Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 5:6 - Biblia Habari Njema

6 Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema - BHND

6 Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watatoshelezwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watatoshelezwa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

6 Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.

Tazama sura Nakili




Mathayo 5:6
29 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye huwatosheleza walio na kiu; na wenye njaa huwashibisha mema.


Huwapatia mahitaji yao wote wanaomcha; husikia kilio chao na kuwaokoa.


Lakini mimi nitauona uso wako, kwani ni mwadilifu; niamkapo nitajaa furaha kwa kukuona.


Roho yangu inafurahi kama kwa karamu na vinono; kwa shangwe nitaimba sifa zako.


Heri wale unaowachagua na kuwaleta karibu, waishi katika maskani yako. Sisi tutatoshelezwa na mema ya nyumba yako; mema ya hekalu lako takatifu.


Nafsi yangu yatamani mno maskani ya Mwenyezi-Mungu! Moyo na mwili wangu wote wamshangilia Mungu aliye hai.


Anachoogopa mtu mwovu ndicho kitakachompata, lakini anachotamani mwadilifu ndicho atakachopewa.


Anayepania uadilifu na huruma, ataishi maisha marefu na kuheshimiwa.


Naingia bustanini mwangu, dada yangu, bi arusi. Nakusanya manemane na viungo, nala sega langu la asali, nanywa divai yangu na maziwa yangu. Kuleni enyi marafiki, kunyweni; kunyweni sana wapendwa wangu.


Juu ya mlima Siyoni, Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawafanyia watu wote karamu ya vinono na divai nzuri, nyama tamu na mafuta, pamoja na divai safi.


“Maskini na fukara wakitafuta maji wasipate, wakiwa wamekauka koo kwa kiu, mimi Mwenyezi-Mungu nitawajibu; mimi Mungu wa Israeli, sitawaacha.


“Nitaimwagilia maji nchi iliyokauka, na kutiririsha mto katika nchi kame. Nitawamiminia roho yangu wazawa wako, nitawamwagia watoto wako baraka yangu.


Basi, mimi Mwenyezi-Mungu nasema, watumishi wangu watakula, lakini nyinyi mtaona njaa; watumishi wangu watakunywa, lakini nyinyi mtaona kiu; watumishi wangu watafurahi, lakini nyinyi mtafedheheka.


Kama mama, Yerusalemu utawanyonyesha, nanyi mtashiba kwa riziki zake; mtakunywa shibe yenu na kufurahi, kutokana na wingi wa fahari yake.


Waliochoka nitawachangamsha, na walegevu nitawapa nguvu.


Wenye njaa amewashibisha mema, matajiri amewaondoa mikono mitupu.


Heri nyinyi mnaosikia njaa sasa, maana baadaye mtashiba. Heri nyinyi mnaolia sasa, maana baadaye mtacheka kwa furaha.


Ole wenu nyinyi mnaoshiba sasa, maana baadaye mtasikia njaa. Ole wenu nyinyi mnaocheka kwa furaha sasa, maana baadaye mtaomboleza na kulia.


Lakini atakayekunywa maji nitakayompa mimi, hataona kiu milele. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji ya uhai na kumpatia uhai wa milele.”


Msikishughulikie chakula kiharibikacho; kishughulikieni chakula kidumucho kwa ajili ya uhai wa milele. Mwana wa Mtu ambaye Baba amemthibitisha atawapeni chakula hicho.”


Siku ya mwisho ya sikukuu hiyo ilikuwa siku maalumu. Yesu alisimama, akasema kwa sauti kubwa, “Aliye na kiu na aje kwangu anywe.


Hawataona tena njaa wala kiu; jua wala joto kali halitawachoma tena,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo