Methali 16:18 - Swahili Revised Union Version Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kiburi hutangulia maangamizi; majivuno hutangulia maanguko. Biblia Habari Njema - BHND Kiburi hutangulia maangamizi; majivuno hutangulia maanguko. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kiburi hutangulia maangamizi; majivuno hutangulia maanguko. Neno: Bibilia Takatifu Kiburi hutangulia maangamizi, roho ya majivuno hutangulia maanguko. Neno: Maandiko Matakatifu Kiburi hutangulia maangamizi, roho ya majivuno hutangulia maanguko. BIBLIA KISWAHILI Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko. |
Basi Hamani akaingia. Mfalme akamwambia, Afanyiwe nini yule ambaye mfalme apenda kumheshimu? Hamani akasema moyoni mwake, Ni nani ambaye mfalme apenda kumheshimu kuliko mimi?
Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia.
Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.
Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.
Ikawa alipokuwa akiabudu katika nyumba ya Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza, wanawe, wakampiga kwa upanga; wakakimbilia nchi ya Ararati; naye Esar-hadoni, mwanawe, akatawala baada yake.
Kuhusu kuogofya kwako, Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Ushikaye kilele cha milima; Ujapofanya kiota chako juu sana kama tai, Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.
Na mwenye kiburi atajikwaa, na kuanguka, wala hapana atakayemwinua; nami nitawasha moto katika miji yake, nao utawala wote wamzungukao pande zote.
Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.
Nayo nchi ya Misri itakuwa ukiwa na jangwa; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA; kwa sababu amesema, Mto huu ni wangu, nami nimeufanya.
Atakapokwisha kuchukua lile jeshi, moyo wake utatukuzwa; naye atawaangusha makumi ya maelfu; lakini hataongezewa nguvu.
Ndipo kile kiganja cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa.
akaja yule aliyewaalika wewe na yeye, na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma.
Vema. Yalikatwa kwa kutoamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune, bali uogope.
Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuri.