Biblia Todo Logo
Mistari ya Biblia
- Matangazo -


Vikundi Vidogo

AYA ZA MKESHA

AYA ZA MKESHA

Rafiki, Biblia inatuonyesha matukio mengi yanayotendeka kabla ya alfajiri, matukio muhimu yaliyoandikwa na Roho Mtakatifu ili tujifunze nguvu kubwa ya vita vya kiroho wakati wa kesha. Mungu anatuita, anataka kutuonyesha kwamba kusali wakati wa mchana si sawa na kusali usiku, hasa alfajiri. Neno la Mungu linatuambia tusikilize kile roho zetu zinatuonyesha.

Waefeso 6:18 inasema, "Mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha katika hilo kwa uvumilivu wote na maombi kwa ajili ya watakatifu wote." Kesha ni kukaa macho usiku kucha (au sehemu ya usiku) tukimwomba Mungu. Pia inamaanisha kusimama linda usiku. Kwa maana pana, neno kesha linatukumbusha kwamba tunapaswa kuwa macho kiroho wakati huu ambapo dunia imelala gizani.

Tunapokuwa na shida, tunapaswa pia kufanya kesha ili kutafuta faraja ya Mungu. Maombolezo 2:19 inasema, "Ondoka, ulalamike usiku, mwanzo wa makesha; Mimina moyo wako kama maji mbele za Bwana; Nyosha mikono yako kwake."


Mathayo 26:41

Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho inataka lakini mwili ni dhaifu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 5:8

Muwe macho; kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi, huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mawindo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Marko 13:33

Muwe waangalifu na kesheni, maana hamjui wakati huo utafika lini.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 21:36

Muwe waangalifu basi, na salini daima ili muweze kupata nguvu ya kupita salama katika mambo haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele ya Mwana wa Mtu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 5:6

Basi, tusilale usingizi kama wengine; tunapaswa kukesha na kuwa na kiasi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 130:6

Ninamtumainia Mwenyezi-Mungu kuliko walinzi wanavyongojea pambazuko; kuliko walinzi wanavyongojea kuche asubuhi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 13:11

Zaidi ya hayo, nyinyi mnajua tumo katika wakati gani: Sasa ndio wakati wa kuamka usingizini; naam, wokovu wetu uko karibu zaidi sasa kuliko wakati ule tulipoanza kuamini.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 24:42

Basi, kesheni, kwa maana hamjui siku atakayokuja Bwana wenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 121:4

Kweli mlinzi wa Israeli hasinzii wala halali.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 16:13

Kesheni, simameni imara katika imani, muwe hodari na wenye nguvu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 12:37

Heri yao watumishi wale ambao bwana wao atakaporudi atawakuta wanakesha! Nawaambieni hakika, huyo bwana atajifunga mkanda kiunoni, atawaketisha mezani na kuwahudumia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 52:8

Sikiliza sauti ya walinzi wako; wanaimba pamoja kwa furaha, maana wanaona kwa macho yao wenyewe, kurudi kwa Mwenyezi-Mungu mjini Siyoni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:148

Nakaa macho usiku kucha, ili nitafakari juu ya maagizo yako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Marko 14:38

Kisha akawaambia, “Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho inataka, lakini mwili ni dhaifu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 16:8

Namweka Mwenyezi-Mungu mbele yangu daima; yuko pamoja nami, wala sitatikisika.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 4:23

Linda moyo wako kwa uangalifu wote, maana humo zatoka chemchemi za uhai.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 90:12

Utufundishe ufupi wa maisha yetu ili tuweze kuwa na hekima.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 13:17

Watiini viongozi wenu na kushika amri zao; wao huchunga roho zenu usiku na mchana, na watatoa ripoti ya utumishi wao mbele ya Mungu. Kama mkiwatii watafanya kazi zao kwa furaha, la sivyo, watazifanya kwa huzuni, na hiyo haitakuwa na faida kwenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 3:20

Lakini sisi ni raia wa mbinguni, na twatazamia kwa hamu kubwa Mwokozi aje kutoka mbinguni, Bwana Yesu Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 6:9

Basi, tusichoke kutenda mema; maana tusipolegea tutavuna mavuno kwa wakati wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 59:1

Ee Mungu wangu, uniokoe na maadui zangu; unikinge na hao wanaonishambulia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 56:10

Maana viongozi wao wote ni vipofu; wote hawana akili yoyote. Wote ni kama mbwa bubu wasiobweka, hulala tu na kuota ndoto, hupenda sana kusinzia!

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 25:13

Kisha Yesu akasema, “Kesheni basi, kwa maana hamjui siku wala saa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:7

Tulia mbele ya Mwenyezi-Mungu, mngojee kwa saburi; usihangaike juu ya wale wanaofanikiwa, watu wanaofaulu katika mipango yao mibaya.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 8:19

Viumbe vyote vinangojea kwa hamu Mungu awadhihirishe watoto wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Timotheo 4:5

Wewe, lakini, uwe macho katika kila hali; vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Habari Njema, timiza kikamilifu utumishi wako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:55

Usiku ninakukumbuka, ee Mwenyezi-Mungu, na kushika sheria yako.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 2:28

Naam, watoto, kaeni ndani yake kusudi wakati atakapotokea tuwe hodari bila kuwa na sababu ya kujificha kwa aibu siku ya kuja kwake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 12:38

Hata kama atarudi usiku wa manane au alfajiri na kuwakuta wanakesha, heri yao watumishi hao!

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 12:12

Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida, na kusali daima.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 3:12-13

Basi ndugu, jihadharini asije akawako yeyote miongoni mwenu aliye na moyo mbaya hivyo na asiyeamini hata kujitenga na Mungu aliye hai. Maadamu hiyo “Leo” inayosemwa katika Maandiko bado inatuhusu sisi, mnapaswa kusaidiana daima, ili mtu yeyote miongoni mwenu asidanganywe na dhambi na kuwa mkaidi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 104:23

Hapo naye binadamu huenda kwenye shughuli zake; na kufanya kazi zake mpaka jioni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 8:34

Heri mtu anayenisikiliza, anayekaa kila siku mlangoni pangu, anayekesha karibu na milango yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 86:5

Wewe, ee Bwana, u mwema na mwenye kusamehe; mwingi wa fadhili kwa wote wakuombao.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 6:12

Piga mbio kadiri uwezavyo katika shindano la mbio za imani, ukajipatie tuzo la uhai wa milele uliloitiwa wakati ulipokiri imani yako mbele ya mashahidi wengi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 26:3

Ee Mungu, wawaweka katika amani walio thabiti, wawaweka katika amani kwa kuwa wanakutegemea.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:16

Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 5:16

Basi, nasema hivi: Mwenendo wenu na uongozwe na Roho, nanyi hamtafuata tena tamaa za kidunia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 5:14

na kila kilichodhihirishwa huwa mwanga. Ndiyo maana Maandiko yasema: “Amka wewe uliyelala, fufuka kutoka kwa wafu, naye Kristo atakuangaza.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:37

Uniepushe, nisifuate mambo ya upuuzi; unioneshe njia yako, unipe uhai.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 22:46

Akawaambia, “Mbona mnalala? Amkeni msali, msije mkaingia katika kishawishi.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 15:13

Basi, Mungu aliye msingi wa matumaini, awajazeni furaha yote na amani kutokana na imani yenu; tumaini lenu lipate kuongezeka kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 15:58

Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 2:14-16

Fanyeni kila kitu bila kunungunika na bila ubishi, ili mpate kuwa watu safi, wasio na lawama, kama watoto wanyofu wa Mungu wanaoishi katika ulimwengu mbaya na uliopotoka. Mtangara kati yao kama nyota zinavyoliangaza anga, mkishika imara ujumbe wa uhai. Na hapo ndipo nami nitakapokuwa na sababu ya kujivunia katika siku ile ya Kristo, kwani itaonekana dhahiri kwamba bidii yangu na kazi yangu havikupotea bure.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 101:3

sitavumilia kamwe upuuzi. Nayachukia matendo ya watu wapotovu, mambo yao hayataambatana nami.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 52:1

Amka! Amka! Jipe nguvu zako ewe mji wa Siyoni! Jivike mavazi yako mazuri, ewe Yerusalemu, mji mtakatifu. Maana hawataingia tena kwako watu wasiotahiriwa na walio najisi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 7:24-25

“Kwa hiyo, kila mtu anayeyasikia maneno yangu na kuyazingatia, anafanana na mtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga nyumba hiyo. Lakini haikuanguka kwa sababu ilikuwa imejengwa juu ya mwamba.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 24:32-34

Nilitazama, nikawaza, mwishowe nikapata funzo: Lala tu kidogo; sinzia tu kidogo! Kunja mikono yako tu upumzike! Lakini kumbuka kwamba uwapo usingizini, umaskini utakuvamia kama mnyanganyi, ufukara kama mtu mwenye silaha.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 4:7

Mwisho wa vitu vyote umekaribia. Kwa hiyo mnapaswa kuwa na utaratibu na kukesha ili muweze kusali.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 10:24-25

Tujitahidi kushughulikiana kwa ajili ya kuongezeana bidii ya kupendana na kutenda mema. Tusiache ile desturi ya kukutana pamoja, kama vile wengine wanavyofanya. Bali tunapaswa kusaidiana kwani, kama mwonavyo, siku ile ya Bwana inakaribia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 18:1

Basi, Yesu aliwasimulia mfano kuonesha kwamba ni lazima kusali daima bila kukata tamaa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:105

Neno lako ni taa ya kuniongoza, na mwanga katika njia yangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 4:1

Wapenzi wangu, msimsadiki kila mtu asemaye kwamba ana Roho wa Mungu, bali chunguzeni kwa makini kama huyo mtu anaongozwa na Roho wa Mungu au la, maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 27:12

Mwenye busara huona hatari akajificha, lakini mjinga hujitokeza mbele akaumia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 62:1-2

Namngojea Mungu peke yake kwa utulivu, kwake watoka wokovu wangu. Msitegemee dhuluma, msijisifie mali ya wizi; kama mali zikiongezeka, msizitegemee. Mungu ametamka mara moja, nami nimesikia tena na tena: Kwamba enzi ni mali yake Mungu; naam, nazo fadhili ni zake Bwana; humlipa kila mtu kadiri ya matendo yake. Yeye peke yake ndiye mwamba na wokovu wangu, yeye ni ngome yangu, sitatikisika.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wakolosai 3:2

Muwe na hamu ya mambo ya huko juu, na siyo mambo ya hapa duniani.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 25:1-3

“Wakati huo, ufalme wa mbinguni utafanana na wasichana kumi waliochukua taa zao, wakaenda kumlaki bwana arusi. Basi, wale wasichana wapumbavu walipokwenda kununua mafuta, bwana arusi akafika, na wale wasichana waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye katika jumba la harusi, kisha mlango ukafungwa. Baadaye wale wasichana wengine wakaja, wakaita: ‘Bwana, Bwana, tufungulie!’ Lakini yeye akawajibu, ‘Nawaambieni kweli, siwajui nyinyi.’” Kisha Yesu akasema, “Kesheni basi, kwa maana hamjui siku wala saa. “Wakati huo itakuwa kama mtu mmoja aliyetaka kusafiri ngambo: Aliwaita watumishi wake, akawakabidhi mali yake. Alimpa kila mmoja kadiri ya uwezo wake: Mmoja fedha talanta tano, mwingine talanta mbili na mwingine talanta moja, kisha akasafiri. Mara yule aliyekabidhiwa fedha talanta tano akafanya kazi nazo akapata faida talanta tano. Hali kadhalika na yule aliyekabidhiwa talanta mbili akapata faida talanta mbili. Lakini yule aliyekabidhiwa fedha talanta moja akaenda, akachimba shimo ardhini, akaificha fedha ya bwana wake. “Baada ya muda mrefu, yule bwana alirudi, akaanza kukagua hesabu ya matumizi na mapato ya fedha yake. Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara. Mtumishi aliyekabidhiwa fedha talanta tano akaja amechukua talanta tano faida, akamwambia, ‘Bwana, ulinikabidhi talanta tano, hapa pana talanta tano zaidi faida niliyopata.’ Bwana wake akamwambia, ‘Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.’ “Mtumishi aliyekabidhiwa talanta mbili akaja, akatoa talanta mbili faida, akisema, ‘Bwana, ulinikabidhi talanta mbili. Chukua talanta mbili zaidi faida niliyopata.’ Bwana wake akamwambia, ‘Vema, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu katika mambo madogo, nitakukabidhi makubwa. Njoo ufurahi pamoja na bwana wako.’ “Lakini yule aliyekabidhiwa fedha talanta moja akaja, akasema, ‘Bwana, najua wewe ni mtu mgumu; wewe huvuna pale ambapo hukupanda, na kukusanya pale ambapo hukutawanya. Niliogopa, nikaificha fedha yako katika ardhi. Chukua basi mali yako.’ “Bwana wake akamwambia, ‘Wewe ni mtumishi mwovu na mvivu! Unajua kuwa mimi huvuna mahali ambapo sikupanda, na hukusanya pale ambapo sikutawanya. Ilikupasa basi, kuiweka fedha yangu katika benki, nami ningelichukua mtaji wangu na faida yake! Basi, mnyanganyeni hiyo fedha mkampe yule mwenye talanta kumi. Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa. Wale wapumbavu walichukua taa zao, lakini hawakuchukua akiba ya mafuta.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 6:10

Hatimaye, nawatakeni muwe imara katika kuungana na Bwana na kwa msaada wa nguvu yake kuu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 141:3

Ee Mwenyezi-Mungu ukilinde kinywa changu, uweke ulinzi mlangoni mwa mdomo wangu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 58:1

Mwenyezi-Mungu asema: “Piga kelele, wala usijizuie; paza sauti yako kama tarumbeta. Watangazie watu wangu makosa yao, waambie wazawa wa Yakobo dhambi zao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 12:11

Msilegee katika bidii, ila muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:147

Naamka kabla ya pambazuko na kukuomba msaada; naweka tumaini langu katika maneno yako.

Sura   |  Matoleo Nakili
2 Wakorintho 4:16

Kwa sababu hiyo hatufi moyo; na hata kama maumbile yetu ya nje yataoza, lakini kwa ndani tunafanywa wapya siku kwa siku.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 24:43

Lakini kumbukeni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua siku mwizi atakapofika, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 5:10

ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tu hai au tumekufa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:1-2

Heri watu wanaoishi bila kosa, wanaozingatia sheria ya Mwenyezi-Mungu. Najitahidi kukutii kwa moyo wote; usiniache nikiuke amri zako. Nawapita wazee kwa busara yangu, kwa sababu nazishika kanuni zako. Najizuia nisifuate njia mbaya, nipate kulizingatia neno lako. Sikukiuka maagizo yako, maana wewe mwenyewe ulinifundisha. Maneno yako ni matamu sana kwangu; naam, ni matamu kuliko asali! Kwa kanuni zako napata hekima, kwa hiyo nachukia kila mwenendo mbaya. Neno lako ni taa ya kuniongoza, na mwanga katika njia yangu. Nimeapa na kuthibitisha kiapo changu, kwamba nitashika maagizo yako adili. Ee Mwenyezi-Mungu, ninateseka mno; unijalie uhai kama ulivyoahidi. Ee Mwenyezi-Mungu, upokee sala yangu ya shukrani; na kunifundisha maagizo yako. Maisha yangu yamo hatarini daima, lakini siisahau sheria yako. Nimeshika neno lako moyoni mwangu, nisije nikakukosea. Waovu wamenitegea mitego, lakini sikiuki kanuni zako. Maamuzi yako ni riziki kubwa kwangu milele; hayo ni furaha ya moyo wangu. Nimekusudia kwa moyo wote kufuata masharti yako milele. Nawachukia watu wanafiki, lakini naipenda sheria yako. Wewe ni ngao yangu, kwako napata usalama; naweka tumaini langu katika neno lako. Ondokeni kwangu, enyi waovu, ili nipate kushika amri za Mungu wangu. Uniimarishe ulivyoahidi, nami nitaishi; usikubali niaibike katika tumaini langu. Unitegemeze, niwe salama; niwe daima msikivu kwa masharti yako. Unawakataa wote wanaokiuka masharti yako; mawazo yao maovu ni ya bure. Waovu wote wawaona kuwa takataka, kwa hiyo mimi napenda maamuzi yako. Utukuzwe, ee Mwenyezi-Mungu! Unifundishe masharti yako. Natetemeka kwa kukuogopa wewe; nimejaa hofu kwa sababu ya hukumu zako. Nimefanya mambo mema na adili; usiniache makuchani mwa maadui zangu. Uahidi kunisaidia mimi mtumishi wako; usikubali wenye kiburi wanidhulumu. Macho yangu yanafifia nikingojea uniokoe, nikingojea utimize uliyoahidi. Unitendee mimi mtumishi wako kadiri ya wema wako, unifundishe masharti yako. Mimi ni mtumishi wako, unipe maarifa, nipate kujua maamuzi yako. Ee Mwenyezi-Mungu, sasa ni wakati wa kufanya kitu, kwa maana watu wanavunja sheria yako. Mimi, nazipenda amri zako, kuliko hata dhahabu safi kabisa. Kwa hiyo, nafuata kanuni zako zote; kila njia potovu naichukia. Maamuzi yako ni ya ajabu; kwa hiyo nayashika kwa moyo wote. Nitayarudia kwa sauti maagizo yako yote uliyotoa. Maelezo ya mafundisho yako huleta mwanga; huwapa akili watu wasiojua kitu. Nafungua kinywa kwa hamu kubwa, maana ninatamani sana amri zako. Unigeukie na kunionea huruma, kama uwatendeavyo wanaokupenda. Uniimarishie hatua zangu kama ulivyoahidi; usikubali mimi nitawaliwe na uovu. Unikomboe kutoka udhalimu wa binadamu, ili nipate kuzishika kanuni zako. Uniangazie uso wako kwa wema, unifundishe masharti yako. Macho yangu yabubujika machozi kama mto, kwa sababu watu hawaishiki sheria yako. Ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni mwadilifu; na hukumu zako ni za haki. Umetoa maamuzi yako, kwa haki na uthabiti. Upendo wangu kwako wanifanya niwake hasira, maana maadui zangu hawajali maneno yako. Nafurahi kufuata maamuzi yako, kuliko kuwa na utajiri mwingi. Ahadi yako ni hakika kabisa, nami mtumishi wako naipenda. Mimi ni mdogo na ninadharauliwa; hata hivyo sisahau kanuni zako. Uadilifu wako ni wa haki milele; sheria yako ni ya kweli. Taabu na huzuni vimenipata, lakini amri zako ndizo furaha yangu. Maamuzi yako ni ya haki daima; unijalie maarifa nipate kuishi. Nakulilia kwa moyo wangu wote; unijibu, ee Mwenyezi-Mungu, nifuate kanuni zako. Nakulilia, unisalimishe; nipate kuyazingatia maamuzi yako. Naamka kabla ya pambazuko na kukuomba msaada; naweka tumaini langu katika maneno yako. Nakaa macho usiku kucha, ili nitafakari juu ya maagizo yako. Kwa fadhili zako, ee Mwenyezi-Mungu, unisikie; unisalimishe kwa uadilifu wako. Nazitafakari kanuni zako, na kuzizingatia njia zako. Wale wanaonidhulumu vibaya wanakaribia, hao wako mbali kabisa na sheria yako. Lakini wewe u karibu nami, ee Mwenyezi-Mungu, na amri zako zote ni za kuaminika. Tangu zamani, nimejifunza maamuzi yako; ambayo umeyaweka hata yadumu milele. Uangalie mateso yangu, uniokoe, kwa maana sikuisahau sheria yako. Unitetee na kunikomboa; unijalie uhai kama ulivyoahidi. Waovu hawataokolewa kamwe, maana hawajali juu ya masharti yako. Huruma yako ni kubwa, ee Mwenyezi-Mungu, unijalie uhai kama ulivyoahidi. Maadui na wadhalimu wangu ni wengi, lakini mimi sikiuki maamuzi yako. Niwaonapo wahaini hao nachukizwa mno, kwa sababu hawazishiki amri zako. Tazama, ee Mungu, ninavyozipenda kanuni zako! Unijalie uhai kadiri ya fadhili zako. Nayafurahia masharti yako; sitalisahau neno lako. Kitovu cha neno lako ni ukweli, maagizo yako yote adili, yadumu milele. Wakuu wanidhulumu bila kisa, lakini mimi naheshimu maneno yako kwa moyo wote. Nafurahi kwa sababu ya neno lako, kama mtu aliyekuta kitu cha thamani kuu. Nachukia kabisa uongo, lakini naipenda sheria yako. Nakusifu mara saba kila siku, kwa sababu ya maagizo yako adili. Wapendao sheria yako wana amani kuu; hakuna kinachoweza kuwaangusha. Ee Mwenyezi-Mungu, nakungojea uniokoe; mimi natimiza amri zako. Nazingatia maamuzi yako; nayapenda kwa moyo wote. Nazingatia kanuni na maamuzi yako; wewe wauona mwenendo wangu wote. Kilio changu kikufikie, ee Mwenyezi-Mungu! Unijalie akili kama ulivyoahidi. Unitendee mimi mtumishi wako kwa ukarimu, nipate kuishi na kushika neno lako. Ombi langu likufikie; uniokoe kama ulivyoahidi. Nitasema sifa zako mfululizo, maana wanifundisha masharti yako. Nitaimba juu ya neno lako, maana amri zako zote ni za haki. Uwe daima tayari kunisaidia, maana nimeamua kufuata kanuni zako. Natazamia sana uniokoe, ee Mwenyezi-Mungu; sheria yako ndiyo furaha yangu. Unijalie kuishi nipate kukusifu; na maagizo yako yanisaidie. Natangatanga kama kondoo aliyepotea; uje kunitafuta mimi mtumishi wako, maana sikusahau amri zako. Uyafumbue macho yangu, niyaone maajabu ya sheria yako. Mimi ni mkimbizi tu hapa duniani; usinifiche amri zako. Heri wanaozingatia matakwa yake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote,

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 4:25-27

Uyaelekeze macho yako mbele kwa ujasiri, mtazamo wako uwe mbele moja kwa moja. Fikiria njia utakayochukua, na hatua zako zote zitakuwa kamili. Usigeukie kulia wala kushoto; epusha mguu wako mbali na uovu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 5:20

Twajua pia kwamba Mwana wa Mungu amekuja, akatupa elimu ili tumjue Mungu wa kweli; tuishi katika muungano na Mungu wa kweli – katika muungano na Mwanae, Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na huu ndio uhai wa milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 88:13

Lakini mimi nakulilia, ee Mwenyezi-Mungu; kila asubuhi nakuletea ombi langu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 26:38

Hapo akawaambia, “Nina huzuni kubwa moyoni hata karibu kufa. Kaeni hapa mkeshe pamoja nami.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 11:6

Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa maana kila mtu anayemwendea Mungu ni lazima aamini kwamba Mungu yuko, na kwamba huwatuza wale wanaomtafuta.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 6:4

Jitahidi usiache macho yako yapate usingizi, wala kope za macho yako zisinzie.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 5:25

Tukiishi kwa msaada wa Roho, na tuufuate mwongozo wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 21:34-36

“Muwe macho, mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na shughuli za maisha haya. La sivyo, siku ile itawajieni ghafla. Kwa maana itawajia kama mtego wote wanaoishi duniani pote. Muwe waangalifu basi, na salini daima ili muweze kupata nguvu ya kupita salama katika mambo haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele ya Mwana wa Mtu.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 121:2

Msaada wangu watoka kwa Mwenyezi-Mungu, aliyeumba mbingu na dunia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 62:5-6

Namngojea Mungu peke yake kwa utulivu; kwake naliweka tumaini langu. Yeye peke yake ndiye mwamba na wokovu wangu, yeye ni ngome yangu, sitatikisika.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 10:12

Anayedhani amesimama imara ajihadhari asianguke.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:70

Mioyo yao imejaa upumbavu, lakini mimi nafurahia sheria yako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 5:3

Ee Mwenyezi-Mungu, alfajiri waisikia sauti yangu, asubuhi nakutolea tambiko yangu, kisha nangojea unijibu.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Petro 1:13

Kwa hiyo, basi, muwe tayari kabisa, na kukesha. Wekeni tumaini lenu lote katika neema ile mtakayopewa wakati Yesu Kristo atakapoonekana!

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 68:19

Mwenyezi-Mungu asifiwe siku kwa siku! Yeye hutubebea mizigo yetu; yeye ndiye Mungu wa wokovu wetu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 91:2

ataweza kumwambia Mwenyezi-Mungu: “Wewe ni kimbilio langu na ngome yangu; Mungu wangu, ninayekutumainia!”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 16:17-18

Ndugu zangu, nawasihi mwafichue wote wanaosababisha mafarakano na kuwafanya watu wengine waanguke, kinyume cha mafundisho mliyofundishwa. Jiepusheni na watu hao, maana watu wa namna hiyo hawamtumikii Kristo Bwana wetu, bali wanayatumikia matumbo yao wenyewe. Kwa maneno yao matamu na hotuba za kubembeleza hupotosha mioyo ya watu wanyofu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 7:15-16

“Jihadharini na manabii wa uongo. Wao huja kwenu wakionekana kama kondoo kwa nje, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali. Mtawatambua kwa matendo yao. Je, watu huchuma zabibu katika miti ya miiba, au tini katika mbigili? La!

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 12:1-2

Sisi tunalo kundi hili kubwa la mashahidi mbele yetu. Kwa hiyo tuondoe kila kizuizi kinachotuzuia, na dhambi ile inayotungangania. Tupige mbio kwa uvumilivu katika mashindano yaliyowekwa mbele yetu. Wazazi wetu hapa duniani walituadhibu kwa muda, kama wao wenyewe walivyoona kuwa vema; lakini Mungu anatuadhibu kwa ajili ya faida yetu wenyewe, tupate kuushiriki utakatifu wake. Kuadhibiwa si jambo la kufurahisha bali la kuhuzunisha. Lakini wale waliofunzwa kuwa na nidhamu mwishowe watavuna tuzo la amani kutoka katika maisha adili. Basi, inueni mikono yenu inayolegea na kuimarisha magoti yenu yaliyo dhaifu. Endeleeni kutembea katika njia iliyonyoka, ili kile kilicholemaa kisiumizwe, bali kiponywe. Jitahidini kuishi kwa amani na watu wote. Ishini maisha ya utakatifu, kwa sababu hakuna mtu atakayemwona Bwana bila ya maisha kama hayo. Jitahidini sana mtu yeyote asije akapoteza neema ya Mungu. Muwe waangalifu ili mti mchungu usizuke kati yenu na kuwaua wengi kwa sumu yake. Jihadharini ili miongoni mwenu pasiwe na mtu mwasherati au mtu asiyemcha Mungu kama Esau, aliyeuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa mlo mmoja. Nyinyi mnafahamu kwamba hata alipotaka kuipata tena ile baraka iliyokuwa yake, alikataliwa, maana hakupata tena nafasi ya kutubu, ingawa aliitafuta kwa machozi. Nyinyi hamkuwasili mlimani Sinai, ambao unaweza kushikika kama walivyofanya watu wa Israeli; hamkufika kwenye moto uwakao, penye giza, tufani, mvumo wa tarumbeta na sauti ya maneno. Wale waliosikia sauti hiyo waliomba wasisikie tena neno lingine, Tumwelekee Yesu ambaye ndiye aliyeianzisha imani yetu na ambaye ataikamilisha. Kwa ajili ya furaha iliyokuwa inamngojea, yeye alivumilia kifo msalabani, bila kuijali aibu yake, na sasa anaketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 2:37

Halafu alibaki mjane hadi wakati huo akiwa mzee wa miaka themanini na minne. Wakati huo wote alikaa hekaluni akifunga na kusali usiku na mchana.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 40:29-31

Yeye huwapa uwezo walio hafifu, wanyonge huwapa nguvu. Sauti ya mtu anaita jangwani: “Mtayarishieni Mwenyezi-Mungu njia, nyosheni barabara kuu kwa ajili ya Mungu wetu. Hata vijana watafifia na kulegea; naam, wataanguka kwa uchovu. Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu, watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mabawa kama tai; watakimbia bila kuchoka; watatembea bila kulegea.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 3:1

Oneni, basi, jinsi Baba alivyotupenda mno hata tunaitwa watoto wa Mungu! Na kweli, ndivyo tulivyo. Ndiyo maana ulimwengu haututambui sisi, kwani haumjui Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 25:5

Uniongoze katika ukweli wako na kunifundisha, kwani wewe ni Mungu, mwokozi wangu; ninakutegemea wewe kila siku.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 6:7

Msidanganyike; Mungu hafanyiwi dhihaka. Alichopanda mtu ndicho atakachovuna.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 4:30

Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, maana Roho huyo ni alama ya Mungu kwenu kwamba nyinyi ni watu wake, na thibitisho kwamba siku itakuja ambapo Mungu atawakomboeni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 121:1

Natazama juu milimani; msaada wangu utatoka wapi?

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 10:16

“Sasa, mimi nawatuma nyinyi kama kondoo kati ya mbwamwitu. Muwe na busara kama nyoka, na wapole kama njiwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 10:17

Hivyo basi, imani inatokana na kuusikia ujumbe, na huo ujumbe unatokana na neno la Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 4:8

Hatimaye, ndugu zangu, zingatieni mambo mema na yanayostahili kusifiwa; mambo ya kweli na bora; mambo ya haki, safi, ya kupendeza na ya heshima.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wakorintho 4:5

Basi, msihukumu kabla ya wakati wake; acheni mpaka Bwana atakapokuja. Yeye atayafichua mambo ya giza yaliyofichika, na kuonesha wazi nia za mioyo ya watu. Ndipo kila mmoja atapata sifa anayostahili kutoka kwa Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:65

Umenitendea vema mimi mtumishi wako, kama ulivyoahidi, ee Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 1:14

Hawa wote walikusanyika pamoja kusali, pamoja na wanawake kadha wa kadha, na Maria mama yake Yesu, na ndugu zake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 18:19

Tena nawaambieni, wawili miongoni mwenu wakikubaliana hapa duniani kuhusu jambo lolote la kuomba, Baba yangu wa mbinguni atawafanyia jambo hilo.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 5:17

salini kila wakati

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Wathesalonike 5:11

Kwa hiyo farijianeni na kusaidiana nyinyi kwa nyinyi, kama mnavyofanya sasa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 5:14-15

Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, nao watamwombea na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na dhambi alizotenda zitaondolewa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waefeso 6:18

Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wakolosai 4:2

Dumuni katika sala, na mnaposali muwe waangalifu, mkimshukuru Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 5:16

Basi, ungamanieni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate kuponywa. Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 2:1

Kwanza kabisa, nawasihi muombe dua, msali na kumshukuru Mungu kwa ajili ya watu wote,

Sura   |  Matoleo Nakili
Wakolosai 4:3

Vilevile, mtuombee sisi pia ili Mungu atupe fursa ya kuuhubiri ujumbe wake kuhusu siri ya Kristo. Kwa ajili hiyo mimi niko sasa kifungoni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wakolosai 1:3

Daima tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, wakati tunapowaombea.

Sura   |  Matoleo Nakili
Matendo 2:42

Hawa wote waliendelea kujifunza kutoka kwa mitume, kuishi pamoja kindugu, kumega mkate na kusali.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 18:20

Kwa maana popote pale wanapokusanyika wawili au watatu kwa jina langu, mimi nipo hapo kati yao.”

Sura   |  Matoleo Nakili

Maombi kwa Mungu

Ee Mungu Mwenyezi Baba, kwako utukufu na heshima yote. Katika wakati huu niliotenga kuomba na kutafakari neno lako usiku huu, nakushukuru Roho Mtakatifu, najua uko hapa. Asante kwa uwepo wako na kwa kuniongoza kukutana nawe. Ninaweka mikononi mwako mizigo yangu, hofu zangu, mashaka yangu na mateso yangu, uyatawanye kwa uwepo wako mkuu. Ujaze moyo wangu usiku huu kwa upendo wako, ung'oe chuki, kinyongo na uchungu maishani mwangu. Uniweke huru kutoka kwa wivu, tamaa na ubinafsi ili nifurahie usiku huu wa maombi kwa amani na baraka. Naomba unisamehe dhambi zangu, kwa lolote nililokufanya lisilokupendeza. Unihurumie Ee Bwana na uisikie sala yangu, tega sikio lako kwa kilio changu, natamani kuuona utukufu wako na kuhisi moto wa Roho wako Mtakatifu. Bwana, nakupa moyo wangu kwa unyenyekevu, uutakase na uujaze kwa uwepo wako wa ajabu. Ninakuomba uchukue udhibiti wa maisha yangu, matendo yangu na maneno yangu. Upake mafuta akili yangu na neuroni zangu nipokee neno lako kwa ufahamu. Bwana, ihifadhi moyoni mwangu kila neno kutoka usiku huu na unisaidie nibaki macho ili niwe na usiku wa maombi wenye utaritibu na baraka, kwa maana neno lako linasema, "Dumuni katika kusali, mkikesha katika sala pamoja na kushukuru". Katika jina la Yesu. Amina!

Vikundi Vidogo

Tufuate:

Matangazo


Matangazo