Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Methali 18:21 - Swahili Revised Union Version Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ulimi una nguvu ya kufanya hai na kuua; wanaopenda kuutumia watakula matunda yake. Biblia Habari Njema - BHND Ulimi una nguvu ya kufanya hai na kuua; wanaopenda kuutumia watakula matunda yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ulimi una nguvu ya kufanya hai na kuua; wanaopenda kuutumia watakula matunda yake. Neno: Bibilia Takatifu Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi, nao wanaoupenda watakula matunda yake. Neno: Maandiko Matakatifu Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi, nao waupendao watakula matunda yake. BIBLIA KISWAHILI Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake. |
Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya.
Mmelima dhuluma, mmevuna uovu; mmekula matunda ya uongo; kwa maana uliitumainia njia yako, na wingi wa mashujaa wako.
Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.
katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo?
Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.
Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolezwa chumvi, ili mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwahadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu;