzimu vikatupwa ndani ya ziwa la moto. Ziwa hili la moto ndicho kifo cha pili.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 6:8

Apandaye katika tamaa za kidunia, atavuna humo uharibifu; lakini akipanda katika Roho, atavuna kutoka kwa Roho uhai wa milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 13:3

Nawaambieni hakika sivyo; lakini nanyi, hali kadhalika, msipotubu mtaangamia kama wao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 13:49-50

Ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati: Malaika watatokea, watawatenganisha watu wabaya na watu wema, Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi. Zikaota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina. na kuwatupa hao wabaya katika tanuri ya moto. Huko watalia na kusaga meno.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 28:13

Afichaye makosa yake hatafanikiwa; lakini anayeungama na kuyaacha atapata rehema.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 1:15

Tamaa ikiiva huzaa dhambi; nayo dhambi ikikomaa huzaa kifo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 10:26-27

Maana, tukiendelea kutenda dhambi makusudi baada ya kufahamu ukweli, hakuna tambiko iwezayo kutolewa tena kwa ajili ya kuondoa dhambi. Linalobaki ni kungojea tu kwa hofu hukumu ya Mungu na moto mkali utakaowaangamiza wote wanaompinga.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 2:6

Siku hiyo Mungu atamlipa kila mmoja kufuatana na matendo yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 5:10

Maana sote ni lazima tusimame mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mmoja apokee anayostahili kwa matendo aliyoyafanya wakati alipokuwa anaishi duniani, mema au mabaya.

Sura   |  Matoleo Nakili
Ufunuo 3:16

Basi, kwa kuwa hali yako ni vuguvugu, si baridi wala si moto, nitakutapika!

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 1:19

na ushike imani yako na dhamiri njema. Watu wengine hawakusikiliza dhamiri zao na hivyo wakaiharibu imani yao.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 11:14

Wala si ajabu, maana hata Shetani mwenyewe hujisingizia kuwa malaika wa mwanga!

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 1:24-27

Kwa sababu hiyo, Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya za mioyo yao na kufanyiana mambo ya aibu kwa miili yao. Wanaubadili ukweli juu ya Mungu kwa uongo; wanaheshimu na kuabudu kiumbe badala ya Muumba mwenyewe, ambaye ndiye astahiliye sifa milele! Amina. Kwa hiyo, Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya. Hata wanawake wanabadili matumizi yanayopatana na maumbile. Nao wanaume hali kadhalika, wanaacha kufuata matumizi ya maumbile ya mume na mke, wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume wanafanyiana mambo ya aibu, na hivyo wanajiletea wenyewe adhabu wanayostahili kwa vitendo vyao viovu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 18:23-35

Ndiyo maana ufalme wa mbinguni unafanana na mfalme mmoja aliyeamua kukagua hesabu za watumishi wake. Ukaguzi ulipoanza, akaletewa mtu mmoja aliyekuwa na deni la fedha talanta 10,000. Mtu huyo hakuwa na chochote cha kulipa; hivyo bwana wake aliamuru auzwe, yeye, mke wake, watoto wake na vitu vyote alivyokuwa navyo, ili deni lilipwe. Basi, huyo mtumishi akapiga magoti mbele yake, akasema, ‘Unisubiri nami nitakulipa deni lote’. Yule bwana alimwonea huruma, akamsamehe lile deni, akamwacha aende zake. “Lakini huyo mtumishi akaondoka, akamkuta mmoja wa watumishi wenzake aliyekuwa na deni lake fedha dinari 100. Akamkamata, akamkaba koo akisema, ‘Lipa deni lako!’ Huyo mtumishi mwenzake akapiga magoti, akamwomba, ‘Unisubiri nami nitakulipa’. kisha akasema, “Nawaambieni kweli, msipogeuka na kuwa kama watoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Lakini yeye hakutaka, bali alimtia gerezani mpaka hapo atakapolipa lile deni. “Basi, watumishi wenzake walipoona jambo hilo walisikitika sana, wakaenda kumpasha habari bwana wao juu ya mambo hayo yaliyotukia. Hapo yule bwana alimwita huyo mtumishi, akamwambia, ‘Wewe ni mtumishi mbaya sana! Uliniomba, nami nikakusamehe deni lako lote. Je, haikukupasa nawe kumhurumia mtumishi mwenzako kama nilivyokuhurumia?’ “Basi, huyo bwana alikasirika sana, akamtoa huyo mtumishi aadhibiwe mpaka hapo atakapolipa deni lote. Na baba yangu aliye mbinguni atawafanyieni vivyo hivyo kama kila mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake kwa moyo wake wote.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 12:14

Jitahidini kuishi kwa amani na watu wote. Ishini maisha ya utakatifu, kwa sababu hakuna mtu atakayemwona Bwana bila ya maisha kama hayo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 23:15

“Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumpata mtu mmoja afuate dini yenu. Mnapompata, mnamfanya astahili maradufu kwenda katika moto wa Jehanamu kuliko nyinyi wenyewe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 6:24-26

Lakini ole wenu nyinyi mlio matajiri, maana mmekwisha pata faraja yenu. Ole wenu nyinyi mnaoshiba sasa, maana baadaye mtasikia njaa. Ole wenu nyinyi mnaocheka kwa furaha sasa, maana baadaye mtaomboleza na kulia. Ole wenu nyinyi iwapo watu wote wanawasifu, maana wazee wao waliwafanyia manabii wa uongo vivyo hivyo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:119

Waovu wote wawaona kuwa takataka, kwa hiyo mimi napenda maamuzi yako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 14:10

Kwa nini basi, wewe wamhukumu ndugu yako? Nawe, kwa nini wamdharau ndugu yako? Sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 7:24-27

“Kwa hiyo, kila mtu anayeyasikia maneno yangu na kuyazingatia, anafanana na mtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga nyumba hiyo. Lakini haikuanguka kwa sababu ilikuwa imejengwa juu ya mwamba. “Lakini yeyote anayesikia maneno yangu haya bila kuyazingatia, anafanana na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga. Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga nyumba hiyo, nayo ikaanguka; tena anguko hilo lilikuwa kubwa.”

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 2:8

Tena Maandiko yasema: “Jiwe hilo ni jiwe la kujikwaa, mwamba wa kuwaangusha watu.” Watu hujikwaa kwa sababu hawauamini ule ujumbe; na ndivyo walivyopangiwa tangu mwanzo.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Timotheo 2:12

Tukiendelea kuvumilia, tutatawala pia pamoja naye. Tukimkana, naye pia atatukana.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:30

Na kama mkono wako wa kulia unakukosesha, ukate ukautupe mbali. Afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote uende katika moto wa Jehanamu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 19:13

Unikinge mimi mtumishi wako na makosa ya makusudi, usikubali hayo yanitawale. Hapo nitakuwa mkamilifu, wala sitakuwa na hatia ya kosa kubwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 31:17-18

Usiniache niaibike ee Mwenyezi-Mungu, maana mimi ninakuomba; lakini waache waovu waaibike, waache wapotelee kwa mshangao huko kuzimu. Izibe midomo ya hao watu waongo, watu walio na kiburi na majivuno, ambao huwadharau watu waadilifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 2:17

Ulimwengu pamoja na vitu vyake vyote vyenye kutamanika unapita; lakini mtu atendaye atakalo Mungu, anaishi milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 3:12

Basi ndugu, jihadharini asije akawako yeyote miongoni mwenu aliye na moyo mbaya hivyo na asiyeamini hata kujitenga na Mungu aliye hai.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 4:4

Nyinyi ni watu msio na uaminifu kama wazinzi. Je, hamjui kwamba kuwa rafiki wa ulimwengu ni kuwa adui wa Mungu? Yeyote anayetaka kuwa rafiki wa ulimwengu anajifanya adui wa Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:13

Lakini Mwenyezi-Mungu humcheka mwovu, kwani ajua mwisho wake u karibu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 14:14

Mtu mpotovu atavuna matunda ya mwenendo wake, naye mtu mwema atapata tuzo la matendo yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:37-39

Lakini, katika mambo haya yote, tumepata ushindi mkubwa kwa msaada wake yeye aliyetupenda. Maana ninajua hakika kwamba hakuna kitu kiwezacho kututenganisha na upendo wake: Wala kifo, wala uhai; wala malaika au nguvu nyingine za mbinguni; wala yanayotokea sasa, wala yatakayotokea baadaye; wala mamlaka; wala ulimwengu wa juu, wala wa chini kabisa. Hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 11:42

“Lakini ole wenu Mafarisayo, kwa sababu mnatoza watu zaka hata juu ya majani ya kukolezea chakula, mchicha na majani mengine, na huku hamjali juu ya haki na upendo kwa Mungu. Mambo haya iliwapasa muwe mmeyazingatia bila kuyasahau yale mengine.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 92:7

Kwamba waovu waweza kustawi kama nyasi, watenda maovu wote waweza kufanikiwa, lakini mwisho wao ni kuangamia milele,

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 3:19-20

Tunajua kwamba sheria huwahusu walio chini ya sheria hiyo, hata hawawezi kuwa na kisingizio chochote, na ulimwengu wote uko chini ya hukumu ya Mungu. Naam, iko faida kwa kila upande. Kwanza, Mungu aliwakabidhi Wayahudi ujumbe wake. Maana hakuna binadamu yeyote anayekubaliwa kuwa mwadilifu mbele yake Mungu kwa kushika sheria; kazi ya sheria ni kumwonesha tu mtu kwamba ametenda dhambi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 12:30

“Yeyote asiyejiunga nami, ananipinga; na yeyote asiyekusanya pamoja nami, hutawanya.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 5:5

mkabidhini mtu huyo kwa Shetani ili mwili wake uharibiwe na roho yake iweze kuokolewa siku ile ya Bwana.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 6:19-20

“Msijiwekee hazina hapa duniani ambako nondo na kutu huharibu, na wezi huingia na kuiba. “Basi, unapomsaidia maskini, usijitangaze. Usifanye kama wanafiki wafanyavyo katika masunagogi na njiani ili watu wawasifu. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao. Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 5:16

Basi, nasema hivi: Mwenendo wenu na uongozwe na Roho, nanyi hamtafuata tena tamaa za kidunia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:13

“Nyinyi ni chumvi ya dunia. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 1:12

Heri mtu anayebaki mwaminifu katika majaribu, kwani akisha stahimili, atapewa tuzo la uhai ambalo Mungu aliwaahidi wale wanaompenda.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 3:19

Mwisho wao ni kuangamia, kwani tumbo lao ndilo mungu wao; wanaona fahari juu ya mambo yao ya aibu, hufikiria tu mambo ya kidunia.

Sura   |  Matoleo Nakili

Maombi kwa Mungu

Ee Mungu Mwenyezi, kwako utukufu na heshima! Mungu wangu wa mbinguni, nakuomba kwa jina la Yesu, katika wakati huu wa kuagana, uwatie nguvu familia na marafiki. Ninaomba Roho wako Mtakatifu awe mfariji wao, akiwapa amani ambayo wewe pekee unaweza kutoa. Nakulilia nikijua kwamba wewe pekee ndiwe mwenye uwezo wa kuweka huru, kuponya na kurejesha. Roho Mtakatifu, tusaidie kuelewa kwamba mpendwa wetu ameenda kuishi maisha ya milele, ambapo hakuna maumivu, huzuni wala magonjwa. Ututie nguvu kwa kuondokewa na mtu muhimu kwetu, teremsha faraja yako juu yao, na zaidi ya yote, waweze kuhifadhi mioyoni mwao tumaini la kukutana tena, kwamba sio kwaheri, bali ni tutaonana baadaye. Kama neno lako linavyosema: "Mimi ndimi ufufuo na uzima; yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, ataishi." Katika jina la Yesu. Amina!
Tufuate:

Matangazo


Matangazo