Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 5:6 - Neno: Maandiko Matakatifu

6 Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watatoshelezwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watatoshelezwa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

6 Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.

Tazama sura Nakili




Mathayo 5:6
29 Marejeleo ya Msalaba  

kwa maana yeye humtosheleza mwenye kiu, na kumshibisha mwenye njaa kwa vitu vyema.


Huwatimizia wamchao matakwa yao, husikia kilio chao na kuwaokoa.


Na mimi katika haki nitauona uso wako, niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako.


Nafsi yangu itatoshelezwa kama kwa wingi wa vyakula; kwa midomo iimbayo kinywa changu kitakusifu wewe.


Heri wale uliowachagua na kuwaleta karibu ili waishi katika nyua zako! Tunashibishwa kwa mema ya nyumba yako, mema ya Hekalu lako takatifu.


Nafsi yangu inatamani sana, naam, hata kuona shauku, kwa ajili ya nyua za bwana; moyo wangu na mwili wangu vinamlilia Mungu Aliye Hai.


Kile anachoogopa mwovu ndicho kitakachompata; kile anachoonea shauku mwenye haki atapewa.


Yeye afuatiaye haki na upendo hupata uzima, mafanikio na heshima.


Nimekuja kwenye bustani yangu, dada yangu, bibi arusi wangu; nimekusanya manemane yangu pamoja na kikolezo changu. Nimekula sega langu la asali na asali yangu; nimekunywa divai yangu na maziwa yangu. Kuleni, enyi marafiki, mnywe; kunyweni ya kutosha, ee wapenzi.


Juu ya mlima huu bwana Mwenye Nguvu Zote ataandaa karamu ya vinono kwa mataifa yote, karamu ya mvinyo wa zamani, nyama nzuri sana na divai zilizo bora sana.


“Maskini na wahitaji wanatafuta maji, lakini hayapo, ndimi zao zimekauka kwa kiu. Lakini Mimi bwana nitawajibu, Mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha.


Kwa maana nitamimina maji juu ya nchi yenye kiu, na vijito vya maji juu ya ardhi iliyokauka; nitamimina Roho wangu juu ya watoto wako, nayo baraka yangu juu ya wazao wako.


Kwa hiyo hili ndilo asemalo bwana Mwenyezi: “Watumishi wangu watakula, lakini ninyi mtaona njaa; watumishi wangu watakunywa lakini ninyi mtaona kiu; watumishi wangu watafurahi, lakini ninyi mtaona haya.


Kwa kuwa mtanyonya na kutosheka katika faraja ya matiti yake; mtakunywa sana, na kuufurahia wingi wa mafuriko ya ustawi wake.”


Nitawaburudisha waliochoka na kuwatuliza walio na huzuni.”


Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, bali matajiri amewafukuza mikono mitupu.


Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashibishwa. Mmebarikiwa ninyi mnaolia sasa, kwa sababu mtacheka.


Ole wenu ninyi mlioshiba sasa, maana mtaona njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, maana mtaomboleza na kulia.


Lakini yeyote anywaye maji nitakayompa, hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji yakibubujika uzima wa milele.”


Msishughulikie chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye Mungu Baba Mwenyezi amemtia muhuri.”


Siku ile ya mwisho ya Sikukuu, siku ile kuu, wakati Isa akiwa amesimama huko, akapaza sauti yake akasema, “Kama mtu yeyote anaona kiu na aje kwangu anywe.


Kamwe hawataona njaa wala kiu tena. Jua halitawapiga wala joto lolote liunguzalo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo