BWANA Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
Methali 3:18 - Swahili Revised Union Version Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu anayeshikamana naye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hekima ni mti wa uhai kwa wote wampatao; wana heri wote wanaoshikamana naye. Biblia Habari Njema - BHND Hekima ni mti wa uhai kwa wote wampatao; wana heri wote wanaoshikamana naye. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hekima ni mti wa uhai kwa wote wampatao; wana heri wote wanaoshikamana naye. Neno: Bibilia Takatifu Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia; wale wamshikao watabarikiwa. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia; wale wamshikao watabarikiwa. BIBLIA KISWAHILI Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu anayeshikamana naye. |
BWANA Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
BWANA Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;
Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.
Ana heri mtu yule anisikilizaye, Akisubiri sikuzote malangoni pangu, Akingoja penye vizingiti vya milango yangu.
Kwa maana ulinzi wa hekima ni kama ulinzi wa fedha na ubora wa maarifa ni kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.
katikati ya njia yake kuu. Na upande huu na huu kando ya ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.