Na nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yako. Nacho kiti chako kitaimarishwa milele.
Methali 12:7 - Swahili Revised Union Version Waovu huangamia, hata hawako tena; Bali nyumba ya mwenye haki itasimama. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waovu huangamizwa na kutoweka kabisa, lakini jamaa ya waadilifu hudumishwa. Biblia Habari Njema - BHND Waovu huangamizwa na kutoweka kabisa, lakini jamaa ya waadilifu hudumishwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waovu huangamizwa na kutoweka kabisa, lakini jamaa ya waadilifu hudumishwa. Neno: Bibilia Takatifu Watu waovu huondolewa na kutoweka, bali nyumba ya mwenye haki husimama imara. Neno: Maandiko Matakatifu Watu waovu huondolewa na kutoweka, bali nyumba ya mwenye haki husimama imara. BIBLIA KISWAHILI Waovu huangamia, hata hawako tena; Bali nyumba ya mwenye haki itasimama. |
Na nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yako. Nacho kiti chako kitaimarishwa milele.
Jina lako na litukuzwe milele, kwa kusema, BWANA wa majeshi ndiye Mungu juu ya Israeli; na nyumba ya mtumishi wako, Daudi, itaimarika mbele zako.
Mfalme akaamuru ifanyike vivyo hivyo, mbiu ikapigwa huko Susa, wakawatundika wale wana kumi wa Hamani.
Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho.
Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo, Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo.
Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.