Biblia Todo Logo
Mistari ya Biblia
- Matangazo -


MISTARI KUHUSU MAUMIVU NA UGUMU

MISTARI KUHUSU MAUMIVU NA UGUMU

Safari ya maisha ina mambo mengi, na wakati mwingine yanakuwa magumu sana. Kifo cha mpendwa, shida za kifedha, magonjwa... ni mengi sana yanayotupata, na inatubidi kuyapitia. Lakini jambo zuri ni kujua kwamba Mungu yuko pamoja nasi kila wakati na atatusaidia daima.

Katika Biblia, kuna mistari mizuri ambapo Mungu anatukumbusha kwamba hatatuacha, kwamba atakuwa pamoja nasi siku zote, kwamba tusihofu kwani yeye ndiye anayetupigania. Mungu anatupa moyo, na anafika kwa wakati wake mwafaka. Kwa msaada wa Mungu, utaendelea mbele ukiwa na imani kwake yeye mwenye uwezo wote, aliyetoa mwanawe mpendwa kwa ajili ya upendo wake kwako.


Zaburi 34:18

Mwenyezi-Mungu yu karibu na waliokufa moyo; huwaokoa wote waliokata tamaa kabisa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 11:28-30

Njoni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifungeni nira yangu, mkajifunze kwangu, maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtatulizwa rohoni mwenu. wamwulize: “Je, wewe ni yule anayekuja, au tumngoje mwingine?” Maana, nira niwapayo mimi ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 147:3

Anawaponya waliovunjika moyo; na kuwatibu majeraha yao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 41:10

Basi, usiogope, mimi nipo pamoja nawe. Usifadhaike, mimi ni Mungu wako. Nitakuimarisha na kukusaidia; nitakulinda kwa mkono wangu wa ushindi.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 5:7

Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 23:4

Nijapopita katika bonde la giza kuu la kifo, sitaogopa hatari yoyote, maana wewe ee Mwenyezi-Mungu u pamoja nami; gongo lako na fimbo yako vyanilinda.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 14:27

“Nawaachieni amani; nawapeni amani yangu. Siwapi nyinyi kama vile ulimwengu ufanyavyo. Msiwe na wasiwasi, wala msifadhaike.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 4:6-7

Msiwe na wasiwasi juu ya kitu chochote, ila kwa kila hali, mwombeni Mungu katika sala juu ya mahitaji yenu, kwa shukrani. Nayo amani ya Mungu ipitayo akili zote za watu italinda salama mioyo na akili zenu katika kuungana na Kristo Yesu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 46:1

Mungu ni kimbilio letu na nguvu yetu; yeye ni msaada wetu daima wakati wa taabu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 55:22

Mwachie Mwenyezi-Mungu mzigo wako, naye atakutegemeza; kamwe hamwachi mwadilifu ashindwe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:18

Naona kuwa mateso ya wakati huu wa sasa si kitu kamwe kama tukiyalinganisha na ule utukufu utakaodhihirishwa kwetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 1:3-4

Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba mwenye huruma na Mungu mwenye kuleta faraja yote. Yeye hutufariji sisi katika taabu zetu zote, ili nasi tupate kuwafariji wengine katika kila taabu kwa faraja hiyohiyo tunayopokea kutoka kwa Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 16:33

Nimewaambieni mambo haya ili mpate kuwa na amani katika kuungana nami. Ulimwenguni mtapata masumbuko; lakini jipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu!”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 62:1-2

Namngojea Mungu peke yake kwa utulivu, kwake watoka wokovu wangu. Msitegemee dhuluma, msijisifie mali ya wizi; kama mali zikiongezeka, msizitegemee. Mungu ametamka mara moja, nami nimesikia tena na tena: Kwamba enzi ni mali yake Mungu; naam, nazo fadhili ni zake Bwana; humlipa kila mtu kadiri ya matendo yake. Yeye peke yake ndiye mwamba na wokovu wangu, yeye ni ngome yangu, sitatikisika.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 56:8

Wewe wakujua kusukwasukwa kwangu; waweka kumbukumbu ya machozi yangu yote. Je, yote si yamo kitabuni mwako?

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 53:4

Hata hivyo alivumilia majonzi yetu, na kubeba huzuni zetu. Sisi tulifikiri amepata adhabu, amepigwa na Mungu na kuteswa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 15:13

Basi, Mungu aliye msingi wa matumaini, awajazeni furaha yote na amani kutokana na imani yenu; tumaini lenu lipate kuongezeka kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 42:11

Mbona nasononeka hivyo moyoni? Kwa nini nahangaika hivyo? Nitamtumainia Mungu, maana nitamsifu tena Mungu, aliye msaada wangu na Mungu wangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 43:2

Mkipita katika mafuriko, mimi nitakuwa pamoja nanyi; mkipita katika mito, haitawashinda nguvu. Mkitembea katika moto, hamtaunguzwa; mwali wa moto hautawaunguza.

Sura   |  Matoleo Nakili
Maombolezo 3:22-23

Kwamba fadhili za Mwenyezi-Mungu hazikomi, huruma zake hazina mwisho. Kila kunapokucha ni mpya kabisa, uaminifu wake ni mkuu mno.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:50

Hata niwapo taabuni napata kitulizo, maana ahadi yako yanipa uhai.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:28

Tunajua kwamba, katika mambo yote, Mungu hufanya kazi na kuifanikisha pamoja na wote wampendao, yaani wale aliowaita kadiri ya kusudi lake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 27:14

Mtegemee Mwenyezi-Mungu! Uwe na moyo, usikate tamaa! Naam, mtegemee Mwenyezi-Mungu!

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 4:15-16

Huyu Kuhani Mkuu wetu anaelewa kabisa unyonge wetu; yeye mwenyewe alijaribiwa kama sisi kwa kila namna lakini hakutenda dhambi. Basi, na tukikaribie bila hofu kiti cha enzi cha Mungu mwenye neema, tupokee huruma na neema ya kutusaidia wakati wa shida.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 40:29-31

Yeye huwapa uwezo walio hafifu, wanyonge huwapa nguvu. Sauti ya mtu anaita jangwani: “Mtayarishieni Mwenyezi-Mungu njia, nyosheni barabara kuu kwa ajili ya Mungu wetu. Hata vijana watafifia na kulegea; naam, wataanguka kwa uchovu. Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu, watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mabawa kama tai; watakimbia bila kuchoka; watatembea bila kulegea.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 25:16-17

Unielekee, ee Mungu, unionee huruma, maana mimi ni mpweke na mnyonge. Uniondolee mahangaiko ya moyoni mwangu; unitoe katika mashaka yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 147:11

lakini hupendezwa na watu wamchao, watu wanaotegemea fadhili zake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 13:5

Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema: “Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa.”

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 10:13

Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 91:1-2

Anayekaa chini ya ulinzi wa Mungu Mkuu, anayeishi chini ya kivuli cha Mungu Mwenye Nguvu, Kwa hiyo, hutapatwa na maafa yoyote; nyumba yako haitakaribiwa na baa lolote. Maana Mungu atawaamuru malaika zake, wakulinde popote uendapo. Watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe. Utakanyaga simba na nyoka, utawaponda wana simba na majoka. Mungu asema: “Nitamwokoa yule anipendaye; nitamlinda anayenitambua! Akiniita, mimi nitamwitikia; akiwa taabuni nitakuwa naye; nitamwokoa na kumpa heshima. Nitamridhisha kwa maisha marefu, nitamjalia wokovu wangu.” ataweza kumwambia Mwenyezi-Mungu: “Wewe ni kimbilio langu na ngome yangu; Mungu wangu, ninayekutumainia!”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 12:12

Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida, na kusali daima.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:105

Neno lako ni taa ya kuniongoza, na mwanga katika njia yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 1:6-7

Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka, majaribio ambayo shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe, ambayo huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu, ambayo ni ya thamani kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate kuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 103:1-5

Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu; nafsi yangu yote ilisifu jina lake takatifu! Yeye hatuadhibu kama tunavyostahili; hatulipizi kadiri ya uovu wetu. Kama vile anga lilivyo juu mbali na dunia, ndivyo ulivyo mwingi wema wake kwa watu wanaomcha. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo azitengavyo dhambi zetu mbali nasi. Kama vile baba amhurumiavyo mwanawe, ndivyo Mwenyezi-Mungu awahurumiavyo wote wamchao. Mungu ajua mfumo wa nafsi zetu; ajua kwamba sisi ni mavumbi. Walakini binadamu, maisha yake ni kama nyasi tu; huchanua kama ua shambani: Upepo huvuma juu yake nalo latoweka; na mahali lilipokuwa hapaonekani tena. Lakini fadhili za Mwenyezi-Mungu hudumu milele, kwa wale wote wanaomheshimu; na wema wake wadumu vizazi vyote, kwa wote wanaozingatia agano lake, wanaokumbuka kutii amri zake. Mwenyezi-Mungu ameweka kiti chake cha enzi mbinguni; yeye anatawala juu ya vitu vyote. Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu! Usisahau kamwe wema wake wote. Enyi malaika wakuu, msifuni Mwenyezi-Mungu; mnaotimiza amri zake na kutekeleza neno lake! Enyi jeshi lote la mbinguni, msifuni Mwenyezi-Mungu; enyi watumishi wake mnaotekeleza matakwa yake! Msifuni Mwenyezi-Mungu enyi viumbe vyake vyote; msifuni popote mlipo katika milki yake. Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu! Ndiye anayenisamehe uovu wangu wote, na kuniponya magonjwa yote. Ndiye aniokoaye kutoka kifoni, na kunijalia rehema na fadhili zake. Ndiye anayeniridhisha mema maisha yangu yote, hata nabaki kijana mwenye nguvu kama tai.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 57:15

Hivi ndivyo asemavyo Mungu aliye juu kabisa, aishiye milele na ambaye jina lake ni “Mtakatifu”: “Mimi nakaa huko juu, mahali patakatifu, nakaa pia na wenye majuto na wanyenyekevu. Mimi nitawatia moyo walio wanyenyekevu na kuwapa nguvu wenye majuto.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 5:3-5

Naam, si hayo tu, bali tunafurahi pia katika taabu tukijua kwamba taabu huleta saburi, nayo saburi huleta uthabiti, na uthabiti huleta tumaini. Tumaini hilo haliwezi kutuhadaa, maana Mungu amekwisha mimina mioyoni mwetu upendo wake kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetujalia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 40:1-2

Nilimngojea Mwenyezi-Mungu kwa uvumilivu, akanielekea na kukisikia kilio changu. Sikuuficha moyoni mwangu ukombozi ulionijalia, nimetangaza daima kuwa wewe ni mwokozi mwaminifu; sikulificha kusanyiko kubwa la watu fadhili zako na uaminifu wako. Ee Mwenyezi-Mungu, usininyime huruma yako! Fadhili zako na uaminifu wako vinihifadhi daima. Maafa yasiyohesabika yanizunguka, maovu yangu yanikaba hata siwezi kuona; ni mengi kuliko nywele kichwani mwangu, nami nimevunjika moyo. Upende ee Mwenyezi-Mungu kuniokoa; ee Mwenyezi-Mungu, uje haraka kunisaidia. Wanaonuia kuniangamiza, na waaibike na kufedheheka! Hao wanaotamani niumie, na warudi nyuma na kuaibika! Hao wanaonisimanga, na wapumbazike kwa kushindwa kwao! Lakini wote wale wanaokutafuta wafurahi na kushangilia kwa sababu yako. Wapendao wokovu wako, waseme daima: “Mwenyezi-Mungu ni Mkuu!” Mimi ni maskini na fukara, ee Bwana; lakini ee Bwana wewe wanikumbuka. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu; uje, ee Mungu wangu, usikawie! Aliniondoa katika shimo la hatari, alinitoa katika matope ya dimbwi, akanisimamisha salama juu ya mwamba, na kuziimarisha hatua zangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 25:8

Bwana Mungu atakiangamiza kifo milele! Atayafuta machozi katika nyuso za watu wote na kuwaondolea watu wake aibu duniani kote. Bwana Mwenyezi-Mungu ametamka.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 4:16-18

Kwa sababu hiyo hatufi moyo; na hata kama maumbile yetu ya nje yataoza, lakini kwa ndani tunafanywa wapya siku kwa siku. Taabu tunayopata ni kidogo, tena ya muda tu; lakini itatupatia utukufu upitao matazamio yote, utukufu ambao hauna mwisho. Hivyo tunatazamia kwa makini si vitu vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Maana vinavyoonekana ni vya muda tu; lakini vile visivyoonekana ni vya milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 86:17

Unioneshe ishara ya wema wako, ee Mwenyezi-Mungu, ili wale wanaonichukia waaibike, waonapo umenisaidia na kunifariji.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:31-32

Kutokana na hayo, tuseme nini zaidi? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, nani awezaye kutupinga? Mungu hakumhurumia hata Mwanae wa pekee, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote. Ikiwa amefanya hivyo, je, hatatujalia pia mema yote?

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 126:5-6

Wanaopanda kwa machozi, watavuna kwa shangwe. Wanaokwenda kupanda mbegu wakilia, watarudi kwa furaha wakichukua mavuno.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 3:5-6

Mtumaini Mwenyezi-Mungu kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe. Umtambue Mungu katika kila ufanyalo, naye atazinyosha njia zako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 54:10

Milima yaweza kutoweka, vilima vyaweza kuondolewa, lakini fadhili zangu hazitakuondoka, agano langu la amani halitaondolewa. Mimi Mwenyezi-Mungu nikuhurumiaye nimesema.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 31:24

Muwe hodari na kupiga moyo konde, enyi nyote mnaomtumainia Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 15:5

“Mimi ni mzabibu, nanyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami nikiwa ndani yake, huyo huzaa matunda mengi, maana bila mimi hamwezi kufanya chochote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 71:20-21

Umenifanya nione taabu nyingi ngumu, lakini utanirudishia tena uhai, wewe utaniinua tena kutoka huko chini. Utaniongezea heshima yangu, na kunifariji tena.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 61:1-2

Bwana Mwenyezi-Mungu amenijaza roho yake, maana Mwenyezi-Mungu ameniweka wakfu, akanituma niwaletee wanaokandamizwa habari njema, niwatibu waliovunjika moyo, niwatangazie mateka kwamba watapata uhuru, na wafungwa kwamba watafunguliwa. Nitafurahi sana kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu, nafsi yangu itashangilia kwa sababu ya Mungu wangu. Maana amenivika vazi la wokovu, amenivalisha vazi la uadilifu, kama bwana arusi ajipambavyo kwa shada la maua, kama bibi arusi ajipambavyo kwa johari zake. Hivyo, kama vile ardhi ioteshavyo mimea, na shamba lichipushavyo mbegu zilizopandwa humo, Mwenyezi-Mungu atasababisha uadilifu na sifa kuchomoza mbele ya mataifa yote. Amenituma niutangaze mwaka wake wa neema, na siku ya Mungu wetu ya kulipiza kisasi; niwafariji wote wanaoomboleza;

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 4:13

Naweza kuikabili kila hali kwani Kristo hunipa nguvu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 14:18

“Sitawaacha nyinyi yatima; nitakuja tena kwenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 91:14-15

Mungu asema: “Nitamwokoa yule anipendaye; nitamlinda anayenitambua! Akiniita, mimi nitamwitikia; akiwa taabuni nitakuwa naye; nitamwokoa na kumpa heshima.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 11:1

Kuwa na imani ni kuwa na hakika ya mambo tunayotumainia; kusadiki kabisa mambo tusiyoyaona.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:1

Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu kwa wale ambao katika maisha yao wameungana na Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 118:6

Mwenyezi-Mungu yuko nami, siogopi kitu; binadamu ataweza kunifanya nini?

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:38-39

Maana ninajua hakika kwamba hakuna kitu kiwezacho kututenganisha na upendo wake: Wala kifo, wala uhai; wala malaika au nguvu nyingine za mbinguni; wala yanayotokea sasa, wala yatakayotokea baadaye; wala mamlaka; wala ulimwengu wa juu, wala wa chini kabisa. Hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 34:4

Nilimwomba Mwenyezi-Mungu naye akanijibu, na kuniondoa katika hofu zangu zote.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 3:14

Lakini, hata kama itawapasa kuteseka kwa sababu ya kutenda mema, basi, mna heri. Msimwogope mtu yeyote, wala msikubali kutiwa katika wasiwasi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 40:1

Mungu wenu asema: “Wafarijini watu wangu, nendeni mkawafariji.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 33:20-21

Mioyo yetu yamtumainia Mwenyezi-Mungu. Yeye ni msaada wetu na ngao yetu. Naam twafurahi kwa sababu yake; tuna matumaini katika jina lake takatifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 3:20

Kwa maana, hata kama dhamiri zetu zatuhukumu, twajua kwamba Mungu ni mkuu kuliko dhamiri, na kwamba yeye ajua kila kitu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 27:5

Siku ya taabu atanificha bandani mwake; atanificha katika hema lake, na kunisalimisha juu ya mwamba.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 29:11

Maana, mimi Mwenyezi-Mungu ninajua mambo niliyowapangia. Nimewapangieni mema na si mabaya, ili mpate kuwa na tumaini la baadaye.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 56:3-4

Ee Mungu Mkuu, hofu inaponishika, mimi nakutumainia wewe. Namtumainia Mungu na kusifu neno lake; namtumainia Mungu, wala siogopi. Binadamu dhaifu atanifanya nini?

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 12:2

Mungu ndiye mwenye kuniokoa, nitamtegemea yeye, wala sitaogopa; Mwenyezi-Mungu hunijalia nguvu; yeye mwenyewe ndiye aniokoaye.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 6:37

Wote anaonipa Baba watakuja kwangu; nami kamwe sitamtupa nje yeyote anayekuja kwangu,

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 28:7

Mwenyezi-Mungu ndiye nguvu yangu na ngao yangu; tegemeo la moyo wangu limo kwake. Amenisaidia nami nikashangilia kwa moyo; kwa wimbo wangu ninamshukuru.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:35-37

Ni nani awezaye kututenga na upendo wa Kristo? Je, ni taabu, au dhiki, au mateso, au njaa, au ukosefu wa nguo, au hatari, au kifo? Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Kwa ajili yako, twakikabili kifo kutwa kucha; tunatendewa kama kondoo wa kuchinjwa.” Lakini, katika mambo haya yote, tumepata ushindi mkubwa kwa msaada wake yeye aliyetupenda.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:23-24

Mwenyezi-Mungu huziongoza nyayo za mtu, humlinda yule ampendezaye. Ajapoanguka, haanguki akabaki chini, kwa sababu Mwenyezi-Mungu humtegemeza.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 4:13-14

Ndugu, twataka mjue ukweli kuhusu wale ambao wamekwisha fariki dunia, ili msipatwe na huzuni kama watu wengine wasio na matumaini. Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 49:15-16

Lakini Mwenyezi-Mungu asema: “Je, mama aweza kumsahau mwanawe anayenyonya, asimwonee huruma mtoto wa tumbo lake? Hata kama mama aweza kumsahau mwanawe, mimi kamwe sitakusahau. Nimekuchora katika viganja vyangu; kuta zako naziona daima mbele yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 10:23

Tuzingatie kabisa tumaini letu tunalokiri, maana Mungu aliyefanya ahadi zake ni mwaminifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 1:6

Basi, nina hakika kwamba Mungu aliyeanza kazi hii njema ndani yenu, ataiendeleza mpaka ikamilike katika siku ile ya Kristo Yesu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 9:12

Mungu hulipiza kisasi kwa umwagaji damu; kamwe hasahau kilio cha wanaoonewa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 18:10

Jina la Mwenyezi-Mungu ni mnara imara; mwadilifu huukimbilia akawa salama.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 116:1-2

Nampenda Mwenyezi-Mungu, kwa maana anisikia, maana amesikia kilio cha ombi langu. Nilikuwa na imani hata niliposema: “Mimi nimetaabika mno.” Hata nilisema kwa hofu yangu: “Binadamu wote hawaaminiki!” Nimrudishie nini Mwenyezi-Mungu, kwa ukarimu wote alionitendea? Nitamtolea tambiko ya divai kwa kunikomboa, nitaomba kwa jina lake Mwenyezi-Mungu. Nitamtimizia Mwenyezi-Mungu nadhiri zangu, mbele ya watu wake wote. Kifo cha waaminifu wake Mwenyezi-Mungu si jambo dogo mbele yake. Ee Mwenyezi-Mungu, mimi ni mtumishi wako; ni mtumishi wako, mtoto wa mjakazi wako; umenifungulia vifungo vyangu. Nitakutolea tambiko za shukrani, na kukupa heshima zangu. Nitakutimizia ahadi zangu, ee Mwenyezi-Mungu mbele ya watu wako wote, waliokusanyika hekaluni mwako, katikati ya Yerusalemu. Msifuni Mwenyezi-Mungu! Yeye amenitegea sikio, hivyo nitamwomba muda wote niishio.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 32:2

Kila mmoja atakuwa kama mahali pa kujikinga na upepo, kama mahali pa kujificha wakati wa tufani. Watakuwa kama vijito vya maji katika nchi kame, kama kivuli cha mwamba mkubwa jangwani.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 42:8

Mwenyezi-Mungu atanijalia fadhili zake mchana; nami nimwimbie wimbo wa sifa usiku, nimwombe Mungu anipaye uhai.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 5:8

Lakini Mungu amethibitisha kwamba anatupenda, maana wakati tulipokuwa bado wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 5:17

Mtu yeyote akiungana na Kristo huwa kiumbe kipya, mambo ya kale yamepita, hali mpya imefika.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 55:16-17

Lakini mimi namlilia Mungu, naye Mwenyezi-Mungu ataniokoa. Jioni, asubuhi na adhuhuri, nalalama na kulia, naye ataisikia sauti yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 6:19

Tunalo tumaini hilo kama nanga ya maisha yetu. Tumaini hilo lapenya mpaka mahali patakatifu mbinguni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 14:1

Yesu aliwaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 16:8

Namweka Mwenyezi-Mungu mbele yangu daima; yuko pamoja nami, wala sitatikisika.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 94:19

Mahangaiko ya moyo wangu yanapozidi, wewe wanifariji na kunifurahisha.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 30:5

Hasira yake hudumu kitambo kidogo, wema wake hudumu milele. Kilio chaweza kuwapo hata usiku, lakini asubuhi huja furaha.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Timotheo 1:7

Kwa maana Roho tuliyepewa na Mungu si wa kutufanya tuwe waoga; sivyo, ila ni Roho wa kutujalia upendo na nidhamu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 31:7

Nitashangilia na kufurahia fadhili zako, maana wewe waiona dhiki yangu, wajua na taabu ya nafsi yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 14:8

maana tukiishi twaishi kwa ajili ya Bwana; tukifa, tunakufa kwa ajili ya Bwana. Basi, kama tukiishi au tukifa, sisi ni mali yake Bwana.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 41:13

Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ndimi ninayetegemeza mkono wako. Mimi ndimi ninayekuambia: ‘Usiogope, nitakusaidia.’”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 23:6

Kweli wema wako na fadhili zako zitakuwa pamoja nami, siku zote za maisha yangu; nami nitakaa nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:4

Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:26

Hali kadhalika, naye Roho anatusaidia katika udhaifu wetu. Maana hatujui inavyotupasa kuomba; lakini Roho mwenyewe anatuombea kwa Mungu kwa mlio wa huzuni usioelezeka.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 63:7-8

maana wewe umenisaidia daima. Kivulini mwa mabawa yako nitashangilia. Roho yangu inaambatana nawe kabisa, mkono wako wa kulia wanitegemeza.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 3:20-21

Kwake yeye ambaye kwa nguvu yake ifanyayo kazi ndani yetu aweza kufanya mambo makuu zaidi ya yale tuwezayo kuomba au kufikiria; kwake Mungu uwe utukufu katika kanisa na katika Kristo Yesu, nyakati zote, milele na milele! Amina.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 3:3

Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu u ngao yangu kila upande; kwako napata fahari na ushindi wangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 1:9

Mungu ni mwaminifu; yeye aliwaita nyinyi muwe na umoja na Mwanae Yesu Kristo Bwana wetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 8:12

Yesu alipozungumza nao tena, aliwaambia, “Mimi ndimi mwanga wa ulimwengu. Anayenifuata mimi hatembei kamwe gizani, bali atakuwa na mwanga wa uhai.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 40:3

Alinifundisha wimbo mpya, wimbo wa sifa kwa Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa, na kumtumainia Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 46:10

Asema: “Nyamazeni na kujua kuwa mimi ni Mungu! Mimi natukuka katika mataifa yote; mimi natukuzwa ulimwenguni kote!”

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 2:9

Lakini nyinyi ni ukoo mteule, makuhani wa Mfalme, taifa takatifu; watu wake Mungu mwenyewe, mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya Mungu aliyewaiteni kutoka gizani, akawaingizeni katika mwanga wake mkuu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 2:13

kwani Mungu ndiye afanyaye kazi daima ndani yenu, na kuwapeni uwezo wa kutaka na kutekeleza mambo yanayopatana na mpango wake mwenyewe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 91:4

Atakufunika kwa mabawa yake, utapata usalama kwake; mkono wake utakulinda na kukukinga.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 33:2

Ee Mwenyezi-Mungu, utuonee huruma, kwako tumeliweka tumaini letu. Uwe kinga yetu kila siku, wokovu wetu wakati wa taabu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 42:5-6

Mbona nasononeka hivyo moyoni? Kwa nini nahangaika hivyo ndani mwangu? Nitamtumainia Mungu, maana nitamsifu tena yeye aliye msaada wangu na Mungu wangu. Nimesongwa na huzuni moyoni mwangu, kwa hiyo ninakukumbuka wewe, ee Mungu, kutoka katika eneo la Yordani, kutoka mlima Hermoni na Mizari.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 10:13

Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kila mtu atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa.”

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wathesalonike 3:16

Bwana mwenyewe ambaye ndiye chanzo cha amani, awajalieni amani siku zote kwa kila namna. Bwana awe nanyi nyote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 63:1-3

Ee Mungu, wewe u Mungu wangu, nami nakutafuta kwa moyo; roho yangu inakutamani kama mtu mwenye kiu; nina kiu kama nchi kavu isiyo na maji. Watauawa kwa upanga, watakuwa chakula cha mbweha. Lakini mfalme atafurahi kwa sababu ya Mungu; wanaoahidi kwa jina la Mungu watamsifu, lakini vinywa vya waongo vitafumbwa. Nimetaka kukuona patakatifuni pako, niione nguvu yako na utukufu wako. Fadhili zako ni bora kuliko maisha, nami nitakusifu kwa mdomo wangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 17:13

Basi, sasa naja kwako, na nimesema mambo haya ulimwenguni, ili waweze kushiriki kikamilifu furaha yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 5:10

Lakini mkisha teseka muda mfupi, Mungu aliye asili ya neema yote na ambaye anawaiteni kuushiriki utukufu wake wa milele katika kuungana na Kristo, yeye mwenyewe atawakamilisheni na kuwapeni uthabiti, nguvu na msingi imara.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 94:22

Lakini Mwenyezi-Mungu ni ngome yangu; Mungu wangu ni mwamba wa usalama wangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:15-16

Kwa maana, hamkumpokea Roho mwenye kuwafanya nyinyi watumwa tena na kuwatia hofu, bali mmempokea Roho mwenye kuwafanya nyinyi watoto wa Mungu, na kwa Roho huyo, sisi tunamwita Mungu, “Aba,” yaani “Baba!” Naye Roho mwenyewe anathibitisha na roho zetu kwamba sisi ni watoto wa Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 12:2-3

Tumwelekee Yesu ambaye ndiye aliyeianzisha imani yetu na ambaye ataikamilisha. Kwa ajili ya furaha iliyokuwa inamngojea, yeye alivumilia kifo msalabani, bila kuijali aibu yake, na sasa anaketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu. kwani hawakuweza kustahimili amri iliyotolewa: “Atakayegusa mlima huu, hata kama ni mnyama, atapigwa mawe.” Hayo yote yalionekana ya kutisha mno, hata Mose akasema, “Naogopa na kutetemeka.” Lakini nyinyi mmefika katika mlima wa Siyoni, kwenye mji wa Mungu aliye hai. Mmefika Yerusalemu, mji wa mbinguni, ambapo wamekusanyika malaika kwa maelfu. Mmefika kwenye kusanyiko kubwa la wazaliwa wa kwanza wa Mungu, ambao majina yao yameandikwa mbinguni. Mnasimama mbele ya Mungu aliye hakimu wa wote, na mbele ya roho za watu waadilifu waliofanywa wakamilifu. Mmefika kwa Yesu ambaye ni mpatanishi katika agano jipya, na ambaye damu yake iliyomwagika inasema mambo mema kuliko ile ya Abeli. Basi, jihadharini msije mkakataa kumsikiliza huyo anayesema nanyi. Kama wale waliokataa kumsikiliza yule aliyewaonya hapa duniani hawakuokoka, sisi tutawezaje kuokoka kama tukikataa kumsikiliza yule anayetuonya kutoka mbinguni? Wakati ule sauti ilitetemesha nchi, lakini sasa ameahidi: “Nitatetemesha nchi tena, lakini si nchi tu bali pia mbingu.” Neno hili: “Tena” linatuonesha kwamba vitu vyote vilivyoumbwa vitatetemeshwa na kutoweka ili vibaki vile visivyotetemeshwa. Sisi basi, na tushukuru, kwani tunapokea ufalme usiotikisika. Tuwe na shukrani na kumwabudu Mungu kwa namna itakayompendeza, kwa ibada na hofu; maana Mungu wetu kweli ni moto mkali unaoteketeza. Fikirini juu ya mambo yaliyompata Yesu, jinsi alivyostahimili upinzani mkubwa kwa watu wenye dhambi. Basi, msife moyo, wala msikate tamaa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 4:8-9

Hatimaye, ndugu zangu, zingatieni mambo mema na yanayostahili kusifiwa; mambo ya kweli na bora; mambo ya haki, safi, ya kupendeza na ya heshima. Tekelezeni yale mliyojifunza na kupokea kutoka kwangu; mambo mliyosikia nimesema na kuona nimeyatenda. Naye Mungu anayetujalia amani atakuwa pamoja nanyi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:143

Taabu na huzuni vimenipata, lakini amri zako ndizo furaha yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:5

Mkabidhi Mwenyezi-Mungu maisha yako; mtumainie yeye naye atafanya kitu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 4:16

Basi, sisi tunajua na tunaamini upendo alio nao Mungu kwetu sisi. Mungu ni upendo, na kila mtu aishiye katika upendo, anaishi katika muungano na Mungu, na Mungu anaishi katika muungano naye.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 43:1-2

Mwenyezi-Mungu aliyewaumba enyi watu wa Yakobo, yeye aliyewafanya enyi watu wa Israeli, asema: “Msiogope, maana mimi nimewakomboa; nimewaita kwa jina nanyi ni wangu. Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nyinyi Waisraeli ni mashahidi wangu; niliwachagua muwe watumishi wangu, mpate kunijua na kuniamini, kwamba ndimi peke yangu Mungu. Kabla yangu hajapata kuwapo mungu mwingine, wala hatakuwapo mungu mwingine. “Mimi peke yangu ndimi Mwenyezi-Mungu, hakuna mkombozi mwingine ila mimi. Nilitangaza yale ambayo yangetukia, kisha nikaja na kuwakomboa. Hakuna mungu mwingine aliyewahi kufanya hivyo, nanyi ni mashahidi wangu. Mimi ni Mungu na nitakuwa Mungu daima. Hakuna awezaye kuiepa nguvu yangu; hakuna awezaye kupinga ninayofanya.” Mwenyezi-Mungu, Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi: “Kwa ajili yenu nitatuma jeshi Babuloni. Nitayavunjilia mbali malango ya mji wake, na kelele za hao Wakaldayo zitageuka maombolezo. Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wenu; Mimi ndimi Muumba wa Israeli, Mfalme wenu.” Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wakati mmoja nilifanya barabara baharini nikaweka njia kati ya mawimbi makubwa. Nililipiga jeshi lenye nguvu, jeshi la magari na farasi wa vita, askari na mashujaa wa vita. Niliwaangusha chini wasiweze kuinuka tena, niliwakomesha na kuwazima kama utambi wa taa. Sasa nasema: ‘Msiyanganganie mambo yaliyopita, wala msifikirie vitu vya zamani. Tazameni, mimi ninafanya kitu kipya. Kinafanyika sasa hivi, nanyi mtaweza kukiona. Nitafanya njia nyikani, na kububujisha mito jangwani. Mkipita katika mafuriko, mimi nitakuwa pamoja nanyi; mkipita katika mito, haitawashinda nguvu. Mkitembea katika moto, hamtaunguzwa; mwali wa moto hautawaunguza.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 145:18

Mwenyezi-Mungu yuko karibu na wote wanaomwomba, wote wanaomwomba kwa moyo mnyofu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 31:13

Ndipo wasichana wao watafurahi na kucheza, vijana na wazee watashangilia kwa furaha. Nitageuza maombolezo yao kuwa furaha, nitawafariji na kuwapa furaha badala ya huzuni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 18:2

Mwenyezi-Mungu ni mwamba wangu, ngome yangu na mkombozi wangu; Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia usalama; ngao yangu, nguvu za wokovu wangu na ngome yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 15:4

Maana, yote yaliyoandikwa yameandikwa kwa ajili ya kutufundisha sisi ili kutokana na saburi na faraja tupewayo na hayo Maandiko Matakatifu tupate kuwa na matumaini.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 9:8

Mungu anaweza kuwapeni nyinyi zaidi ya yale mnayoyahitaji, mpate daima kuwa na kila kitu mnachohitaji, na hivyo mzidi kusaidia katika kila kazi njema.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 139:1-3

Ee Mwenyezi-Mungu, wewe umenichunguza; wewe wanijua mpaka ndani. hata huko upo kuniongoza; mkono wako wa kulia utanitegemeza. Kama ningeliomba giza linifunike, giza linizunguke badala ya mwanga, kwako giza si giza hata kidogo, na usiku wangaa kama mchana; kwako giza na mwanga ni mamoja. Wewe umeniumba, mwili wangu wote; ulinitengeneza tumboni mwa mama yangu. Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu, matendo yako ni ya ajabu; wewe wanijua kabisakabisa. Umbo langu halikufichika kwako nilipotungwa kwa siri na ustadi ndani ya dunia. Wewe uliniona hata kabla sijazaliwa, uliandika kila kitu kitabuni mwako; siku zangu zote ulizipanga, hata kabla ya kuweko ile ya kwanza. Ee Mungu, mawazo yako ni makuu mno; hayawezi kabisa kuhesabika. Ningeyahesabu yangekuwa mengi kuliko mchanga. Niamkapo, bado nipo pamoja nawe. Laiti, ee Mungu, ungewaua watu waovu! Laiti watu wauaji wangeondoka kwangu! Nikiketi au nikisimama, wewe wajua; wajua kutoka mbali kila kitu ninachofikiria. Wanasema vibaya juu yako; wanasema maovu juu ya jina lako! Ee Mwenyezi-Mungu, nawachukia wanaokuchukia; nawadharau sana wale wanaokuasi! Maadui zako ni maadui zangu; ninawachukia kabisakabisa. Unichunguze, ee Mungu, unijue moyo wangu, unipime, uyajue mawazo yangu. Uangalie kama mwenendo wangu ni mbaya, uniongoze katika njia ya milele. Watambua nikienda au nikipumzika; wewe wazijua shughuli zangu zote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 4:11-12

Sisemi hivyo sasa kwa sababu nahitaji kitu; maana nimejifunza kuridhika na vitu nilivyo navyo. Najua hali ya kutokuwa na vitu na hali ya kuwa na vingi. Nimejizoeza kuridhika katika kila hali na mahali; niwe nina cha kutosha au nina njaa; iwe nina ziada au nimepungukiwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 91:5-6

Huna haja ya kuogopa vitisho vya usiku, wala shambulio la ghafla mchana; huna haja ya kuogopa baa lizukalo usiku, wala maafa yanayotokea mchana.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 30:15

Bwana Mungu, Mtakatifu wa Israeli, asema: “Mkinirudia na kutulia mtaokolewa; kwa utulivu na kunitumainia mtapata nguvu.” Lakini nyinyi hamkutaka.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 18:6

Katika taabu yangu nilimwita Mwenyezi-Mungu, nilimlilia Mungu wangu anisaidie. Aliisikia sauti yangu hekaluni mwake; kilio changu kilimfikia masikioni mwake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:32

Mungu hakumhurumia hata Mwanae wa pekee, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote. Ikiwa amefanya hivyo, je, hatatujalia pia mema yote?

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 26:3-4

Ee Mungu, wawaweka katika amani walio thabiti, wawaweka katika amani kwa kuwa wanakutegemea. Mtumaini Mwenyezi-Mungu siku zote kwa maana yeye ni mwamba wa usalama milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 5:11-12

Lakini wafurahi wote wanaokimbilia usalama kwako, waimbe kwa shangwe daima. Uwalinde wanaolipenda jina lako, wapate kushangilia kwa sababu yako. Maana wewe Mwenyezi-Mungu wawabariki waadilifu; wawakinga kwa fadhili zako kama kwa ngao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 73:23-26

Hata hivyo niko daima nawe, ee Mungu! Wanishika mkono na kunitegemeza. Wewe waniongoza kwa mashauri yako; mwishowe utanipokea kwenye utukufu. Mbinguni, nani awezaye kunisaidia ila wewe? Na duniani hamna ninachotamani ila wewe! Hata nikikosa nguvu mwilini na rohoni, wewe, ee Mungu, u mwamba wangu; riziki yangu kuu ni wewe milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 5:11

Kwa hiyo farijianeni na kusaidiana nyinyi kwa nyinyi, kama mnavyofanya sasa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 62:5-6

Namngojea Mungu peke yake kwa utulivu; kwake naliweka tumaini langu. Yeye peke yake ndiye mwamba na wokovu wangu, yeye ni ngome yangu, sitatikisika.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:14-15

Wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni watoto wa Mungu. Kwa maana, hamkumpokea Roho mwenye kuwafanya nyinyi watumwa tena na kuwatia hofu, bali mmempokea Roho mwenye kuwafanya nyinyi watoto wa Mungu, na kwa Roho huyo, sisi tunamwita Mungu, “Aba,” yaani “Baba!”

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 12:9

Lakini akaniambia: “Neema yangu inatosha kwa ajili yako; maana uwezo wangu hukamilishwa zaidi katika udhaifu.” Basi, ni radhi kabisa kujivunia udhaifu wangu ili uwezo wake Kristo ukae juu yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 57:1

Unihurumie, ee Mungu, unihurumie, maana kwako nakimbilia usalama. Kivulini mwa mabawa yako nitakimbilia usalama, hata hapo dhoruba ya maangamizi itakapopita.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 20:1

Mwenyezi-Mungu akujibu uwapo taabuni; jina la Mungu wa Yakobo likulinde.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yohana 14:16-17

Nami nitamwomba Baba naye atawapeni Msaidizi mwingine, atakayekaa nanyi milele. Yeye ni Roho wa ukweli. Ulimwengu hauwezi kumpokea kwa sababu hauwezi kumwona wala kumjua. Lakini nyinyi mnamjua kwa sababu anabaki nanyi na yu ndani yenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 55:6

Mtafuteni Mwenyezi-Mungu wakati bado anapatikana, mwombeni msaada wakati yupo bado karibu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 30:11-12

Wewe umegeuza maombolezo langu kuwa ngoma ya furaha; umeniondolea huzuni yangu, ukanizungushia furaha. Mimi nitakusifu wala sitakaa kimya. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu nitakushukuru milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Mambo ya Nyakati 16:9

Mwenyezi-Mungu huuchunga kwa makini ulimwengu wote, ili kuwapa nguvu wale walio waaminifu kwake. Umetenda jambo la kipumbavu, kwa hiyo tangu sasa, utakuwa na vita kila mara.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 6:25-27

“Ndiyo maana nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula na kinywaji mnavyohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. Je, maisha ni chakula tu au zaidi? Na mwili, je, si zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa mwituni: Hawapandi, hawavuni, wala hawana ghala yoyote. Hata hivyo, Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, nyinyi si wa thamani kuliko hao? Ni nani miongoni mwenu kwa kuwa na wasiwasi sana anaweza kuuongeza muda wa maisha yake?

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 55:12

“Mtatoka Babuloni kwa furaha; mtaongozwa mwende kwa amani. Milima na vilima mbele yenu vitapaza sauti na kuimba, na miti yote mashambani itawapigia makofi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 9:13-14

Unirehemu, ee Mwenyezi-Mungu! Ona mateso ninayoteswa na wanaonichukia; wewe waninyakua kutoka nguvu za kifo, nisimulie sifa zako mbele ya watu wa Siyoni, nipate kushangilia kwa sababu umeniokoa.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Samueli 22:31-33

Anachofanya Mungu hakina dosari! Ahadi ya Mwenyezi-Mungu ni ya kuaminika; yeye ni ngao kwa wote wanaomkimbilia. “Nani aliye Mungu isipokuwa Mwenyezi-Mungu? Nani aliye mwamba wa usalama ila Mungu wetu? Mungu huyu ndiye kimbilio langu imara, na ameifanya njia yangu iwe salama.

Sura   |  Matoleo Nakili

Maombi kwa Mungu

Ee Bwana, wewe ndiwe Alfa na Omega! Baba, Muumba wa mbingu na nchi, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho. Ninakujia kupitia Bwana wangu Yesu Kristo, katika wakati huu wa uchungu, nakuomba unipe nguvu na uponye jeraha hili linalonisumbua. Linda moyo wangu usijae uchungu na chuki. Ee Bwana Yesu, ninajua uchungu huu ninaopitia utatumia kuponya wengine, kama vile sisi tumeponywa kupitia majeraha yako pale msalabani Kalvari. Neno lako linasema, “Waadilifu hulia, naye Bwana husikia; Huwaokoa na taabu zao zote. Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na huwaokoa wale waliopondeka roho.” Kwani wewe pekee ndiye huwapa nguvu wazimiao, na kuwazidishia nguvu wasio na nguvu. Asante Bwana, kwako utukufu na heshima. Katika jina la Yesu. Amina!
Tufuate:

Matangazo


Matangazo