Mungu wetu hukaa katikati ya sifa za watu wake. Kila siku tuna sababu za kumsifu na kumuabudu Mungu wetu. Anafurahishwa na sifa zitokazo moyoni, sifa za kweli zenye shukrani.
Unaposifu, miujiza hufanyika maishani mwako. Katika sifa, kuna uponyaji, kuna uhuru. Baba yetu wa Mbinguni ametenda maajabu mengi maishani mwako tangu alipokuumba. Amekuwa mwaminifu na amekulinda, kwa hivyo msifu Mungu kwa sababu ni mwema na fadhili zake ni mpya kila asubuhi.
Zaburi 71:8 inasema, "Kinywa changu kijazwe sifa zako, Na utukufu wako mchana mzima." Mungu ataijaza kinywa chako sifa, neno lake linasema hivyo. Anza tu kushukuru kwa wema wake, naye atakupa sifa zitokazo moyoni.
Zaburi 30:12 inasema, "Kwa hiyo nitakuimbia, utukufu wangu, Wala sitanyamaza. Ee Bwana, Mungu wangu, Nitakushukuru milele." Basi, msifu Mungu daima.
Lakini mimi nitaimba sifa za nguvu yako; nitashangilia asubuhi juu ya fadhili zako; maana wewe umekuwa ngome yangu na kimbilio langu wakati wa taabu.
Fadhili zako ni bora kuliko maisha, nami nitakusifu kwa mdomo wangu. Nitakushukuru maisha yangu yote; nitainua mikono yangu na kukuomba.
Njoni tumwimbie Mwenyezi-Mungu, tumshangilie mwamba wa wokovu wetu! Kwa miaka arubaini nilichukizwa nao, nikasema: ‘Kweli, hawa ni watu waliopotoka! Hawajali kabisa njia zangu!’ Basi, nilikasirika, nikaapa: ‘Hawataingia mahali pangu pa pumziko!’” Twende mbele zake na shukrani; tumshangilie kwa nyimbo za sifa.
Ujumbe wa Kristo na ukae ndani yenu pamoja na utajiri wake wote. Fundishaneni na kushauriana kwa hekima yote. Imbeni Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Mungu mioyoni mwenu kwa shukrani.
Mshangilieni Mwenyezi-Mungu, enyi nchi zote! Mwabuduni Mwenyezi-Mungu kwa furaha, nendeni kwake mkiimba kwa shangwe!
Karibu na usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakisali na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, huku wafungwa wengine wakiwa wanasikiliza.
Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake; mtengenezeeni njia yake apandaye mawinguni. Jina lake ni Mwenyezi-Mungu; furahini mbele yake. Mungu akaaye mahali pake patakatifu, ni Baba wa yatima na mlinzi wa wajane.
Mwimbieni Mwenyezi-Mungu wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu! Mkono wake hodari, mkono wake mtakatifu umempatia ushindi. Mwenyezi-Mungu ameonesha ushindi wake; ameyadhihirishia mataifa uwezo wake wa kuokoa.
Lakini mimi nazitumainia fadhili zako; moyo wangu na ufurahie wokovu wako. Nitakuimbia wewe, ee Mwenyezi-Mungu, kwa ukarimu mwingi ulionitendea!
Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Bwana nyimbo na Zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu.
Nitapaza sauti kwa furaha, ninapokuimbia wewe sifa zako, na roho yangu itakusifu maana umeniokoa.
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Jinsi gani ilivyo vizuri kumwimbia sifa Mungu wetu! Yeye ni mwema na astahili kuimbiwa sifa.
Nitamwimbia Mwenyezi-Mungu maisha yangu yote; nitamsifu Mungu wangu muda wote niishipo.
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Mwimbieni Mwenyezi-Mungu wimbo mpya; msifuni katika kusanyiko la waaminifu!
Mwimbieni Mwenyezi-Mungu sifa kwa kuwa ametenda mambo makuu; haya na yajulikane duniani kote.
Alinifundisha wimbo mpya, wimbo wa sifa kwa Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa, na kumtumainia Mwenyezi-Mungu.
Shangilieni kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu enyi waadilifu! Kumsifu Mungu ni wajibu wa watu wanyofu. Mwenyezi-Mungu hupangua mipango ya mataifa, na kuyatangua mawazo yao. Mpango wa Mwenyezi-Mungu hudumu milele; maazimio yake yadumu vizazi vyote. Heri taifa ambalo Mungu wake ni Mwenyezi-Mungu; heri wale aliowachagua kuwa watu wake mwenyewe! Mwenyezi-Mungu huangalia chini kutoka mbinguni, na kuwaona wanadamu wote. Kutoka kwenye kiti chake cha enzi, huwaangalia wakazi wote wa dunia. Yeye huunda mioyo ya watu wote, yeye ajua kila kitu wanachofanya. Mfalme hawezi kuokolewa kwa kuwa na jeshi kubwa; wala shujaa hapati ushindi kwa nguvu zake kubwa. Farasi wa vita hafai kitu kwa kupata ushindi; nguvu zake nyingi haziwezi kumwokoa mtu. Mwenyezi-Mungu huwaangalia wale wamchao, watu ambao wanatumainia fadhili zake. Yeye huwaokoa katika kifo, huwaweka hai wakati wa njaa. Msifuni Mwenyezi-Mungu kwa zeze; mwimbieni kwa kinubi cha nyuzi kumi. Mioyo yetu yamtumainia Mwenyezi-Mungu. Yeye ni msaada wetu na ngao yetu. Naam twafurahi kwa sababu yake; tuna matumaini katika jina lake takatifu. Fadhili zako zikae nasi, ee Mwenyezi-Mungu, kwani sisi tumekuwekea tumaini letu. Mwimbieni wimbo mpya; pigeni kinubi vizuri na kushangilia.
Mwimbieni Mwenyezi-Mungu wimbo mpya! Dunia yote iimbe sifa zake: Bahari na vyote vilivyomo, nchi za mbali na wakazi wake;
Fadhili zako ee Mwenyezi-Mungu zaenea hata mbinguni; uaminifu wako wafika mawinguni. Uadilifu wako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama vilindi vya bahari. Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, wawalinda wanadamu na wanyama
Mwimbieni Mwenyezi-Mungu wimbo mpya! Mwimbieni Mwenyezi-Mungu, ulimwengu wote! Yaambieni mataifa: “Mwenyezi-Mungu anatawala! Ameuweka ulimwengu imara, hautatikisika. Atawahukumu watu kwa haki!” Furahini enyi mbingu na dunia! Bahari na ivume pamoja na vyote vilivyomo! Furahini enyi mashamba na vyote vilivyomo! Ndipo miti yote misituni itaimba kwa furaha, mbele ya Mwenyezi-Mungu anayekuja; naam, anayekuja kuihukumu dunia. Ataihukumu dunia kwa haki, na mataifa kwa uaminifu wake. Mwimbieni Mwenyezi-Mungu na kulisifu jina lake. Tangazeni kila siku matendo yake ya wokovu.
Mwenyezi-Mungu ni mkuu, astahili sifa nyingi; ukuu wake hauwezi kuchunguzika. Kizazi hata kizazi, sifa za matendo yako zitasimuliwa, watu watatangaza matendo yako makuu. Nitanena juu ya utukufu na fahari yako, nitayatafakari matendo yako ya ajabu.
Lakini wafurahi wote wanaokimbilia usalama kwako, waimbe kwa shangwe daima. Uwalinde wanaolipenda jina lako, wapate kushangilia kwa sababu yako.
Mwimbieni Mwenyezi-Mungu sifa, enyi waaminifu wake; kumbukeni utakatifu wake na kumshukuru.
Mwimbieni Mwenyezi-Mungu, ulimwengu wote. Tangazeni kila siku matendo yake ya wokovu. Yatangazieni mataifa utukufu wake, waambieni watu wote matendo yake ya ajabu. Maana Mwenyezi-Mungu ni mkuu, anasifika sana anastahili kuheshimiwa kuliko miungu yote.
Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake; mtengenezeeni njia yake apandaye mawinguni. Jina lake ni Mwenyezi-Mungu; furahini mbele yake.
Mwimbieni kwa sauti Mungu, nguvu yetu, mshangilieni Mungu wa Yakobo; Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri. Fumbua kinywa chako, nami nitakulisha. “Lakini watu wangu hawakunisikiliza; Israeli hakunitaka kabisa. Hivyo, nikawaacha wabaki na ukaidi wao; wafuate mashauri yao wenyewe. Laiti watu wangu wangenisikiliza! Laiti Israeli angefuata njia yangu! Ningewashinda maadui zao haraka; ningenyosha mkono dhidi ya wadhalimu wao. Wanichukiao wangenipigia magoti kwa hofu, na adhabu yao ingekuwa ya milele. Lakini wewe ningekulisha kwa ngano bora, ningekushibisha kwa asali ya mwambani.” vumisheni wimbo wa shangwe, pigeni ngoma, chezeni zeze na kinubi cha sauti nzuri.
Anayekaa chini ya ulinzi wa Mungu Mkuu, anayeishi chini ya kivuli cha Mungu Mwenye Nguvu,
Mwimbieni Mwenyezi-Mungu wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu! Mkono wake hodari, mkono wake mtakatifu umempatia ushindi.
Mwimbieni Mwenyezi-Mungu sifa kwa kuwa ametenda mambo makuu; haya na yajulikane duniani kote. Pazeni sauti na kuimba kwa furaha, enyi wakazi wa Siyoni, maana aliye mkuu miongoni mwenu ndiye Mungu, Mtakatifu wa Israeli.”
Enyi watu wote duniani mshangilieni Mungu! Umetupima, ee Mungu, umetujaribu kama madini motoni. Umetuacha tunaswe wavuni; umetubebesha taabu nzito. Umewaacha watu watukanyage; tumepitia motoni na majini. Lakini sasa umetuleta kwenye usalama. Nitakuja nyumbani kwako na sadaka za kuteketezwa, nitakutimizia nadhiri zangu, nilizotamka na kukuahidi mimi mwenyewe nilipokuwa taabuni. Nitakutolea sadaka za kuteketezwa nononono, tambiko za kuteketezwa za kondoo madume; nitatoa sadaka za ng'ombe na mbuzi. Enyi mnaomcha Mungu, njoni nyote mkasikilize, nami nitawasimulieni aliyonitendea. Mimi nilimlilia msaada kwa sauti, sifa zake nikazitamka. Kama ningalinuia maovu moyoni, Mwenyezi-Mungu hangalinisikiliza. Lakini kweli Mungu amenisikiliza; naam, amesikiliza maneno ya sala yangu. Imbeni juu ya utukufu wa jina lake, mtoleeni sifa tukufu!
Pazeni sauti za shangwe, enyi magofu ya Yerusalemu! Mwenyezi-Mungu amewafariji watu wake, ameukomboa mji wa Yerusalemu.
Mshukuruni Mwenyezi-Mungu, tangazeni ukuu wake; yajulisheni mataifa mambo aliyotenda! Alimthibitishia Yakobo ahadi yake, alimhakikishia Israeli agano hilo la milele. Alisema: “Nitawapeni nchi ya Kanaani, nayo itakuwa mali yenu wenyewe.” Watu wa Mungu walikuwa wachache; hawakuwa maarufu, tena walikuwa wageni nchini Kanaani. Walitangatanga kutoka taifa hadi taifa; kutoka nchi moja hadi nchi nyingine. Lakini Mungu hakuruhusu mtu awadhulumu; kwa ajili yao aliwaonya wafalme: “Msiwaguse wateule wangu; msiwadhuru manabii wangu!” Mungu alizusha njaa nchini mwao, akaharibu chakula chao chote. Lakini aliwatangulizia mtu mmoja, Yosefu aliyekuwa ameuzwa utumwani. Walimfunga miguu kwa minyororo, na shingoni kwa nira ya chuma, Muda si muda alichotabiri kilitimia. neno la Mwenyezi-Mungu lilimdhibiti. Mshangilieni, mwimbieni Mungu sifa; simulieni matendo yake ya ajabu!
Nitamshukuru Mwenyezi-Mungu kwani ni mwema; nitaimba sifa za jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu.
Amka, ee nafsi yangu! Amkeni, enyi kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko! Ee Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa; nitakuimbia sifa kati ya mataifa.
Lakini mimi nitaimba sifa za nguvu yako; nitashangilia asubuhi juu ya fadhili zako; maana wewe umekuwa ngome yangu na kimbilio langu wakati wa taabu. Ewe uliye nguvu yangu, nitakuimbia sifa; ee Mungu, wewe u ngome yangu; Mungu mwenye kunifadhili!
Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yakubalike mbele yako, ee Mwenyezi-Mungu, mwamba wangu na mkombozi wangu!
Mwenyezi-Mungu ndiye nguvu yangu na ngao yangu; tegemeo la moyo wangu limo kwake. Amenisaidia nami nikashangilia kwa moyo; kwa wimbo wangu ninamshukuru.
Ni vema kukushukuru, ee Mwenyezi-Mungu, kuliimbia sifa jina lako, ee Mungu Mkuu. Wewe umenipa nguvu kama nyati; umenimiminia mafuta ya kuburudisha. Kwa macho nimeona maadui zangu wameshindwa; nimesikia kilio chao watendao maovu. Waadilifu hustawi kama mitende; hukua kama mierezi ya Lebanoni! Kama miti iliyopandwa nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu, hustawi katika nyua za Mungu wetu; huendelea kuzaa matunda hata uzeeni; daima wamejaa utomvu na wabichi; wapate kutangaza kwamba Mwenyezi-Mungu ni mnyofu, Mwamba wangu, kwake hamna upotovu. Ni vema kutangaza fadhili zako asubuhi, na uaminifu wako nyakati za usiku,
ili nao watu wa mataifa mengine wapate kumtukuza Mungu kwa sababu ya huruma yake. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Kwa hiyo nitakusifu miongoni mwa watu wa mataifa. Nitaziimba sifa za jina lako.”
Kwa sifa za watoto wadogo na wanyonyao, umejiwekea ngome dhidi ya adui zako, uwakomeshe waasi na wapinzani wako.
Nakushukuru, ee Mwenyezi-Mungu, kwa moyo wangu wote, naimba sifa zako mbele ya miungu. Ninasujudu kuelekea hekalu lako takatifu; nalisifu jina lako, kwa sababu ya fadhili zako na uaminifu wako; kwa sababu umeweka jina lako na neno lako juu ya kila kitu.
Viumbe vyako vyote vitakushukuru, ee Mwenyezi-Mungu, nao waaminifu wako watakutukuza. Watasema juu ya utukufu wa ufalme wako, na kutangaza juu ya nguvu yako kuu, ili kila mtu ajue matendo yako makuu, na fahari tukufu ya ufalme wako.
Mbona nasononeka hivyo moyoni? Kwa nini nahangaika hivyo? Nitamtumainia Mungu, maana nitamsifu tena Mungu, aliye msaada wangu na Mungu wangu.
Nafsi yangu yatamani mno maskani ya Mwenyezi-Mungu! Moyo na mwili wangu wote wamshangilia Mungu aliye hai.
Pitieni milango ya hekalu lake kwa shukrani, ingieni katika nyua zake kwa sifa. Mshukuruni na kulisifu jina lake.
Mungu ni kimbilio letu na nguvu yetu; yeye ni msaada wetu daima wakati wa taabu. Asema: “Nyamazeni na kujua kuwa mimi ni Mungu! Mimi natukuka katika mataifa yote; mimi natukuzwa ulimwenguni kote!” Mwenyezi-Mungu wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu. Kwa hiyo hatutaogopa chochote, dunia ijapoyeyuka na milima kutikisika kutoka baharini; hata kama bahari ikichafuka na kutisha, na milima ikatetemeka kwa machafuko yake.
Umsifu Mwenyezi-Mungu, ee Yerusalemu! Umsifu Mungu wako, ee Siyoni! Maana yeye huimarisha milango yako, huwabariki watu waliomo ndani yako.
Mfalme Daudi na viongozi wa Walawi, waliwateua baadhi ya wana wa Asafu, wa Hemani, na wa Yeduthuni, kuongoza katika huduma ya kutabiri kwa kutumia vinubi, na vinanda na matoazi. Hii ndiyo orodha ya wale waliochaguliwa kuongoza ibada, pamoja na aina ya kazi iliyofanywa na kila kikundi.
Mshukuruni Mwenyezi-Mungu, kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake zadumu milele. Mataifa yote yalinizingira, lakini kwa jina la Mwenyezi-Mungu nikayaangamiza! Yalinizunguka kila upande, lakini kwa jina la Mwenyezi-Mungu, nikayaangamiza! Yalinizunguka, mengi kama nyuki, lakini yakateketea kama kichaka motoni; kwa jina la Mwenyezi-Mungu niliyaangamiza! Nilishambuliwa mno karibu nishindwe, lakini Mwenyezi-Mungu alinisaidia. Mwenyezi-Mungu ni nguvu yangu kuu; yeye mwenyewe ndiye wokovu wangu. Sauti za furaha ya ushindi zasikika hemani mwao waadilifu: “Mkono wa Mwenyezi-Mungu umetenda mambo makuu! Mkono wa nguvu wa Mwenyezi-Mungu umeleta ushindi! Mkono wa Mwenyezi-Mungu umetenda mambo makuu!” Sitakufa, bali nitaishi, na kusimulia matendo ya Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu ameniadhibu sana, lakini hakuniacha nife. Nifungulie milango ya watu waadilifu, niingie na kumshukuru Mwenyezi-Mungu! Watu wa Israeli na waseme: “Fadhili zake zadumu milele.”
“Twaa kinubi chako uzungukezunguke mjini, ewe malaya uliyesahaulika! Imba nyimbo tamutamu. Imba nyimbo nyinginyingi ili upate kukumbukwa tena.”
Wafalme wote duniani watakusifu, ee Mwenyezi-Mungu, kwa sababu wameyasikia maneno yako.
Nitasema sifa zako mfululizo, maana wanifundisha masharti yako. Nitaimba juu ya neno lako, maana amri zako zote ni za haki.
Lakini mimi umenijalia furaha kubwa moyoni, kuliko ya hao walio na divai na ngano kwa wingi.
Hatutawaficha watoto wetu; ila tutakisimulia kizazi kijacho matendo matukufu ya Mwenyezi-Mungu na uwezo wake; tutawaambia maajabu yake aliyotenda.
Watakaosalia watapaza sauti, wataimba kwa shangwe. Kutoka magharibi watatangaza ukuu wa Mwenyezi-Mungu,
Nitatangaza sifa za Mwenyezi-Mungu; viumbe vyote vilisifu jina lake takatifu, milele na milele.
Ee Mwenyezi-Mungu, matendo yako yanifurahisha; nitashangilia kwa sababu ya mambo yote uliyotenda.
kama asemavyo: “Ee Mungu, nitawasimulia ndugu zangu matendo yako. Nitakusifu katika kusanyiko lao.”
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Msifuni Mungu katika patakatifu pake; msifuni katika mbingu zake kuu.
Dunia yote imshangilie Mwenyezi-Mungu; imsifu kwa nyimbo na vigelegele. Msifuni Mwenyezi-Mungu kwa shangwe, msifuni kwa sauti tamu za zeze. Mpigieni vigelegele Mwenyezi-Mungu mfalme wetu, mshangilieni kwa tarumbeta na sauti ya baragumu.
Tutashangilia kwa ajili ya ushindi wako; tutatweka bendera kulitukuza jina la Mungu wetu. Mwenyezi-Mungu akutimizie maombi yako yote!
Mimi nitakusifu wala sitakaa kimya. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu nitakushukuru milele.
Unitoe humu kifungoni, ili nipate kukushukuru. Watu waadilifu watajiunga nami kwa sababu umenitendea mema mengi.
Heri mtu asiyefuata shauri la waovu, asiyeshiriki njia za wenye dhambi, wala kujumuika na wenye dharau; bali huifurahia sheria ya Mwenyezi-Mungu, na kuitafakari mchana na usiku.
Wafu wako wataishi tena, miili yao itafufuka. Wanaolala mavumbini wataamka na kuimba kwa furaha! Mungu atapeleka umande wake wa uhai, nao walio kwa wafu watatoka hai.
Ee Mwenyezi-Mungu, Bwana wetu, kweli jina lako latukuka duniani kote! Utukufu wako waenea mpaka juu ya mbingu!
Lakini nyinyi watu wa Yerusalemu mtaimba kwa furaha kama mfanyavyo wakati wa mkesha wa sikukuu. Mtajaa furaha kama watu wanaotembea kwa mdundo wa muziki wa filimbi kwenda mlimani kwa Mwenyezi-Mungu, Mwamba wa Israeli.
Kwa hiyo, ndugu zangu, maadamu Mungu ni mwenye huruma nyingi, nawasihi kwa moyo wote: Mtoleeni Mungu miili yenu kama tambiko iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njia yenu halisi ya kumwabudu.