Esta 7:10 - Swahili Revised Union Version10 Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema10 Naye, Hamani akauawa hapo kwenye mti wa kuulia aliokuwa amemtayarishia Mordekai. Basi, hasira ya mfalme ikapoa. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND10 Naye, Hamani akauawa hapo kwenye mti wa kuulia aliokuwa amemtayarishia Mordekai. Basi, hasira ya mfalme ikapoa. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza10 Naye, Hamani akauawa hapo kwenye mti wa kuulia aliokuwa amemtayarishia Mordekai. Basi, hasira ya mfalme ikapoa. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu10 Kwa hiyo wakamtundika Hamani mahali alipokuwa ameandaa kwa ajili ya Mordekai. Ndipo ghadhabu ya mfalme ikatulia. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu10 Kwa hiyo wakamtundika Hamani mahali alipokuwa ameandaa kwa ajili ya Mordekai. Ndipo ghadhabu ya mfalme ikatulia. Tazama sura |
Basi Zereshi mkewe na marafiki wote wa Hamani wakamwambia, Na kitengenezwe kiunzi cha mti wa kunyongea wa urefu wa mikono hamsini, na kesho asubuhi useme na mfalme ili Mordekai atundikwe juu yake; ndipo utakapoingia kwa furaha pamoja na mfalme karamuni. Basi ushauri huu ukamridhisha Hamani, akautengeneza mti wa kunyongea.
Kisha mfalme akarudi kutoka katika bustani ya ngome hadi mahali pa karamu ya divai. Ikawa Hamani amejitupa chini penye kitanda alipokuwapo Esta. Mfalme akasema, Namna gani! Je! Atamfanyia malkia jeuri hata machoni pangu nyumbani mwangu? Na neno lilipotoka kinywani mwa mfalme, wakamfunika uso Hamani.